Ngurumo acha kumchafua JK baada ya kukunyima nafasi Ikulu

Ngurumo ni majeruhi wa siasa za mtandao hayuko kwa maslahi ya taifa anagombana na waliomtosa
 
mwandishi makini hawezi kuandika habari moja na ya mtu mmoja kwa miaka 5 ana lake jambo
 
nilishaacha kusoma makala ya Ngurumo baada ya uchambuzi nikagundua ana ajenda ya siri iliyojificha kwa maslahi yake lakini wengi wetu tunamuona ni mwandishi makini tujaribu kufuatilia
 
MBONA KWELI TUPU?Anayekanusha lolote hapo akanushe!
Usihangaike nao,wengi wanaolialia humu ni waandishi wa habari wa mlengo wa salva! Hawawezi kuandika shutuma hizi kama makala kwenye magazeti yao.kwa vile wote tunajificha humu kwa majina feki wanajiona uhuru! Kumbe hata maandishi yao yanawatambulisha.hawana hoja,wajibu hoja za ngurumo basi tuone!!
 
napata kichefuchefu kumjadili Ngurumo hana mpya kwenye uandishi yeye ana ugomvi binafsi na kikwete
 
sikutegemea kwamba mtu kama Ansbert Ngurumo angaweza kuandika habari za kumchafua Rais Kikwete na kubeza yote yaliyofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi

tutakumbuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Ngurumo ni mmoja kati ya watu waliotegemea kupata nafasi ikulu kama shukrani toka kwa Jk na chama cha mapinduzi amekuwa akilalamika kwa muda mrefu baada ya kukosa nafasi hiyo na akasema wazi kupitia mtandao huu wa JF kwamba mtu pekee anayeweza kumshambulia ni Rais Kikwete.
Imbecile@work
 
nilishaacha kusoma makala ya Ngurumo baada ya uchambuzi nikagundua ana ajenda ya siri iliyojificha kwa maslahi yake lakini wengi wetu tunamuona ni mwandishi makini tujaribu kufuatilia
Uandishi ni kuchagua,yeye kachagua taasisi ya Urais,mnataka kila mtu aandike habari za ujenzi wa barabara? Ngurumo ni jasiri ndio maana hawamgusi wala kujibu hoja zake! Jibuni hoja zake basi mbona hamyajibu maandishi yake? Yote ni kweli tupu!
 
Ngurumo anatupeleka kusiko huwezi kujadili ajenda ya mtu mmoja kwa muda mrefu kiasi hicho na kuacha mambo mengi ya msingi kwa maslahi ya nchi kwani ajenda ya Ngurumo inaacha mambo kadhaa ambayo tunatakiwa kuyaweka sawa bila kujali Jk tunamkubali au la
 
Hebu tuangalia mambo mengi aliyosema Ngurumo kama yana uongo, tutajua:

"Chuki ya wazi dhidi ya CCM inasababishwa na maisha magumu waliyonayo wananchi. Udhaifu wa serikali ndio umekiua CCM, maana kimegeuka chama cha viongozi waongo, wasioaminika." TRUE KABISA!


"Ile jeuri ya wanachama na mashabiki wa CCM kutembea kifua mbele wakiwa wamevaa mashati na fulana na kijani na njano mitaani, imenyauka." TRUE KABISA, mfano ni baba yangu mzazi, japo ccm siku hizi hata Tshirt ya kijani ukimnunulia havai!

"Hii ndiyo sababu inayowafanya CCM kuandaa mikutano ya hadhara kwa gharama kubwa mno, ikuhusisha kubeba wananchi kwenye malori na mabasi kutoka sehemu za mbali na kuwaleta mahali pa mkutano, tena baada ya kuwaahidi au kuwagawia pesa au fadhila nyinginezo." TRUE KABISA! imekuwa jadi! hadi kuhudhuria kwenye mikutano ya shina, tawi au kata wanadai posho!

