Nguvu ya CHADEMA mitandaoni imeenda wapi?

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928
1,000
Amani iwe nanyi.

Inasikitisha sana ukifuatilia page na post mbalimbali za Chadema wanavyotukanwa kwenye comments na wachangiaji.

Kuna group linaitwa Chadema in Blood kule Facebook yani kila wanachopost ni kutukanwa tu na watu, huko Instagram ndiyo balaa kabisa, njoo JamiiForums hali ni hiyo hiyo!

Nimeangalia comments za kwenye hotuba ya Mbowe aliyoitoa akisema vibaya utawala wa hayati Magufuli, kwa kweli ni huzuni raia walivyomtukana Mbowe. Swali la kujiuliza Chadema imefikaje huku?

Enzi za Dr Slaa ulikuwa unavaa gwanda la Chadema kwa maringo yote, leo tuvae kwa aibu ya kujifichaficha?

Je, Tundu Lissu ameharibu image ya chama baada ya kuanza kutetea mabeberu?

Je, ni Mbowe ameharibu image ya chama baada ya kuwa anaangushwa na Konyagi anasingizia amepigwa na wasiojulikana? Au ule uongo wake wa kuibia familia inapompeleka mahakamani anasingizia amefungiwa akaunti zake na serikali?

Hili wimbi la wafuasi wa Chadema kutukanwa mitandaoni chanzo ni nini?

Kiukweli inahitajika tathimini ya haraka sana kuikoa na kuirudisha Chadema kwa wananchi ili waiamini tena kama zamani.
 
Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
9,787
2,000
Ule wimbo wa mabeberu umerudi tena? Anyway, Kilichotokea sasa hivi ni kwamba watoto wengi wamekua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao, watoto hao ndio wamekuwa vinara wa kutukana, na hii inatokana na ukweli kwamba kizazi cha sasa, kizazi cha singeli... Kizazi kina Paula.

Kizazi cha kina Harmonize na Rayvan ni hybrid flani tofauti na ile ya waliozaliwa 1995 kurudi nyuma! 90% of them wamesoma shule za kata hivyo wao uwezo wao wa akili kuchakata mambo uko tofauti sana ndiyo maana sasahivi unaona mambo ya ajabu mitandaoni, na hii sio kwenye siasa tu, hadi kwenye Mpira, angalia vizuri mashabiki wa SIMBA Kwa miaka hii ya Manara wakoje! Wakipokea habari kuhusu timu yao wanaipokeaje iwe positive au negative, utajifunza kitu!

Kuhusu zama za Dr. Slaa, hawa wote wanaotukana most of them walikua nursery school na primary chini ya darasa la 5! Hivyo kizazi cha sasa ni tofauti na kizazi cha nyuma yake, wao ni kama mbuzi kwenye msafara, ukiweka mti mbele ya njia mbuzi wa kwanza akaruka, wa pili akaruka then ukatoa ule mti, mbuzi wote waliosalia wataruka ilhali mti ushatoka!

Mbaya zaidi wao wanapokua na kuanza kupata akili wanakutana na utawala wa JPM uliozuia kuhoji, kwahiyo kizazi hicho anapojitokeza mtu kuhoji lolote wanamuona ni muasi maana wao wamekua wakiona na wakiaminishwa Kwamba JPM ni Mkombozi na hatakiwi kuhojiwa Kwa lolote na wanaleta hilo pia Kwa uongozi wa sasa!

Inshort Kwa sasa Mitandaoni ndio sehemu pekee unapoweza kukutana na ujinga wooote ambao kama ingekua mnakutana physically na kundi hilo la watoto hata usingetaka wapite karibu yako mbali hata kutotaka salam zao.
 
mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
871
1,000
Toka lini ccm mkaitakia mema CHADEMA???
Kwanza kuedelea kumtaja Dk Slaa na CHADEMA ni kuonyesha namna mlivyozoea kufanya siasa nyepesi!
Dk Slaa hata angekuwemo ndani ya CHADEMA mpaka leo kwa style ya utawala wa mwendazake katika hiki kipindi cha miaka 5 wala asingewezafanya lolote, zaidi angeishia kutekwa au kushambuliwa kwa risasi 32 !
Tumeshuhudia viongozi wa upinzani wakizuiwa kufaya mikutano, na hata wale waliofannikiwa kuvuka vikwazo lukuki na kujaribu kuhutubia walishushwa majukwaani katika namna iliyojaa udhalilishaji mkubwa!
Ilifika mahala DC anavamia hadi kikao cha ndani na kukaa kusikiliza kinachajadiliwa ilihali sio mjumbe wa kikao hicho a wala hakualikwa!
Pia unapaswa kutambua kuwa CHADEMA haifanyagi biashara ya kununua watu na kuwaweka mitandaoni wakatukane makda au viongozi wa vyama vingine. kwa hao mliowaandaa humo mitandaoni acha waendelee kufanya kazi mliowatuma, CHADEMA wanajenga chama!
 
Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,000
2,000
Chadema wanapaswa kuwa wajanja Sana, kunaupepo ambao si lazima wao waufuate Kwa nyuma, upepo ambao ni lazima kutumia akili kubwa kuuthibiti tena Kwa hoja na sio Kwa vioja

Najua watanitukana hapa, Upepo wa JPM R.I.P, pamoja na mapungufu yake, walipaswa kuuendea Kwa busala ya Hali ya juu!!

Mti wa matunda, hauli matunda yake

Shauri yenu
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,036
2,000
Amani iwe nanyi.

Inasikitisha sana ukifuatilia page na post mbalimbali za Chadema wanavyotukanwa kwenye comments na wachangiaji.

Kuna group linaitwa Chadema in Blood kule Facebook yani kila wanachopost ni kutukanwa tu na watu, huko Instagram ndiyo balaa kabisa, njoo JamiiForums hali ni hiyo hiyo!

Nimeangalia comments za kwenye hotuba ya Mbowe aliyoitoa akisema vibaya utawala wa hayati Magufuli, kwa kweli ni huzuni raia walivyomtukana Mbowe. Swali la kujiuliza Chadema imefikaje huku?

Enzi za Dr Slaa ulikuwa unavaa gwanda la Chadema kwa maringo yote, leo tuvae kwa aibu ya kujifichaficha?

Je, Tundu Lissu ameharibu image ya chama baada ya kuanza kutetea mabeberu?

Je, ni Mbowe ameharibu image ya chama baada ya kuwa anaangushwa na Konyagi anasingizia amepigwa na wasiojulikana? Au ule uongo wake wa kuibia familia inapompeleka mahakamani anasingizia amefungiwa akaunti zake na serikali?

Hili wimbi la wafuasi wa Chadema kutukanwa mitandaoni chanzo ni nini?

Kiukweli inahitajika tathimini ya haraka sana kuikoa na kuirudisha Chadema kwa wananchi ili waiamini tena kama zamani.
Unataka kuuliza kwanini magufuli amekuwa sifuri na aibu kubwa ya watanzania? Mainjinia wa hayo ni CDM unayosema imekufa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom