Ngurumo acha kumchafua JK baada ya kukunyima nafasi Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngurumo acha kumchafua JK baada ya kukunyima nafasi Ikulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FIKRA MBADALA, Nov 7, 2011.

 1. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikutegemea kwamba mtu kama Ansbert Ngurumo angaweza kuandika habari za kumchafua Rais Kikwete na kubeza yote yaliyofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi

  tutakumbuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Ngurumo ni mmoja kati ya watu waliotegemea kupata nafasi ikulu kama shukrani toka kwa Jk na chama cha mapinduzi amekuwa akilalamika kwa muda mrefu baada ya kukosa nafasi hiyo na akasema wazi kupitia mtandao huu wa JF kwamba mtu pekee anayeweza kumshambulia ni Rais Kikwete.
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mganga njaa tu huyo
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Yaliyofanywa yepi hayo?

  Au ni ile list ndefu ya data za Megawati zitakazojengwa 2014?

  Hongera sana Ansbert kwa kuwa mwandishi huru, na kuheshimu fani ya habari!
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenikumbusha mbali, nikweli alitegemea nafasi pale magogoni tena ni ile aliyonayo SALVA. Anadhani anachofanya ni kulipiza kisasi kumbe ni kuwapotosha wananchi.
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi ngurumo ni nani tena?
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  tegemea ulichokuwa nacho usitegemee utakachotafuta. Nalog off
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @FIKRA MBADALA, Sidhani kama ni sahihi kumshambulia Ngurumo maana hayuko peke yake kuonesha masikitiko, watanzania zaidi ya 80% waliompigia kura ya ndiyo Kikwete are very disspointed. Unakumbuka 'maisha bora kwa kila mtanzania? we've all been duped!
   
 8. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwanamuziki wa msondo ngoma
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni Naibu mhariri mtendaji wa Tanzania Daima ambalo ni la CHADEMA ... si rahisi akaisifia Serikali huyu zaidi ya kuibeza kwa vile bado ana njaa ya kuingia ikulu na anadhani CDM watamsaidia. Fikra za kutumia masaburi.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Yule Gurumo bana

  [​IMG]
   
 11. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kila mtanzania yupo disappointed at the government's staggering movement lakini mleta mada amejaribu kuhusisha kitendo cha JK kumnyima ulaji Ngurumo na mashambulizi ya sasa yanayofanywa na Ngurumo juu ya JK. Nadhani anajaribu kujenga picha juu ya watu ambao huwa wanaipenda CCM kwasababu ya ulaji waliopewa ilihali wanajua kuwa imejaa uozo. Kwanini asubiri hadi anyimwe cheo ndiyo agundue kuwa CCM haifai?
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Muone, kichwa kama CCM!

  Ansbert Ngurumo
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]NAWAHUSUDU, na wakati mwingine nawashangaa sana Watanzania wenzangu wanaojipanga kuomba uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hawa ni watu waliojilipua. Wanahitaji nguvu ya ziada.

  Maana zama zimebadilika. CCM sasa kimekuwa mzigo mzito usiobebeka kwa kila Mtanzania.
  Hata viongozi wa chama, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, wameanza kutambua kwamba kuongoza CCM si jambo la kujivunia tena. Ni changamoto kubwa sana. Ni adhabu!

  Wanachama nao wamefika mahali wanaona aibu kujitambulisha kama wana CCM, kwa sababu wanaogopa kuzomewa. Siku hizi, ukitaka kulinda heshima yako, fiche u-CCM wako.

  Baadhi ya makada maarufu, wakiwamo wabunge, wamekiri kwangu kwamba katika maeneo mengi ya nchi hii, chama hakiuziki, hakibebeki. Wanasisitiza kwamba tofauti na zamani ambapo chama kilikuwa nyenzo muhimu inayotumika kuwabeba wanasiasa wanaogombea uongozi, sasa hivi imefika mahali ambapo wagombea ndio wanatarajiwa kukibeba chama.

  Maana yake ni kwamba ukitaka kugombea uongozi CCM lazima uwe na pesa nyingi za kuhonga wananchi na kununua ushindi, na uwe na uhakika wa kuitumia dola dhidi ya wapinzani wako.

  Ni siri iliyo wazi kwamba wabunge wengi wa CCM waliochaguliwa mwaka jana, walipita kwa sababu ya majina yao, na jitihada binafsi; si kwa sifa ya chama.

  Baadhi ya wale niliozungumza nao, wamekiri kwamba katika majimbo yao, wao ndio CCM – maana ndio wanaokibeba chama badala ya chama kuwabeba wao. Mmoja wao aliniambia kwamba ingawa yeye ni mbunge wa CCM, ana uhakika kwamba pale jimboni kwake hakuna CCM, bali kuna CHADEMA.

  Maana yake ni kwamba wabunge hao wangechaguliwa tu, hata kama wangegombea kupitia chama kingine.
  Tafsiri ya haraka ni kwamba iwapo wabunge hao wa CCM wakihama chama leo, wataondoka na wapiga kura wao.
  Na hii ndiyo tofauti kubwa ya sasa kati ya CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mbele ya umma.

  Kwa asilimia kubwa, chuki ya wananchi dhidi ya CCM imegeuka ushabiki na mapenzi kwa CHADEMA. Pale ambapo kada au mgombea wa CCM anaona aibu kujinadi kwa chama chake, yule wa CHADEMA anajua kuwa asipotumia mwamvuli wa chama kujinadi anakuwa na nafasi ndogo ya kushinda.

  Ile jeuri ya wanachama na mashabiki wa CCM kutembea kifua mbele wakiwa wamevaa mashati na fulana na kijani na njano mitaani, imenyauka.

  Ndiyo maana kada mmoja wa CCM aliyekuwa mstari wa mbele katika uchaguzi mdogo wa Igunga aliniambia kuwa ilifika mahali wakagundua kwamba kijani chao ni nuksi, kinachukiwa na kitawanyima fursa ya kufanya kampeni kwa amani.

  Akasema, "Tuligundua hilo, tukawa hatuvai mashati na fulana za kijani, bali tunavaa kiraia, ndipo tunapata uhuru wa kupita mitaani na kuomba kura nyumba kwa nyumba."

  Hii ndiyo sababu inayowafanya CCM kuandaa mikutano ya hadhara kwa gharama kubwa mno, ikuhusisha kubeba wananchi kwenye malori na mabasi kutoka sehemu za mbali na kuwaleta mahali pa mkutano, tena baada ya kuwaahidi au kuwagawia pesa au fadhila nyinginezo.

  Ndiyo maana vijana waendesha pikipiki na daladala hawaendi kwenye mikutano ya CCM kwa hiari. Lazima wahongwe mafuta na kupewa pesa ya kula; wakati vijana hao hao hushindana wao kwa wao kununua mafuta na kujaza matanki ya pikipiki au magari yao kwenda kwenye maandamano na mikutano ya CHADEMA.

  Hiii ni sehemu ya maelezo kwa nini CCM hawawezi kushinda bila kutegemea nguvu ya pesa na polisi. Wakati tuliomo ni ule wa chama tawala kuishi kwa kudra za dola, huku upinzani ukikua kwa kasi ya ajabu kwa kudra za nguvu ya umma.
  Miaka kadhaa iliyopita, katika maeneo mengi ya nchi hii, ilikuwa aibu na kejeli mtu kujinadi kuwa mpinzani. Sasa hivi ni jambo lisilo la kujivunia mtu kujitambulisha hadharani kuwa ni mwana CCM.

  Miaka saba iliyopita, wananchi kadhaa huko vijijini waliwahi kuniambia kuwa mtu anayetamani kugombea uongozi, kama ana nia ya kushinda apitie CCM.

  Mwaka huu, wananchi wale wale wamenieleza kwamba kama mtu anataka kushindwa agombee kwa tiketi ya CCM.
  Kama ambavyo baadhi yetu tumesema huko nyuma, CCM kinakufa. Hata hiyo idadi ya wanachama wanayotangaza, milioni nne, haipo. Ni propaganda tu za kisiasa.

  Ikumbukwe kuwa waasisi wa CCM wanazidi kufa. Wengine wanazeeka. Wengine wamekihama chama. Sehemu kubwa ya idadi ya Watanzania ni vijana. Ni wao wamezaliwa miaka ya harakati za mageuzi ya kisiasa. Wengi wao wamejiunga kwenye vyama vya mageuzi. Sasa hivi hata watoto wadogo wanasalimiana kwa kunyosha vidole viwili, ishara ya ushindi inayotumiwa CHADEMA.

  Shule za sekondari na vyuo vya elimu ya kati na ya juu vimejaa wanafunzi wasiokipenda CCM. Katika mazingira haya, CCM kinazidi kukosa mvuto, na wanachama wa CCM wanazidi kupungua.

  Kinawapata wapi hao milioni nne? Kama kina wanachama wengi hivyo, mbona hawakubali kuhudhuria mikutano ya CCM bila kubembelezwa na kuhongwa?

  Kama CCM kingekuwa na idadi kubwa kiasi hicho, CHADEMA kingepata wapi jeuri ya nguvu ya umma?
  Chuki ya wazi dhidi ya CCM inasababishwa na maisha magumu waliyonayo wananchi. Udhaifu wa serikali ndio umekiua CCM, maana kimegeuka chama cha viongozi waongo, wasioaminika.

  Mwaka huu, wakati tunatimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, tunatimiza pia miaka sita ya utawala wa Rais Kikwete.

  Ni miaka sita ya shida na umaskini unaosababisha chuki ya wananchi dhidi ya Rais Kikwete. Hatujasahau kwamba mwaka 2005 Kikwete aliomba kura akiahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Yako wapi?

  Utafiti uliofanywa na taasisi ya takwimu, ya serikali hii hii, kuhusu mapato binafsi ya kaya, unaonyesha kuwa mwaka huo (2005) Watanzania waliokuwa wanakula mara moja tu kwa siku walikuwa asilimia 34 ya wananchi wote.

  Mwaka huu, idadi ya Watanzania wanaobahatisha mlo mmoja tu kwa siku imeongezeka hadi asilimia 41. Maana yake, idadi ya Watanzania wanaoshinda au kulala njaa katika miaka mitano ya Rais Kikwete imeongezeka kwa asilimia saba!

  Hawa wana sababu ya kuiamini CCM? Wana sababu ya kuipenda CCM? Wana sababu ya kuiamini serikali ya Rais Kikwete? Wameyaona maisha bora waliyoahidiwa na JK?

  Utafiti huo huo unaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto wote wenye miaka mitano katika kipindi hichi hicho wamedumaa. Kama wazazi wao wanakula mara moja tu kwa siku, tena kwa kubahatisha, watoto wao watawezaje kukua vizuri na kupata maisha bora? Wazazi wa watoto hawa waliodumaa wana sababu za kushangilia miaka 50 ya utawala wa CCM na sita ya maisha magumu ya JK?

  Taifa la watoto waliodumaa linajivunia miaka 50 ya CCM na sita ya Kikwete? Taifa la namna hii linaona manufaa ya kuongozwa na CCM yenye magamba au isiyo na magamba?

  Takwimu hizo hizo za serikali zinaonyesha kuwa katika kipindi kile kile walichoahidiwa maisha bora, asilimia 54 ya Watanzania wote hawali nyama kabisa!

  Tutawezaje kujivunia afya na usitawi wa watu wetu kama wanakosa hata virutubisho muhimu kama protini itokanayo na nyama?

  Hii ina maana gani kwa taifa linalosemekana kuwa la tatu kwa wingi wa mifugo katika Afrika, ambalo zaidi ya nusu ya watu wake hawali nyama?

