Nguo za sikukuu enzi zilee

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
846
432
Nakumbuka enzi zile............... siku chache kabla ya sikukuu kama hizi za Krismas na Mwaka Mpya tulikuwa tukiomba kununuliwa nguo za sikukuu. Endapo mzazi asipokununulia basi sikukuu haina maana kwako!

Mimi niliikuwa nikinunuliwa nguo mpya mfano kama wiki moja kabla then.....kufika siku ya siku kuu tayari ilishachafuka kwani nilikuwa nikijiiba na kuijaribu kila mara!

Mama yangu alikuwa akipenda kutununulia nguo ndefu sana eti........hii utakuwa nayo.....yaani umasikini unasababisha mpaka viatu anakununulia oversize........eti utakuwa navyo........basi ni kuweka mavitambaa, sponji ilimradi tu uweze kutembea!!

Siku moja tukiwa kanisani siku ya maombi mchungaji akaruhusu wenye maombi wayataje iliwaombewe.....basi mtoto wa Mchungaji akasimama akasema........naomba mimi naomba maombi ili Mungu anipatie nguo ya sikukuu!!

Vp ninyi hali yenu ili kuwaje kuhusiana na suala zima la nguo za siku kuu?
 
mie hata sasa bila nguo ya sikukuu hakukaliki
muulize The Finest
keshanunulia nyeupe
 
Dah...enzi hizo bila nguo mpya hapatoshi. Lakini kwa sasa hivi eti nachukia/naona noma kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu! Yaani hata kama nimenunua nguo mpya sitaivaa siku ya sikukuu.
 
Dah...enzi hizo bila nguo mpya hapatoshi. Lakibi kwa sasa hivi eti nachukia/naona noma kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu! Yaani hata kama nimenunua nguo mpya sitaivaa siku ya sikukuu.

kaka ww kama mm huwa najihis kama vile kuvaa nguo mpya xmas/mwaka mpya ni utoto, mi km kawa natinga pamba zangu za siku zote.
 
Dah...enzi hizo bila nguo mpya hapatoshi. Lakini kwa sasa hivi eti nachukia/naona noma kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu! Yaani hata kama nimenunua nguo mpya sitaivaa siku ya sikukuu.

hata mimi sipendi kuvaa nguo mpya sikukuu na huwa navaa nguo za zamani ili eti nisiwe kama mtoto
 
hiyo toka enzi zetu ilikuwepo.
hata leo hii binti yangu ameondoka kwenda huko kwetu
kuwapelekea ndugu wengine nguo za sikukuu.
 
nakumbuka nilinunuliwa BWANGA fagia uwanja nililia toka nyumbani hadi kanisani na kurudi ikabidi waende tena dukani kunichukulia mchelemchele ndo nkanyamaza
 
Hili suala limenikumbusha enzi za utotoni. Kweli ilikuwa raha sana. Mkiwa mnacheza mnaulizana vipi nyie mmeshanunuliwa nguo za sikukuu? Watoto ambao wazazi wao wanachelewa kununua huwa wanakosa raha kabisa. Siku hizi sipendi kabisa kuzoeza watoto hiyo tabia.
 
nakumbuka nilinunuliwa BWANGA fagia uwanja nililia toka nyumbani hadi kanisani na kurudi ikabidi waende tena dukani kunichukulia mchelemchele ndo nkanyamaza

tehetehe....mie nilinunuliwa sketi na blauzi ambazo siyo za resi material siku ya komunio......nililia sana ilikuwa ni siku moja kabla ya tukio kwa hiyo zoezi la kubadilisha halikuwezekana........ nililia sana mpaka kwenye siku yenyewe nikakosa raha.....picha zote nilikuwa nimenuna hata nikiambiwa cheka......nakataa nakunja x.......:lol:
 
Huu uzi inabidi uunganishwe na ule wa TF..hapa sioni kipya!

Hujaona kipya kwenye thread hii .....:juggle:... kwasababu thread hii inazungumzia nguo mpya za enzi zileee......tofauti na ile ya TF's
 
Back
Top Bottom