Nguvu ya shirika la Kijasusi la kanisa Katoliki duniani na Tanzania

Kwanza sii kweli Jesuit ni shirika la kijasusi la Kanisa Katoliki, japo lilipoanzishwa, ni kweli lilifanya ujasusi, ila baadaye likabadilika na sasa linaongoza kwa kutoa elimu.

Kuhusu ujasusi, kwa taarifa yako, wale wote walioitwa wavumbuzi, explorers ni majasusi na walidhaminiwa na makanisa!. Wamisionari wote ni majasusi!, wanabalozi wote ni majasusi!, wawekezaji wengi tuu ni majasusi!, hata humu jf tuna members kibao ni majasusi!.

Pili sii kweli ukipingana na ukatoliki umepigana na Uhai wako!, wako Wakatoliki kibao walioasi na leo wanaendelea kuishi!.
  1. Padri Felician Mkwera ni Padri wa Katoliki, amepgana Ukatoliki, ameanzisha kundi la Wanamambi na anaendelea kuishi!.
  2. Askofu Zakaria Kakobe alikuwa Mkatoliki, amepigana na Ukatoliki ameanzisha kanisa lake la FGBF na anendelea kuishi!.
  3. Mtume na Nabii, Josephat Mwingira alikuwa Mkatoliki, amepingana na Katoliki kaanzisha Ephata na yupo!.
  4. Mzee wa Upako, Anton Lusekelo alikuwa Mkatoliki, ameanzisha kanisa lake la Upako pale Ubungo na yupo!.
  5. Padri W.P Slaa, ni Padri wa Katoliki, kapingana na useja, akaacha Upadri, na leo ni mwanasiasa na yupo!.
  6. The list goes on....
Hivyo usilete uongo huu, ila pia niliwahi kuuliza humu, Kwanini, Rais wa Tanzania, akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?!, uzi ule ulifutwa fasta ila Julius alikuwa Mkatoliki, Benyamini naye ni Mkatoliki, hivyo aliyepaswa kufuata mwaka huu, 2015 alikuwa ni awe Bernado, Petiro, au Yahane!, ila Eduarado amekubaliwa kutumbukiza pua kwa sababu Regina ni Mkatoliki, ndio maana hamsikii juhudi zozote kutoka kwa Samwilu! au Federiko!.

Na kufuatia Ukatoliki huu, hata majina kama Januari, Anderea ni majina ya kikatoliki!.

Pasiko
Hajasema ukipingana na ukatoliki umepingana na uhai...wewe ni mwanazuoni unatakiwa uwe makini sana unapomkoti mtu.. amesema"ukipingana na ukatoliki umepingana na uhai WAKO KIROHO"... Hivyo majina yote hayo umeorodhesha ni bure
 
Yericko Nyerere
Pengine umedandia bodaboda usiyojua ilikotoka na inakoelekea ndio maana umeandika tu bila kujua kitu chenyewe, mambo kama haya kama huyajui vizuri usichukue ya vijiweni kisha ukaushangaza ulimwengu.

Historia ya maisha ya wamonaki kwa maisha ya kiroho ya watawa wanaume na wanawake ambao kiutaratibu wamegawanyika katika mafungu mbalimbali kadiri ya shughuli zao kwa kanisa na ulimwenu kama:
  1. Wakaa ndani tu kazi yao kusali na kufunga kwa ajili ya kanisa na ulimwengu.
  2. Wanaofanya kazi za kitume kwa kanisa na ulimwengu katika afya, elimu na maendeleo ya jamii.
  3. Kuna wanaofanya huduma za kuzunguka sehemu mbalimbali katika nchi na dunia kwa shughuli mbalimbali za kitume na maendeleo.

Historia inaonyesha jinsi maisha hayo ya kitawa/kimonaki yalivyoanza zamani sana hata kabla ya Yesu, na alichofanya Yesu kufunga siku arobaini hakikuwa kigeni katika utume wa maisha ya kiroho.

