Akasankara
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 4,099
- 5,604
Kuna vijana wameandaliwa na ofisi ya ccm kupotosha kwa makusudi hali halisi ya nchi. Viwanda vimejifia kifo kibaya
Huyu nae eti ana akili!Ajira mbona kaachia,hujaona za madaktari 1000 na baada ya hapo walimu wanaajiri.
www.tamisemi.go.tz
www.moh.go.tz
Achana na huyo anaejiondoa akiliMagufuli wakati akihutubia kwenye mkutano wa mat alikili kuwa Kuna madaktari 5000 mtaani afu zinatolewa ajira 1000 nanchi inauhaba mkubwa wa madaktari huoni Kama Kuna tatizo??? acha kuwa mpambe kwa kila jambo
Vipi vile viwanda vilivyokuwa vinazinduliwa kila kukicha vimekomea wapi ndugu MATAGA?Ajira mbona kaachia,hujaona za madaktari 1000 na baada ya hapo walimu wanaajiri.
www.tamisemi.go.tz
www.moh.go.tz
Hata wakija wataandika nini?Naona kwenye lineup ya uu uzi mataga hata sub hawapo hii mechi ngumu aisee
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukurupukaji na kutohusisha wataalam jambo baya sana, afu cha ajabu yeye mawazo yake hayapingwi na ye yoteBusara zilikuwa ziaze ktk kufufua mazo ya biashara kwanza ili kuvutia uwekezaji ktk viwanda, Pia tuanze kufufua viwanda vyote alivyoanzisha Mwalimu. Badala yake tukaanza mkakati wa kujenga viwanda vipya bila dira ya aina yoyote! Tumeishia kuhesabu vyerehani na machine za kufyatulia matofali kama viwanda! Shame!
Na hakuna wa kuhoji hilo iwe serikani au kwenye chama wote wameufyataToka waziri wa ujenzi mpaka rais wa ujenzi... Kiukweli tunaenda kiporojo tungejua kupima ahadi na utekelezaji wake tungegundua tume
Tuliambiwaa inawekwa nguvu viwanda vya nguo tuachane na mtumba lkn wapi?
Tunatakiwa tuwe na viwanda vya samaki kwakuwa tunavyanzo vingi imeishia stories hatuoni lamaana.
Nchi ya viwanda tuliyosisitiziwa imeishia kuwa ya hadithi za kesi,kufungana,kutiana marisasi na sumu.
Wafanyakazi wataboreshewa maisha hamna lolote ni kufukuzwa ovyo,kutishwa na kutoendelezwa hata kwa seminars,workshop etc.
Kinachofanyika sasa ni kuchukua hela na kujenga sio kubezi kwenye kukuza uzalishaji,ufanisi,elimu bora kama mataifa yaliyoendelea walivyo base
Huyo ni MATAGA au MAZAGA???!!!Vipi vile viwanda vilivyokuwa vinazinduliwa kila kukicha vimekomea wapi ndugu MATAGA?
Kiukweli ccm wanatutia hasara sana kwenye nchii tutakuwa tunafanya kazi ya mark time hadi lini? kila rais wa ccm anakuja na vyake,binafsi sikuona haja ya Magu kuvuruga kila kitu alichokikuta bali angerekebisha alipoona hapafanyi vizuriNgoja waje wale waliopangwa zamu ya leo waje wakanushe kila kitu ulichokisema. Lakini waswahili wana msemo wao, mficha maradhi kifo humuumbua.
Kama kwenye viwanda tumerudi nyuma, kama kwenye kilimo cha mazao hasa ya biashara hatufanyi vizuri kuanzia uzalishaji, kuchakata na hata kuuza nje, kama uvuvi umeathirika na viwanda vya uchakataji samaki vimefungwa na orodha ni ndefu ni nini sasa kinaendelea kwenye uchumi wetu!!!?
Zisipochukuliwa hatua za haraka na za makusudi kabisa kuokoa hali, basi ni suala la muda tu tutakua na crisis ya kiuchumi. Biashara za ndani nazo bado hazijarudia hali yake ya miaka mitano iliyopita. Hata miundombinu inayojengwa kama kutakua hakuna marekebisho muhimu ya sera, sheria na nia ya dhati bado mchango wake hautaonekana sana kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Hata mke wa lutu aligeuka jiwe Kwa kuanza kumbuka ushenzi uliokuwa ukifanyika Gomola na Sodoma,Lazima nikiri bila unafiki kuwa hakika Magufuli katuangusha sana wanaccm tumebaki kutumia nguvu kubwa katika propaganda na matumizi ya nguvu.
Awamu ya JK ilikuwa na mabovu mengi, lakini yalikuwepo mazuri ambayo ndiyo ilipaswa kuyaendeleza kwa nguvu, lakini tuliyapuuza yote na kumfanya Magu kuwa ni mteule wa Mungu huku tukidanganya hili au lile ili kumpamba.
Kilemba cha ukoka hakidumu maana kinanyauka, sasa tumebaki kutumia nguvu kubwa kwa wapinzani ili kuficha udhaifu wake na kulazimisha wananchi wamuelewe positively.
Ukweli lazima tukubali kuwa kwa hali ya sasa ikiundwa Tumehuru ya uchaguzi na wenzetu wakiweka mgombea imara kama yule tuliyetaka kumtoa kwenye mzunguko na amekimbilia nje basi kupata 30% ya kura za urais tutakuwa tumejitahidi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
General welfare ya watu imeshuka chini kuliko miaka 5 iliyopita kila ripoti inaonyesha wabongo ni kati ya watu tusio na furaha duniani..mniambie miradi mipya ya barabara ambayo awamu ya tano wameiasisi na imekamilika ukiacha walizokuwa wanamaliziaDuh yani mwaka 5 no mshahara mpya ase ingekuwa kipindi cha jk sa hv tungekuwa mbali sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Magufuli 4 lifeeeeNakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.
Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.
Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.
Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.
Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.
Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.
Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.
Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!
Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.
Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.
Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.