Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,789
Good morning great thinkers, N sinkers.
Good morning JF. Good morning people!
Matukio ya kuvujiwa nyumba na kuibiwa hali ya kuwa tumeajiri walinzi wa asili na hata wa kisasa huku wengine wakiwa na silaha kali za moto kumesababisha wengine kutokuwa na imani nao tena.
Kufuatia hali hiyo ndio maana wenye uwezo kifedha wameamua kuongeza nguvu na mbwa wenye mafunzo. Na kwa wale wenye kipato cha kawaida wameamua kufuga mbwa kama walinzi waaminifu.
Lakini inakuwaje hata hawa walinzi waaminifu nao wanazidiwa maarifa na kujikuta nao wanalevywa ama kuibiwa kabisa? Kuna kutumia ujanja wa chakula chenye sumu ama madawa ya kulevya.
Lakini mbwa mwenye mafunzo hadanganyiki kamwe. HALI!!!
Akili ya binadamu hailali kila kitu kina mbadala wake. Wewe ukiwaza hivi. Kuna mwenzako anawaza vile. Kama mbwa wako ana mafunzo ya kutokula chochote bila idhini yako. Wenzako wamewaza zaidi ya hapo
Kuna sayansi ya nguvu ya uvutano kati ya mbwa na chatu. Mbwa akishakutana na chatu huishiwa na nguvu na kujikuta anajipeleka mwenyewe bila kupenda mpaka analiwa. Umegundua nini hapo? Kiboko ya mbwa ni chatu.
Hivyo basi siku hizi wezi wanatembea na ngozi za chatu kwenye yale majumba yenye mbwa wakali. Wakifanikiwa tu kuzama ndani na kumwoneshea mbwa wako mwenye mafunzo yote. Hupoteza nguvu zote na kujikuta anaifuata ngozi huku akitoa mate mdomoni na kutikisa tu mkia na kutoa kisauti chenye kutia huruma.
Hapo mwizi atakuwa na uchaguzi. Amuibe na mlinzi mwaminifu? Amuue? Amzimishe kwa muda? Ukiona watu wako busy mikoani kutafuta ngozi za chatu tambua zina matumizi zaidi ujuavyo