  • Musa alifunga na kusali chini ya mlima Sinai na kisha kutokea na Mungu alipokabidhiwa amri kumi za Mungu.
  • Histoira ya maisha ya watawa imetoka mbali kuanzia na mfano Yesu alipofunga siku arobaini jangwani na kisha kujaribiwa na shetani kisha akashinda.
  • Kuna baadhi ya dini katika mashariki ya kati kama Ubuda na Ujaini nazo zinao utaratibu kama huo wa kutafakari upwekeni hadi kufikia kiwango cha juu kijulikanacho kama "NIRVANA" mtu anayatafakari hushtukia ameshachukuliwa kama pepo kuangama angani akiendelea kutafakari na kusali.
  • Kwenye dini ya uislamu watu kama hao wapo pia ambao hujulikana kama 'MASUFII' waswafi na wanaishi maisha kama ya watawa wa kikristo ila hawapo wengi na inaelekea siku hizi kutojulikana sana na wengi ni wenye msimamo mkali sana katika idikadi za dini yao.

Hivyo tunaona kumekuwepo na utaratibu kama huo katika mapokea ya kanisa kuanzia na agano la kale katika dini ya kiyahudi ambayo ni chimbuko la Ukristo duniani.

Katika agano jipya hali iliendelea na wengi wakaa peke wakifunga na kusali maskani yao yalikuwa pangoni chakula cha kukirimiwa na wengine au kuokoteza mimea kando ya mapango yao.

Mmojawapo ni Mtakatifu Benedict wa Nursia ambaye alitoka katika familia yenye uwezo ya kitajiri kule italia, lakini alipokuwa masomoni alichukizwa na mienendo ya vijana wenzake na akatorokea pangoni kusali na kufunga hadi mtawa wa mapangoni mwengine Romanus akatokewa na ndoto kwamba kuna mwenzake katika pango ana njaa na ilikuwa Pasaka akaenda kumpa chakula na hapo akaanza kujulikana. Hayo yalitokea mwaka 529 baada ya Kristo.

Kanisa likaanza kuwatambua hao wakaa peke kwa kufunga na kusali kwa ajili ya kanisa na ulimwengu, hivo kanisa likaamua kuweka utaratibu wa kuwatambua rasmi katika kanisa. Yapo mashirika makubwa ambayo ni ya kipapa na yapo mashirika ambayo ni ya kijimbo yote yakiwa na nadhiri za:
  1. Usafi wa moyo (maisha ya kuepa na kutotenda dhambi, ya useja ipo ndani ya fungu hilo).
  2. Utii kwa shirika na kanisa
  3. Ufukara - kutohodhi mali na kama ipo ni mali ya shirika na mwanashirika hana haki kuitumia apendavyo ila kwa ruhusu ya shirika na kwa manufaa ya shirika, kanisa na ulimwengu.

Orodha ya mashirika Kikatoliki ya kitawa duniani;

Achana na kuchukua ya vijiweni jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza na pengine likakuvunjia heshima yako uliyo nayo hapa JF. Nimekuonyesha utitiri wa mashirika ya kitawa ya utume wa kusali na kufunga, huduma kwa kanisa na dunia katika nyanya mbalimali za maombezi, huduma kanisani, mahospitalini, elimu na maendeleo. Hawa ndio wanaofanya kazi za kanisa na huduma zinazotolewa na kanisa for free bila malipo ila posho za kujikimu kimaisha tu na cho chote walinachona au kupata ni mali ya shirika na kanisa.
Umeandika maneno mengi lakin utopolo mtupu!! Na mbaya zaidi unataka kuonyesha mtoa mada hajui kitu wakati wewe unaongelea vitu tofauti! Hapa tunaongelea Shirika la Kijasusi la Kanisa katoliki- JESUIT. Wewe unatuletea sijui mastory gani hapa! Ingekuwa mtihani ungepata zero! Next time soma swala vizuri kabla ya kujibu
 
Kwanza sii kweli Jesuit ni shirika la kijasusi la Kanisa Katoliki, japo lilipoanzishwa, ni kweli lilifanya ujasusi, ila baadaye likabadilika na sasa linaongoza kwa kutoa elimu.

Kuhusu ujasusi, kwa taarifa yako, wale wote walioitwa wavumbuzi, explorers ni majasusi na walidhaminiwa na makanisa!. Wamisionari wote ni majasusi!, wanabalozi wote ni majasusi!, wawekezaji wengi tuu ni majasusi!, hata humu jf tuna members kibao ni majasusi!.

