Ng'ombe Kipofu Na Aliyevunjika Mguu...

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
NDUGU zangu ,

Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Kwamba ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu. Wote watakufa njaa.

Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng'ombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako, na hata mahala pako pa kazi.

Tumekuwa jamii ya ovyo ovyo. Tunafanya mambo ya ovyo ovyo. Ni kutoka ngazi ya familia hadi ngazi ya kitaifa.

Tubadilike. Na hilo Ni Neno Fupi La Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
3,961
2,000
Ujumbe huu uwe mahususi kwa mjomba wako Philip ambaye kapata cheo juzi na kishaanza kusahau kuwa miezi michache iliyopita ni kama vile hata wembe wa kunyolea ndevu hakuwa na uwezo nao.Kishaanza tambo na kushindwa kujua matatizo ya Tanzania ni umasikini na sio vyama vingi.
 
Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Nov 3, 2012
139
0
Ujumbe huu uwe mahususi kwa mjomba wako Philip ambaye kapata cheo juzi na kishaanza kusahau kuwa miezi michache iliyopita ni kama vile hata wembe wa kunyolea ndevu hakuwa na uwezo nao.Kishaanza tambo na kushindwa kujua matatizo ya Tanzania ni umasikini na sio vyama vingi.
wamemtoa dibwini mzee wa watu saa hz ameanza kutupa mawe.Eti waliopata uongozi kwa rushwa watanyang'olewa madarakani,mh! Alikuwa msitu gani hata hajui kuwa rushwa ndo sitaili mpya ya kupata madaraka ndani ya ccm
 
Top Bottom