GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Hodi wakuu wataalam wa mambo.
Leo ninahitaji mnisaidie jambo moja kuhusu nguvu iliyopo ndani ya damu inasababishwa na nini?
Damu kimekuwa ni kitu ambacho kinaaminika kubeba maajabu na nguvu za ajabu sana za kutenda mambo.
Mifano yake ni kwamba:-
i/ Damu ya Yesu.
Kuna watu wengi sana wanaamini kuwa damu ya yesu iliyotoka masalani imeweza kuwamboa na bado inaendelea kuwakomboa na dhambi zao.
Wengine mpaka leo wametengeneza vitu mfano wa damu ya Yesu na hunywa vitu hivi wakiwa kwenye nyumba zao za ibada ili kuwakilisha ile damu ya Yesu iliyotoka msalabani. Damu ina nini ndani mpaka ipewe nafasi hii?
ii/ Damu katika kafara.
Kuna watu hutoa kafara ya damu ili kutatua mambo yao yanayowasumbua katika maisha yao ya kila siku. Damu ina kitu gani kinachoweza kutatua matatizo ya watu?
iii/ Damu kama kinywaji.
Inasemekana kwamba wachawi hunywa damu kama kinywaji ambacho huwezesha mambo yao yaende vizuri. Damu ina nini ndani yake mpaka wachawi wapende sana kuitumia? Tena mpaka wamewekeana zamu ya kuchangia damu hizo.
iv/ Damu katika chale.
Waganga na wachawi humpaka mtu dawa sehemu ambayo damu inatoka baada ya kumchanja chale. Chale ina lengo la kutoa damu ili mambo mengine yaendelee kwenye damu hiyo. Damu ina nini special sana wakuu?
v/ Kiapo cha damu.
Kuna watu hapa duniåni hufanya viapo vya damu na ukisaliti kiapo hicho basi lazima upatwe na mabaya.
Mambo ni mengi sana kuhusu damu. Sasa swali ni kwamba damu ina kitu gani ndani take mpaka iaminike kuwa na nguvu hizo zote? Wajuzi na wataalam popote mlipo karibuni.
Asanteni