Pili sii kweli ukipingana na ukatoliki umepigana na Uhai wako!, wako Wakatoliki kibao walioasi na leo wanaendelea kuishi!.
  1. Padri Felician Mkwera ni Padri wa Katoliki, amepgana Ukatoliki, ameanzisha kundi la Wanamambi na anaendelea kuishi!.
  2. Askofu Zakaria Kakobe alikuwa Mkatoliki, amepigana na Ukatoliki ameanzisha kanisa lake la FGBF na anendelea kuishi!.
  3. Mtume na Nabii, Josephat Mwingira alikuwa Mkatoliki, amepingana na Katoliki kaanzisha Ephata na yupo!.
  4. Mzee wa Upako, Anton Lusekelo alikuwa Mkatoliki, ameanzisha kanisa lake la Upako pale Ubungo na yupo!.
  5. Padri W.P Slaa, ni Padri wa Katoliki, kapingana na useja, akaacha Upadri, na leo ni mwanasiasa na yupo!.
  6. The list goes on....
Hivyo usilete uongo huu, ila pia niliwahi kuuliza humu, Kwanini, Rais wa Tanzania, akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?!, uzi ule ulifutwa fasta ila Julius alikuwa Mkatoliki, Benyamini naye ni Mkatoliki, hivyo aliyepaswa kufuata mwaka huu, 2015 alikuwa ni awe Bernado, Petiro, au Yahane!, ila Eduarado amekubaliwa kutumbukiza pua kwa sababu Regina ni Mkatoliki, ndio maana hamsikii juhudi zozote kutoka kwa Samwilu! au Federiko!.

Na kufuatia Ukatoliki huu, hata majina kama Januari, Anderea ni majina ya kikatoliki!.

Pasiko
Mwingira hakuwahi kuwa mkatoliki,alikuwa mlutheri
 
Kitendo cha kuambiwa usioe au kuolewa ili ufalme kazi ya Mungu ni falsafa ya hali ya juu!! Na ukakubali? Huoni ndio waliosuka?
 
Tangu mwanzo wa Kanisa kulikuwa na Wakristo walioshika maisha ya useja na pengine walianzisha jumuia.

Kufuatana na mifano ya Yesu Kristo na Bikira Maria, Agano Jipya linatoa habari za wanaume na wanawake waliojinyima ndoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, kama vile mabinti wanne wa Filipo waliokuwa mabikira na manabii (Mdo. 21:9). Hasa mtume Paulo aliwahimiza Wakristo wowote wanaoweza wafanye hivyo kama alivyofanya mwenyewe kwa kufuata shauri la Bwana (taz. 1Kor 7:25-34).

Mababu wa Kanisa kuanzia karne I waliandika juu ya wanaume waseja wanaozungukazunguka ili kuhubiri, na juu ya mabikira ambao utakatifu wao unaonyesha Ukristo ulivyo bora kuliko ulimwengu wa anasa unaoliudhi Kanisa.

Nje ya Dola la Kirumi (Mesopotamia na Persia) useja ulitazamwa kama agano na Kristo la kuwafaa wote.

Polepole mabikira walianza kuorodheshwa na kukubaliwa na askofu na kukusanywa katika jumuia. Ilitokea vilevile kwa wanaume wa toba walioanzisha miundo kamili kuliko juhudi za nyumbani mwao, wakishika ufukara fulani wa hiari, mafungo, kujinyima vyakula mbalimbali, kukesha usiku, kuimba Zaburi na kusali kwa moyo.

Karne XX, ngumu kwa Kanisa na kwa dunia yote, ilileta mangamuzi mapya hasa katika maisha ya ulimwenguni. Kwa mara nyingine walei walichangia sana hali mpya ndani ya Kanisa Katoliki, ya kuthamini na kushughulikia mambo ya kidunia.

Katika juhudi za kuratibu nyanja zote za maisha ya binadamu, baadhi walijisikia haja ya kuwekwa wakfu bila ya kujitenga na maisha ya kawaida.

Polepole Kanisa likafikia uamuzi wa kuwakubalia (1950) mashirika ya kilimwengu ambayo waamini wanawekwa wakfu wawe chumvi, mwanga na chachu kati ya watu. Hivyo wanajitahidi kuwa na moyo wa kujikana na bidii ya kitume kama watawa, lakini pia utaalamu wa kisasa na urahisi wa kupenya mazingira yoyote kama walei.

