Nguvu ya Msamaha - The Power of Forgiveness

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,490
5,525
Sote tumewahi kufanya makosa na tunafahamu jinsi hisia ya ukosefu inavyouma. Hii hali ya kujisikia kwamba una hatia ni moja kati ya hisia zenye maumivu makali sana. Pamoja na ukweli huo lakini bado maumivu hayo hayafikii maamuzi anayopata yule uliyemkosea hasa pale anapokataa kusamehe.

Mtu anapofanyiiwa kosa huwa na uchungu mkubwa sana moyoni. Hudhilika na kuumia sana kwa yale aliyofanyiwa. Maumivu ya kutendewa kosa ni maumivu makali sana. Jaribu kufikiri maumivu unayopata unapoonewa au kutendewa jambo baya na mtu uliyamuamini na kumthamini utaelewa ukubwa wa maumivu haya.

Maumivu ya kutenda au kutendewa jamo baya huwa yana tiba moja tu. MSAMAHA sio kujifanya hujui, sio kujificha, sio kukimbia wala sio kukana hapana ni MSAMAHA-FORGIVENESS

Msamaha una mambo mengi sana ila kubwa kabisa ni kwamba MSAMAHA una NGUVU kubwa sana. MSAMAHA unakupa uhuru,amani na utulivu. Msamaha unakupa nafasi ya kuendelea na maisha yako. Msamaha unakupa nafasi ya kujenga mahusiano mapya. Msamaha unakupa mwanga mpya. MSAMAHA unakufungulia BARAKA.

Ukweli ni kwamba Aliyefanyiwa kosa huwa ndiye anafaidi zaidi pale anapotoa msamaha na siyo aliyetenda.ALiyetenda bado atabaki na deni kwani kutoa msamaha ni process ndefu ila kuomba msamaha ni process ndefu zaidi.

Mtu anapoomba msamaha anakuwa anajaribu kutua mzigo na Unapomsamehe unakuwa umemtwisha na mzigo wako ili aubebe yeye. Yaani ni kama mtu kakukuta na ndoo ya maji kichwani na yeye ana yake kisha ukachukua ndoo moja kubwa ukajaza maji yenu wote ukampa abebe na wewe ukachukua ndoo tupu mbili ukabeba wewe. Hiyo ndio nguvu ya Msamaha. Mtu akikukosea muonye na akiomba msamaha msamehe. Usikubali kubeba mizigo ya watu.

Kuna wale ambao huwa hawaombi msamaha kabisa. Hao wewe waambie ukweli kwamba wamekukosea na uwape msamaha wa bure kabisa kwani hakuna sababu ya kubeba uchafu kwenye nafsi yako.

Msamaha ni muhimu kwa afya yako ya kihisia, kiakili na kimwili.

Nakutakia siku njema
 
Kweli mkuu, nguvu ya msamaha humfanya mtesi wako ajifiche,akimbie au atafute namna ya kua karibu na wewe tena.

Ni ukweli usiopingika kwamba kusamehe ni ujasiri usiopimika wala kulinganishwa.
 
Tuchukulie T.Lissu kupigwa Risasi ndio somo yetu ya Msamaha.

Au Kusalitiwa kwenye mahusiano iwe ndo somo

... Mtoa mada.. Nguvu yako ya msamaha ulomanisha hapa itasimamaje??.

Tuachen masihara, kuna watu wanakufanyia ubaya na bado wanadunda kwelikweli..

JINO KWA JINO.
 
Tujifunze kusamehe na kusahau japo kusahau ni ngumu hususan akikuumiza unayemuamini
 
Kuna mjinga mmoja nataka nimuombe msamaha lakini kahama na simu zote hazipatikani.. Huko aliko anajiona wa maana sana anaposikia nateseka kwa sababu ya maamuzi yake.. Anyway karma is a bitch
 
Dah mimi kuna mtu (mwanamke)alichukua simu yangu akatoa airtel money laki tatu, sijajua aliijua vipi namba yangu ya siri, nikamkamata nikampeleka polisi, akaahidi kuilipa baada ya mwezi yaani tarehe10 ya mwezi ujao, sema hakuomba msamaha na alichukulia kama alichotenda ni haki tuu hapa najiuliza asipolipa hiyo siku nipande naye mahakamani au ndio niapply hii kitu?
 
Pol
Kuna mjinga mmoja nataka nimuombe msamaha lakini kahama na simu zote hazipatikani.. Huko aliko anajiona wa maana sana anaposikia nateseka kwa sababu ya maamuzi yake.. Anyway karma is a bitch
Pole mkuu,samehewa uwe huru
 
Watu niliowaamini na kuwathamini (ndugu) waliniumiza sana, niliteseka na yale maumivu mpk pale nilipoamua kuwasamehe Niko poa kwa Sasa ila ninaishi nao kwa tahadhari sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom