Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, si wa holela tu kama akina Ng'wana Malundi. Soma hapo chini kama ulikuwa humjui Ng'wana MalundiHii hoja inaacha maswali mengi kuliko majibu....mfano tu yaan nguvu ya kafara ni kubwa kiasi kwamba Mungu alishindwa kuiondoa kiasi kwamba yesu akaja kuuwawa kama kafara? How powerful is God then?
Lakin kuna mahala unasema akazaliwa yesu asiyeweza kufa...swali...zile siku 3 alikuwa amelala??
Nahitaji msaada kuelewa.
Nimepata somo zuriView attachment 1191882
Sehemu ya II
Maana katika viumbe wote pamoja na Malaika, Mwanadamu ndiye kiumbe Bora kabisa kuliko wote aliyewahi kuumbwa na Mungu. Naam, Mwanadamu ni bora zaidi ya Malaika.
Kama ilivyoandikwa “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake” (zaburi 8:1-9)
Pamoja na Hayo, upo utafauti wa Thamani kati ya damu ya mtu na mtu. Mtu akitoa sadaka ya kafara ya mtu aliye mpenda zaidi, kafara yake huwa na Nguvu zaidi kuliko kama angemtoa ndugu yake asiyempenda.
Hii ni Kananuni ambayo ingawa Waganga na wachawi huitumia, Pia hata Mungu ameitumia (Yohana 3:16)
Tatizo ni kwamba Ubora huo wa Mwanadamu uliingia Dosari kwa Adamu kutenda Dhambi.
Hivyo yale mamlaka na utukufu wake ukashuka. Kama ilivyaondikwa “wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23)
Mwanadamu akawa anaweza kufa, Hivyo Binadamu akawa mdogo punde kuliko malaika. Malaika wakawa juu ya mwanadamu kasababu ya Mauti.
Kama ilivyoandikwa “tunamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti” (Ebr 2:9).
Kwahiyo kitendo cha Yesu kukubari kufa Mauti kilimfanya ajishushe zaidi hata kuwa mdogo Punde kuliko malaika.(wafilipi 2:5:8). (Maana Malaika hawana mauti).
Sasa ili uwepo ukombozi na Utakaso kwa wanadamu wote na kuwafungua kutoka kwenye vifungo vya maagano ya uovu waliyoingia kwa sadaka mbalimbali, ikiwemo maagano yaliyofungwa kwa kafara za watu;
Ilitakiwa iwepo Dhabihu bora zaidi kuliko zote.
Ndipo Mungu akaamua Kumtoa Yesu azaliwe nje ya Mfumo wa Dhambi, Bila kuhusisha Sperm na Egg Cell za Wanadumu, ili asilisi dhambi kama ambavyo wanadamu wote wanarithi Dhambi kupitia Egg and Sperm Cells za wanadamu.
Mungu akiona haya, na akijua kabisa kuwa katika damu pia upo urithi wa Dhambi, ndiyo maana Tangu mwanzo alitengeneza Tumbo la Mwanamke kiasi kwamba Damu ya Mama na ya mtoto havichangamani.
Ndiyo maana Mama anaweza kuwa na Ukimwi lakini Mtoto asiambukizwe kama wakati wa kuzaliwa hakukutokea mchubuko.
Kwasababu Dhambi hurithiwa kupitia Egg and Sperm Cells, Ilibidi aje Mwanadamu mwingine ambaye hatapitia Uzao wa Mapenzi ya wanadamu.
Atokee Mtu mwingine aliyetengwa na dhambi ya Asili ya Adamu.
Kama Malaika alivyomjibu Mariamu akasema
“Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Luka 1:35)
Hivyo Mariamu tumbo lake likatumika kama Incubator kwa ajili ya kukuza mwili wa Yesu.
Lakini Damu ya Bikara Maria (aliyekuwa na dhambi ya asili, maana naye alizaliwa kama wanadamu wengine),
wala sperm cell ya mwanaume haikutumika, naamu haata yai la Bikira maria nalo halikutumika.
Kwahiyo akatokea Mtu duniani yaani Yesu, Aliyetengwa na Dhambi ya Adamu, Asiye weza kufa (maana kifo kiliingia kwasababu ya dhambi), na kwakuwa hana asili ya Dhambi, Mauti ilikuwa haina Nguvu juu yake.
Pia mtu Huyu Yesu thamani ya Uhai wake ikawa juu ya damu zote za wanadamu wengine. Yeye alikuwa hana Dosari.
Na kwasababu DNA ya Damu yake ni ili ya Mungu, Thamani ya Damu na Uhai wake ikawa ni thamani ya Mungu mwenyewe.
Hivyo Thamani ya Damu ya yesu ni thamani ya uhai wa mungu mwenyewe.
Kama Yesu mwenyewe alivyosema “kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake” (Yohana 5:26)
Kwahiyo huyu Yesu akawa ndiye Mtu Bora kabisa Duniani, Mwana Pekee wa Mungu anayependwa sana Na Mungu, asiye na Dosari yoyote.
