Nguvu ya kitanda

Nguvu ya kitanda

Upande wa pili je? Comfory ya kulala?

1/3 ya maisha yetu inakuwa spent kitandani tumelala. Hatuna budi kuhakikihha tunajinyoosha vizuri kwa afya.
 
Na hivi zisofa vyumbani sjui huwa vinagundi yaani mpka kuja kumpandisha demu kitandani kama taifastars inacheza imeshachapwa 4
 
Acha hiyo ya 6x6 Nyumba nyingine wanakuwa na vitanda viwili chumbani. Cha Baba na cha mama. Sasa ndugu yangu kama wamewashiana Moto panakuwa pagumu. Kwa sababu zifuatazo;
1; kama ugomvi au msuguano ulianza mchana ndio Basi tena, maana usiku hakuna kwenda kwa mwenzake. Na hiyo ndio inafanya mahusiano kuwa magumu zaidi.
Itabidi anayetaka mahusuano yarudi Basi itabidi AJIKOMBE KWA MWENZAKE.

2, Kama valangati mmelianzisha usiku huko chumbani, hapo napo pagumu itabidi Huduma za KUNUNIANA zianze usiku huo kwa kila mtu na kitanda chake mpaka siku mambo yawe shwali au mmoja AJIKOMBE kwa mwenzake.

ANGALIZO; Mfumo huu huleta adabu kidogo kwa sababu kila mtu anajua LIKIHALIBIKA suluhu Ni ngumu kutokana na umbali WA vitanda😁
 
Eti kisa alininunia mchana,ndio asubuhi na barid hili la makambako eti niogope kutaka mambo??!!mimi huyu huyu kabisa??!labda sijashikwa!hata kama vitanda ni viwili.ujinga wa kumvutia mdomo mwanamke sonata aisee
 
Mie kibeseni niko kimya, nafaidi na kimeo changu. LAKINI NIMECHEKA KIMOYOMOYO.

KATIBA MPYA MALI YA WANANCHI
 
%"NGUVU YA KITANDA" %

Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5. Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha.

Hiyo iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala. Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.
Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu.

Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugomvi?

Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugomvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kumpapasa mwingine.

Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremala avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.
 
Huu ndio mwendo wa sasa
tapatalk_1541918332340.jpeg
 
Back
Top Bottom