Kanisa Katoliki duniani lipo imara kufuatia uimara wa shirika lake la kjasusi la Jesuiti ambalo kwa maana halisi ni idara ya ulinzi na usalama ya kanisa Katoliki duniani. Mataifa mengi duniani yanaendesha mifumo yao ya idara za ulinzi kwa kuakisi mfumo wa Jesuiti, hii inasimama mpaka nchini Tanzania. Shirika hilo kwa kiwango kikubwa ndilo linaloamua dunia itawaliwaje.

Shirika la Yesu (kwa Kilatini Societas Iesu, kifupi S.J. au S.I. au SJ au SI) ni shirika kubwa la watawa wanaume 19,216 katika Kanisa Katoliki, lililoenea katika nchi 112 za kontinenti 6.

Wanashirika wanaitwa Wajesuiti na ni maarufu pia kwa elimu yao ya juu katika fani mbalimbali, za kidunia na za kidini.

Mwanzilishi wake ni Ignas wa Loyola ambaye, kisha kuacha jeshi, alifuata kwa juhudi zote maisha ya kiroho na kutunga Mazoezi ya Kiroho ili kuongoza watu wamfuate Yesu Kristo.

Mwaka 1534, Ignas alikusanya vijana sita wakaweka nadhiri za ufukara, useja mtakatifu na utiifu, halafu ile ya kumtii daima Papa.

Miongoni washirika wenye nguvu ndani ya Wajesuiti ni Papa Francis,
Papa Francis au Kardinali Jorge Mario Bergoglio, alizaliwa Desemba 17, 1936 mjini Buenos Aires, Argentina. Ni mfuasi wa Shirika la Wajesuiti tangu mwaka 1969 na alisomea Argentina na Ujerumani. Alipewa ukardinali mwaka 1998.

Na kwa Tanzania miongoni mwa makazi yao wakuu ya wa ujasusi ni Arusha, Dodoma na Dar Es Salaam, Pia kasisi Method Kilain ni miongoni mwa waliopikwa kupitia shule za Wajeisuti ambapo Juni 1985-Juni 1990 Padre Method alitumwa kwenda Roma kujifunzia shahada ya juu ya Kanisa katika Chuo Kikuu maarufu cha wajesuiti cha Gregoriana ambapo baada ya kupata shahada ya M.A (Licence) ya somo hilo aliendelea na kupata shahada ja juu ya udaktari (PhD) katika somo hilo,ilikupata shahada hiyo aliandika kitabu juu ya historia ya kanisa katika Kagera (Bukoba na Rulenge).

Ukipingana na Ukatoliki, umepingana na Uhai wako Kiroho!
Hujaeleza ujasusi wake hapa ukoje. Wanafanya mini, mfano hapa Tanzania. Wanafanya hivyo ili iweje? ......
 
Sio kwamba unapingana na uhai wa kiroho peke yake, na wa mwili pia. Jamaa tulikuwa nae jana, leo haonekani. Wewe endekea kupinga imani za watu.
 
Kwanza sii kweli Jesuit ni shirika la kijasusi la Kanisa Katoliki, japo lilipoanzishwa, ni kweli lilifanya ujasusi, ila baadaye likabadilika na sasa linaongoza kwa kutoa elimu.

Kuhusu ujasusi, kwa taarifa yako, wale wote walioitwa wavumbuzi, explorers ni majasusi na walidhaminiwa na makanisa!. Wamisionari wote ni majasusi!, wanabalozi wote ni majasusi!, wawekezaji wengi tuu ni majasusi!, hata humu jf tuna members kibao ni majasusi!.

Pili sii kweli ukipingana na ukatoliki umepigana na Uhai wako!, wako Wakatoliki kibao walioasi na leo wanaendelea kuishi!.
Hivi bro unajua "mission behind" unajua hii sio bahati mbaya?
Ujasusi una mambo mengi bro take my words
 
Pasco na Yericko

hebu niambieni

1. Kwa nini wazungu na hususana wa Ulaya hawapendi na hawana jazba na mambo ya dini?

2. Kwa nini Ukristo na hususan Ukatoliki hauna nguvu Ulaya?

3. Kwa nini Wazungu hawana muda na mambo haya? kwa nini sisi yunaendekeza.sana haya mambo? je yana mahusiano yoyote na maendeleo?
Wazungu wamegundua dini ni stori kama stori zingine ila hapa kwetu ni chanzo cha ajira, uporaji mfano kuingiza magari na vifaa vingine kwa mlango wa dini ili kukwepa kodi, kupitisha sembe etc
 
Back
Top Bottom