"Sasa hivi hata watoto wadogo wanasalimiana kwa kunyosha vidole viwili, ishara ya ushindi inayotumiwa CHADEMA" hili halina ubishi, nenda hata mtaania ukutane na uangalie watoto wanaocheza uangalia wangapi utasikia wakisema kidumu, ila utasikia salam ya peoplez!

"Sasa hivi hata watoto wadogo wanasalimiana kwa kunyosha vidole viwili, ishara ya ushindi inayotumiwa CHADEMA" hili halina ubishi, nenda mtaani maeneo wanakocheza watoto uone kama utasikia hata mmoja wao akitamka kidumu chama … na uangalie kama utasikia salaam au alama ya peoplez!



"Shule za sekondari na vyuo vya elimu ya kati na ya juu vimejaa wanafunzi wasiokipenda CCM. Katika mazingira haya, CCM kinazidi kukosa mvuto, na wanachama wa CCM wanazidi kupungua." Hili hata kwenye report yao ya kujivua gamba, waliweka kama kiashiria cha kushuka hadhi mbele ya umma!



"Ni miaka sita ya shida na umaskini unaosababisha chuki ya wananchi dhidi ya Rais Kikwete. Hatujasahau kwamba mwaka 2005 Kikwete aliomba kura akiahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Yako wapi? " TRUE KABISA maana hata ile kauli mbiu yao ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya bila fikra mpya na dira mpya, nayo imekufa kibudu kama ahadi ya maisha bora yenyewe! sasa kwa hili Ngurumo karudia tu mambo ambayo yako wazi, hata anaetumia masaburi kufikiri, na mtumwa wa kuchumia tumbo atayaona!

Ukweli uliowazi ni kuwa ccm imekuwa a disappointment! Imewalet watz down siku ilipoamua kuwatelekeza wakulima na wafanya kazi na kukumbatia matajiri! Hata mwalimu alisema siku ikiacha misingi ya kuanzishwa kwake, basi itakufa! Ndio maana wao wenyewe wanakiri hadhi ya ccm imeporomoka na wakaja na usanii wa kujivua gamba, ambalo sasa limegoma!
 
Ngurumo alipolipiwa shule uingereza na mwenyekiti wa chama fulani alipewa jukumu la kummaliza kikwete lakini hataweza atakuwa Rais wake hadi 2015
 
Ngurumo ni mchumia tumbo hamjasikia sasa anataka kuanzisha gazeti baada ya kukosa alichotaka huko alifikiri wanaomtuma wangemlipa fadhila
 
Ni jamaa mmoja hivi mhariri wa Tanzania daima, nasikia Kabla JK hajakataa balozi mmoja toka nchi za ng'amo ambaye alikuwa na mke ambaye ni MTOTO SI RIZIKI, alianza kwa kumkataa NGURUMO kuwa mwandishi wake kwa sababu hiyo hiyo.


ha ha ha kwahiyo unataka sema Ngurumo za radi si Rizki?
 
Watu wengine bwana.maybe walichelewa kutoka tumboni,ndiyo maana akili na mawazo yao yamechelewa hivi.
 
Binafsi Ngurumo sio miongoni mwa waandishi wa habari ninaowakubari ingawa anaweza kuwa anaandika baadhi ya mambo ya kweli lakini namuona ana lengo analolijua mwenyewe si mtu wa kumwamini kwa asilimia 100 kwamba anayoyafanya ni kwa ajili ya sisi sote
 
..........hamna anayemchafua Kikwete; Kuna mawili ama amechafuka tayari au anajichafua mwenyewe, jiongeze kwa jinsi hiyo mkuu
sikutegemea kwamba mtu kama Ansbert Ngurumo angaweza kuandika habari za kumchafua Rais Kikwete na kubeza yote yaliyofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi

tutakumbuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Ngurumo ni mmoja kati ya watu waliotegemea kupata nafasi ikulu kama shukrani toka kwa Jk na chama cha mapinduzi amekuwa akilalamika kwa muda mrefu baada ya kukosa nafasi hiyo na akasema wazi kupitia mtandao huu wa JF kwamba mtu pekee anayeweza kumshambulia ni Rais Kikwete.
 
Back
Top Bottom