Nguvu ya uma yashusha bei za bidhaa kenya!!!

apa tz poa tu
mda si mrefu lita moja mafuta itakuwa 3000
simpatiii pcha bib yangu maposen uko itakuwaje km hatanunua kibiriti kimoja sh 500 sjui.....dah
poa tuchek ivo ivo mzigo ukiwa mkubwa ........
 
Huku kwetu tunanung'unikia chini chini tu,hakuna harakati zozote zinazochukuliwa nasi kupambana na hali hii,kama mabwege vile.....
 
Huku kwetu tunanung'unikia chini chini tu,hakuna harakati zozote zinazochukuliwa nasi kupambana na hali hii,kama mabwege vile.....
Hii issue ni global babu!....hata mamtoni vyakula bei juu,au unataka kuandamana kutaka misaada?
 
Hii issue ni global babu!....hata mamtoni vyakula bei juu,au unataka kuandamana kutaka misaada?

Please stop such kind of sweeping statements!!! Mamtoni gani unayoizungumzia wewe? Usitetee ujinga Bwana!!!!

Tiba
 
Please stop such kind of sweeping statements!!! Mamtoni gani unayoizungumzia wewe? Usitetee ujinga Bwana!!!!

Tiba
Anasema ukweli. Word Food Program walishaonya hili na ndio matokeo hasa ya yale ya kule North Africa na Middle East. Europe (wanakotumia euro) inflation sasa hivi ni above 2% ambayo huwa ni target inakaribia 2.8% wanafikiria kuraise interest rates kuease pressure ya inflation lakini inamaana kwa risk ya uchumi kuporomoka tena. Uingereza ni 4% nao huenda wakaraise interest rate next months lakini wanarisk uchumi wao ndani ya spending cut. China licha ya jitihada za kuongeza interest rate mara nne mfululizo bado inflation ni 5.8%. Brasil pia na sehem nyingine ni hivyo. Hii ni global kama alivyosema mchangiaji hapo juu.
 
Kwetu watz wengi ni kama "kobello" tu!!
Kinachonichekeshaga bongo yangu hii hata akitokea mtu wa kutuamsha, tunamuona mkorofi sananu watakuja wakina "kobello" kujenga "hoja" za kuwa hata "mamtoni" hali ni hivyo hivyo.....
Na watu kama wakina "kobello" ndio wafanya maamuzi...
Kuna nini hapo???
 
Anasema ukweli. Word Food Program walishaonya hili na ndio matokeo hasa ya yale ya kule North Africa na Middle East. Europe (wanakotumia euro) inflation sasa hivi ni above 2% ambayo huwa ni target inakaribia 2.8% wanafikiria kuraise interest rates kuease pressure ya inflation lakini inamaana kwa risk ya uchumi kuporomoka tena. Uingereza ni 4% nao huenda wakaraise interest rate next months lakini wanarisk uchumi wao ndani ya spending cut. China licha ya jitihada za kuongeza interest rate mara nne mfululizo bado inflation ni 5.8%. Brasil pia na sehem nyingine ni hivyo. Hii ni global kama alivyosema mchangiaji hapo juu.

Asante kwa Analysis nzuri....lakini kuna juhudi za makusudi wanajaribu kuchukua kukabiliana na hali halisi..Je hapa kwetu wizara na asasi nyingine zimefanya au zinafanya nini kutuleta unafuu,... maana toka uchaguzi umekwisha bei zimepaa tu
 
Bunge linajadili kwa jazba kupanda kwa gharama za maisha kenya.kbc live.

mkuu nami nimetoka kuangalia bunge la kenya sasa hivi.. yani kila mtu anaangalia maisha ya watu wa chini hoja zinajadiliwa kwa kina tena kwa point na spika yuko makini kutetea wananchi sio hapa kwetu bunge la kipuuzi watu wanaleta ushabiki wa kijinga na mipasho hata kwenye hoja za msingi, ni upuuzi, utumbo na ujinga kwa watu kukaa pale bungeni kwa kodi zetu then wanalinda maslahi yao tu... inakera sana bana

huyu mama aangalie mwenzake wakenya anaendeshaje bunge sio lile group lake la taarab analoongoza pale dodoma!! am pissed off
 
Pamoja na tatizo la kuporomoka kwa uchumi hii hali ya middle east inaigharimu saana dunia. Uzalishaji mwingi na usafiri pia unategemea mafuta kwa kiasi kikubwa saana. Kwa Tanzania tungewekeza kwa nguvu zote kwenye kilimo tuweze kuzalisha chakula cha kutosha na mapambano yawe katika mafuta. Kwahiyo kwenye usafiri tungehangaika na bei ya mafuta na kuhakikisha barabara zinapitika ili kupunguza gharama za usafiri. Lakini kwa bei ya mafuta kwa sasa serikali haina cha kufanya. Maana hata wakiamua kupunguza kodi, inamaana shughuli nyingine za serikali nazo zitakwama. Pia ipo haja ya kurekebisha miundombinu kwa haraka na watu wengi zaidi watumie usafiri wa umma badala ya gari binafsi ili kupunguza akiba ya fedha ya kigeni inayopotea kwenye mafuta.
 
Hivi nyie mnasoma habari za dunia?....au at least mna information zozote za kimataifa?....Au ni mashabiki tu? MNATIA AIBU!
 
Hivi nyie mnasoma habari za dunia?....au at least mna information zozote za kimataifa?....Au ni mashabiki tu? MNATIA AIBU!

mkuu, sio kila mtu ana uwezo wa kufuatilia habari za kimataifa.. Kuna matatizo ya lugha, na hata shughuli za ofisini kuwa nyingi...sasa unapokuja na sentensi kama hii, tukueleweje..wewe mwenyewe umekuja hapa JF kupata taarifa ambazo hauna..
 
True! and i'm sorry if I sounded harsh,ila watu wengine wanapinga vitu ambavyo viko very obvious!
 
Hivi nyie mnasoma habari za dunia?....au at least mna information zozote za kimataifa?....Au ni mashabiki tu? MNATIA AIBU!

Naomba nikupe elimu ya bure kwa lugha rahisi na nyororo, ebu angalia mfano huu halafu jibu utajijibu mwenyewe.
Kama familia yako nyumbani inaishi kwa mlo mmoja kutokana na wewe kuacha kiasi kidogo cha pesa ya matumizi kwa kisingizio cha hali ngumu uliyonayoani kipesa, lakini bado kila siku unarudi nyumbani umelewa chakali na vilevile mtoto wako huwa akipita bar jirani anaona wewe ndio hodari wa kuagiza round na nyama choma, hivi familia yako inaweza kukuamini kwamba maisha ni magumu kwa sababu huna pesa?
Hiyo ndio serikali ya ccm inayohubiri matatizo kila siku lakini matendo yao yako wazi, hayafanani na mtu mwenye shida. kuwapa wabunge milioni 90 ili wanunue magari utasema nchi ina matatizo? zipo gari mpya na zenye hadhi ambazo hazizidi milioni 30 kwa nini serikali isiagize hayo magari kutoka kiwandani moja kwa moja? huitaji degree kujuwa kinachoendelea hapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom