Nguvu ya CHADEMA mitandaoni imeenda wapi?

Toka lini ccm mkaitakia mema CHADEMA???
Kwanza kuedelea kumtaja Dk Slaa na CHADEMA ni kuonyesha namna mlivyozoea kufanya siasa nyepesi!
Dk Slaa hata angekuwemo ndani ya CHADEMA mpaka leo kwa style ya utawala wa mwendazake katika hiki kipindi cha miaka 5 wala asingewezafanya lolote, zaidi angeishia kutekwa au kushambuliwa kwa risasi 32 !
Tumeshuhudia viongozi wa upinzani wakizuiwa kufaya mikutano, na hata wale waliofannikiwa kuvuka vikwazo lukuki na kujaribu kuhutubia walishushwa majukwaani katika namna iliyojaa udhalilishaji mkubwa!
Ilifika mahala DC anavamia hadi kikao cha ndani na kukaa kusikiliza kinachajadiliwa ilihali sio mjumbe wa kikao hicho a wala hakualikwa!
Pia unapaswa kutambua kuwa CHADEMA haifanyagi biashara ya kununua watu na kuwaweka mitandaoni wakatukane makda au viongozi wa vyama vingine. kwa hao mliowaandaa humo mitandaoni acha waendelee kufanya kazi mliowatuma, CHADEMA wanajenga chama!
Wana saccos wa Ufipa kwa ushabiki hamjambo.
 
Kuna sababu nyingi, kati ya hizo ni hizi:
1. Chadema kuacha kupigia kelele mahitaji halisi ya wananchi na badala yake kushupalia zaidi masuala ya kisiasa na wanasiasa. Matokeo ikajitenga na wananchi wa kawaida.
2. Chadema kupinga kila kitu. Serikali inafanya jitihada kuboresha huduma kwa wananchi (hospitali, barabara, maji, shule, nk) chadema inapinga kila kitu kwa ajili ya maslahi ya kisiasa. Aliyebuni hii mbinu ya kisiasa akafie mbali kabisa!
3. Chadema kuhusishwa na kutumiwa na mabeberu. Hii imedhihirika wazi zaidi baada ya mgombea wake wa urais lisu kusepa na kuenda kuishi ubeberuni, akirusha vijembe vya kuishitaki nchi mahakamani, tena akitetewa na mawakiri wa kibeberu. Mlitaka wananchi watafute ushahidi gani tena kuamini kuwa chama chenu kinaisaliti nchi kwa kutumiwa na mabeberu?
4. Msiba wa rais Magufuli ndo umemaliza kabisa. Wananchi wanalia na kuomboleza kwa kufiwa na rais wao mpendwa (umati uliojitokeza kumuaga ni ushahidi tosha), tundu lisu anarusha matusi kila kukicha na HAKUNA KIONGOZI WA CHAMA ALIYEJITOKEZA KUMKEMEA! Wakati wananchi wanahitaji faraja, chadema haikuonekana kabisa kujali hilo hitaji la wananchi.
Hicho kinachotokea huko mitandaoni ndiyo ile waswahili wanasema 'mnavuna mlichopanda'
 
Mbowe achie ngazi umelalamikiwa na wengi,.
ipo siku hao nyumbu unaowalipa kukutetea watachoka.
 
Back
Top Bottom