Nguvu ya ushoga Israel: Baada ya Meya, sasa Waziri shoga maarufu ateuliwa

Jee taifa la mungu,kizazi teule,watoto barikiwa wa mungu wamekuaje tena??


Waziri wa kwanza anayeshiriki wazi mapenzi ya jinsia moja ateuliwa Israel

Mwanaume wa kwanza kutangaza wazi kuwa anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja ameteuliwa kuwa waziri na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Amir Ohana, kutoka chama cha Natanyahu cha Likud , amemteua kama kaimu waziri wa sheria kufuatia kufutwa kazi kwa mtangulizi wake.

Bwana Ohana, mwenye umri wa miaka 43, ni mfuasi sugu wa Netanyahu , ambaye aliunga mkono hatua za kumlinda waziri mkuu dhidi ya kushtakiwa.

Uteuzi wake unakuja siku kadhaa baada ya bunge kuvunjwa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mpya.
Bwana Netanyahu alimfuta kazi waziri wa sheria aliyekuwepo madarakani , Ayelet Shaked, miezi mitatu iliyopita.

Chama cha Shake ,ambacho kilikuwa sehemu ya serikali ya muungano wa Netanyahu, hakikupata viti vya kutosha kukiwezesha kurejea bungeni katiika uchaguzi wa mwezi Mei.

Waisrael watafanya tena uchguzi mwezi wa Septemba baada ya Bwana Netanyahu kushindwa kupata uungaji mkono wa kutosha kutoka kwa vyama kumuwezesha kuunda serikali ya mpito.

Ikitangaza utuzi wake, ofisi ya waziri mkuu ilisema kuwa Bwana Ohana ambaye ana taaluma ya sheria ni mwenye uelewa mkubwa sana mfumo wa sheria''

Bwana Ohana ni mfuasi sugu wa Netanyahu, na ametumia juhudi zake zote kuunga mkono muswada tata uliomuwezesha waziri mkuu aliyeko madarakani kuwa na kinga ya kutoshtakiwa.

Bwana Netanyahu anachunguzwa kwa madai rushwa na ufisadi na anaweza kushtakiwa miezi michache ijayo .Anakanusha vikali shutuma dhidi yake.

Bwana Ohanani mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja , ambaye anatetea ndoa za jinsia moja, jambo ambalo halitambuliki nchini Israeli isipokuwa kwa wale watakaoamua kufunga ndoa yao nje ya nchi . Mwaka jana apinga muswada wa sheria uliopiga marufuku ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja kwa kuzingatia utambulisho.

Ingawa haki za wapenzi wa jinsia moja zinapingwa na jamii ya Wayahudi nchini Israeli, kwa ujumla taifa hilo limekuwa na mafanikio katika kucommunity zenye sheria inayowalinda wapenzi wa jinsia moja .

My take:Wafuasi wa imani B kazi mnayo maana sasa sielewi kitabu chenu kikoje maana hawa ni watoto wa mungu kabisa

Source:BBC SWAHILI
Piga mswaki kwanza kabla yakuongea ongea.

Israel ni taifa teule hadi msaafu umeandikwa hivo, ukihukumu hukumu kwa madhaifu yao binafsi na si vinginevyo.

Au ujui kama kuna Ufir**ji (ushoga) wakutisha kwa waarabu je tuhukumu quran kuwapa daraja la juu?
 
Wewe kinachokuuma nini?
hili ndilo tatizo la waislamu mnataka watu wote wawe na imani kama yenu kitu ambacho daima hakitawezekana.

Israel sio religion state kama Saudia, Iran, Algeria n.k ni secular state ndio maana kuna amani

Msipende kuropoka vitu msivyovijua, hujui uliza ujibiwe na sio kuropoka tu.


لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَدْ تَبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَنْ يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِنْ بِاللَّهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انْفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ



Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet´ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
 
Siuungi mkono, lakini si kwamba Israel hakuna mabaya yapo mengi tu na haimaanishi yanafanywa na watu wote.

ndio maana nikakupa taarifa sahihi kuwa Israel sio religion state ni secular.
iran kuna dhambi, Saudia kuna dhambi Tanzania kuna dhambi na kote huku kuna mashoga kataa sasa
Pia waelewe nchi takatifu siyo watu ni ardhi ya eneo hilo husika, watu wanaweza kuwa wachafu nchi ikawa safi ni uelewa tuu
 
Back
Top Bottom