Nguvu ya Umoja

Nguvu ya Umoja

F R D NOVO

Member
Joined
Jul 23, 2025
Posts
15
Reaction score
25
Hapo zamani za kale, katika msitu mdogo uliokuwa umejaa matundu ya panya na majani mabichi, aliishi paka mmoja mjanja na mwenye hila nyingi. Paka huyu alijulikana kama Bwana Koma, na alikuwa tishio kubwa kwa panya wote wa msituni. Kila alipohisi njaa, alijificha kimya kimya na kuwinda panya mmoja mmoja, akiwaangamiza bila huruma.

Panya walikuwa wengi, lakini walikuwa na tatizo moja kubwa—hawakuwa na umoja. Kila mmoja alifikiria maisha yake tu. Wengine waliishi kwa kuonya wenzao, lakini bila vitendo. Mikutano ilifanyika lakini kila mmoja alikuwa anaogopa kuchukua hatua. “Tutauawa kama tutamshambulia paka,” walinong’onezana.

Siku moja, hali ilizidi kuwa mbaya. Panya waliona ndugu zao wakitoweka mmoja baada ya mwingine. Walifanya kikao cha dharura pangoni mwa Kiongozi wao, Mzee Mdomo-Mkavu. Panya mdogo aliyeitwa Komeo alisimama na kusema kwa sauti ya ujasiri:

“Umoja ni silaha yetu pekee! Kama kila mmoja atashika sehemu ya paka, hata yeye hatatuweza!”

Baada ya mvutano kidogo, walikubaliana. Wakaandaa mpango wa kumvamia Bwana Koma pangoni kwake usiku wa manane.

Mpango ulifanyika kama ulivyopangwa. Panya zaidi ya hamsini walivamia pangoni. Wengine wakamshika miguu, wengine mikono, wengine sikio lake refu, wengine mkia wake mrefu uliokuwa ukiwatishia, wengine wakang’ang’ania sharubu zake, na mmoja akamshika pua yake ndefu kwa nguvu. Bwana Koma akapiga mayowe ya kuomba msaada—lakini hakuwa na msaada wowote. Wale aliohisi ndio walinzi wake hakika hakuwaona, Kwa mara ya kwanza, alihisi uchungu wa kushindwa.

Panya walimfundisha adabu, wakamtoa nje ya pango na kumwambia:

“Huu ni msitu wetu! Kuanzia leo, hatutakubali tena mateso!”

Bwana Koma alikimbia kwa uoga, akapotea msituni na hakurudi tena.

Tangu siku hiyo, panya waliishi kwa amani, na walijifunza kwamba umoja ni silaha kali kuliko makucha ya paka mmoja.

:Kwa hisani ya watu wa mataifa:
 
Back
Top Bottom