Kama yohana Mbatizaji Alipomuaona akasema “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”
Nayo Imeshuhudiwa na Roho Mtakatifu kwa kusema;
“Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;” ambaye “kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa“ (Ebr 7:26, 9:14)
Sasa ili Yesu aweze kufa, ilibidi awe na Dhambi ili Mauti iwe na Nguvu. Lakini kwasababu hakuwa na Dhambi, ikabidi apokee dhambi zetu.
Na kwa hizo dhambi zetu kwa kuzipokea akiwa msalababi, Yeye akafa.
Na kwa Jinsi hiyo dhambi zote za ulimwengu zimeondelea, kwa kila atakayemwamini Yesu, Dhambi zake zinafutwa, na badala yake anapewa Uzima wa Milile.
Kwa damu yake, Hakuna agano au kafara ambayo inaweza kuishanda damu ya Yesu.
Damu ya Yesu imesafisha hadi vitu vya Mbinguni pia.
Kama ililvyoandikwa
“katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi, ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; (Ebr 9:22-24)
Na kwa jinsi hiyo Yesu akaunganisha Mbingu na Dunia kuwa kitu kimoja, kwa wale walio mpokea.
Kama ilivyoandikwa
“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. …, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;” (Efeso 1:7-10)
Haki yote ya Mungu imetimizwa na ukombozi umethishwa kupitia msalaba wa Yesu. Na kila ampokeaye Yesu Moyoni mwake, amepata ukombozi.
Kwa njia ya Damu ya Yesu, Maagaono yote aliyofunga mtu huvunjwa kwa hiyo damu Bora kuliko damu yoyote ile Mbinguni na Duniani. Pamoja na hati zote za Mashitaka zilizokuwa kinyume nawe, zili zilitokana na Dhambi au maagano ya vizazi na Vizazi. Zote zilibatilisha pale msalabani.
Kama ilivyoandikwa
“ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” (Col 2:13-15)
Jambo Moja usisahau,
Baada ya kuokoka Hakikisha umebatizwa, Maana ni katika ubatizo unapozamishwa na kutolea ndani ya Maji, katika ulimwengu wa Roho unakuwa umetangiza Enzi na Mamlaka na Fulme zote za Giza kuwe wewe ni wa Yesu.
Ndipo hapo unapounganishwa katika kutembea kwa Haki (justice) katika upya wa Uzima ambao Yesu anautumia sasa.
Kama hujui Nguvu na kazi ya ubatizo soma HAPA na HAPA
Pasipo kubatizwa, Mamlaka na Enzi za Giza bado zitajaribu kukusumbua na kutumia Historia ya maagano na dhambi za kale kujaribu kukurudisha katika ufalme wa Giza.
Kwasababu ni kwa kubatizwa ndipo unafanya Public decralation katika ulimwengu wa Roho na Maliaka kuwa sasa wewe umeunganika katia mauti na ufufuo wa Yesu.
Bila hivyo ndio maana wengine wanasumbuliwa na maagano kila siku ingawa wamevunja katika maombi kwa damu ya Yesu mala kwa Mala. Lakini yanaonekana kana kwamba bado hayakuvunjwa kwasababu umekataa kutimiza haki yote.
Sioni JINSI YESU ALIVYOWAKOMBOA WANADAMU..mbona dhambi ndo Kwanza zinaongezeka??? Huwa hainiingii akilin hata chembe kusema WANADAMU WALIKOMBOLEWAHapa ndipo kwenye fumbo kuu kuhusu ufalme wa Mbinguni; ni kweli kulikuwa hakuna njia yoyote ile ya kuokoa ulimwengu huu ulio katika dhambi bila damu ya Yesu kumwagika; ambaye ndiye mwana pekee wa Mungu.
Yesu aliyajua yote hayo kwamba ni lazima auwawe kwa ukombozi wa ulimwengu....alikifuata kifo Yerusalem na akaingia kwa shangwe kubwa...
Lakini kumbuka siku kadhaa kabla ya kusurubiwa kwake alikwenda kusali na wanafunzi watatu seniors Yakob, Yohana; Petro - Yesu aliomba sana na kusema " Baba kama itakurahisha basi kikombe hiki na kiniepuke" lakini jibu lilikuwa hakuna namna. Btn - walitokea Elia na Mussa hawa mitume wa Mungu na kumtia moyo..
Na ni kweli ndugu unadhani bila damu ya Yesu hivi maisha yetu yangekuwaje? Shetani si angekuwa mfalme wa ulimwengu!! Watu wote tungemsujudia yeye kwani tusingekuwa na kisingena kitu cha kutusaidia yaani damu ya Yesu Kristo ama Roho Mtakatifu.
MT. 26:39-46 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba ...
... akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Ukombozi hauji automatically mjomba; hapa duniani hatuishi kwa bahati hapana bali kuna Sheria ambazo lazima uzifuate, na msingi wa sheria hizi ni HAKI.Sioni JINSI YESU ALIVYOWAKOMBOA WANADAMU..mbona dhambi ndo Kwanza zinaongezeka??? Huwa hainiingii akilin hata chembe kusema WANADAMU WALIKOMBOLEWA