  Mambo haya na mengine ndiyo yamewafanya baadhi ya watu kuogopa kujitambulisha kuwa wana CCM. Na sasa nimesikia katika baadhi ya maeneo nchini, CCM imegeuka tusi miongoni mwa vijana. Ukimuudhi mtu siku hizi, akakosa tusi la kistaarabu dhidi yako, atakwambia: "Muone, macho kama CCM!"
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Njaaaaaaaaa inamsumbua. TD ulaji hautoshi.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa nini NGURUMO hataki kuridhika na ajira aliopewa na FREEMEDIA? Acha tamaa hizo, mtu mzima wewe
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwenzako NGURUMO ana chuki binafsi kwa kukosa kuwa mwandishi wa habari wa Rais , sasa wewe unamchukia JK kwa lipi au bendera fuata upepo nini?
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  NGURUMO, katika uandishi wako wa habari una daraja gani manake nashindwa kukupa hata 5% katika uandishi. Nasema hivyo nikitambua wazi kabisa kuwa maneno uliyoyaandika hapa ni maneno ya majungu, chuki binafsi. Watu wa aina yenu , Mwanafalsafa mmoja aliwapa jina la IRONBOYS.

  Ni watu wanaopenda kuongelea watu na siyo maendeleo. Kama unaelewa vizuri, lazima utatambua maneno ya wanafiki kama wewe yanaanzaje, utasikia mara mtu mmoja aliniambia, mara wanasema kwamba, mara utasikia wamekiri n.k ni lazima ujifanye kuwa umepata toka kwa watu, ebu cheki maandishi mekundu hayo unavyojikanyaga.

  Huo ni U-IRON BOYS. NGURUMO, hivi CHADEMA ni nini? au CCM nini. Nasema hivyo kwa sababu nimeona unawasingizia wanachama na makada wa CCM kuwa hakuna tena CCM bali wao ndiyo wamekibeba chama. Unataka kusema , CHADEMA ni kitu tofauti na wana-CHADEMA?

  NGURUMO mimi naamini ni heri kuchagua mtu kuliko chama kama ambavyo wana -CCM walivyo sahihi, hii ni kwa sababu wananchi wanatumikiwa na Mtu na siyo jina la Chama. utaniambia JANUARI MAKAMBA amechaguliwa kwa sababu ya uwezo wake na siyo kwa sababu ya CCM nakubali.

  Sasa niambie SUGU na wenzake wengi wamebebwa na jina la Chama nini ambacho wananchi wanakipata. Hapo napingana na wewe kabisa. Watanzania sasa mmeshagundua kuwa CHADEMA watu wake ni aina ya NGURUMO wanachaguliwa kwa sababu ya jina la Chama, na hapa natahadharisha si kwa sababu ya CHADEMA bali kwa sababu ya kelele za SLAA manake kwa mujibu wa MBUMBUMBU Ngurumo ni dhahiri kwamba CHADEMA na SLAA ni vitu viwili tofauti.

  POLENI kwa kujivunia MA-MBUMBUMBU kama NGURUMO. na kuna haja ya kwenda mbele zaidi tukajua madarasa aliyopitia tukajua alichokuwa akikifanya darasani isije ikawa naye alikuwa akicheza MDAKO na matokeo ndiyo tunayoyapata leo ya sera za U-CAMERON.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni jamaa mmoja hivi mhariri wa Tanzania daima, nasikia Kabla JK hajakataa balozi mmoja toka nchi za ng'amo ambaye alikuwa na mke ambaye ni MTOTO SI RIZIKI, alianza kwa kumkataa NGURUMO kuwa mwandishi wake kwa sababu hiyo hiyo.
   
 18. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,499
  Likes Received: 2,037
  Trophy Points: 280
  mwimbaji wa bendi ya MSONDO NGOMA...
   
 19. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,499
  Likes Received: 2,037
  Trophy Points: 280
  kwani wewe unampenda jk.?
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  MBONA KWELI TUPU? Anayekanusha lolote hapo akanushe!
   
Loading...