Ngoma ya kwetu.

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Ngoma yetu ya asili watu wa manda ludewa inaitwa MGANDA. Tunacheza tukiwa tumevaa kaptula nyeupe na mashati meupe huku tukipuliza "ligubu" na tukiwa tumeshika mkia wa ng'ombe mkononi. Ngoma ya kwenu inaitwaje? Ni ya kabila gani?
 
yetu inaitwa ritungu, tunacheza na mafimbo makubwa na tuachezesha vichwa, nadhani umeshaelewa inimply nini hapo
 
Ngoma yetu ya asili watu wa manda ludewa inaitwa MGANDA. Tunacheza tukiwa tumevaa kaptula nyeupe na mashati meupe huku tukipuliza "ligubu" na tukiwa tumeshika mkia wa ng'ombe mkononi. Ngoma ya kwenu inaitwaje? Ni ya kabila gani?
monirii , umenikumbusha mbali jamani. vipi kuhusu ligambusi? hizi ngoma uwa zinanipaga mzuka kweli kama ikipigwa lazima niende kucheza ingawa MGANDA nachemka step ila LIGAMBUSI uwa siliachii mpaka MC atufukuze.
 
Hapa patamu, aisey !
Nasubiri kwa hamu (kule kenya wangeongeza) na gamu.
Nione ngoma ya Wachagga ! Mambo ya Shimboni na shisha (kama nimekosea kichagga samahani! Mtani'clear )
Sie kwetu Pwani kuna Baikoko, liko Goma kuu pia !
Uchezaji wa Baikoko ili niunyambulishe niombee kibali frm Moderetors nipewe FreeBanZone !
Na hata waki'allow nitalazimika nielezee usiku wama8.
Goma kuu lina starehe yake bwanaa, chini unakwenda kwa Msuli mlaini (ule mwepesi, juu unapanda na Tshart white, mkononi kuna bakora ya asili, mdundo (bit) huwa ni wa polepole , na wachezao hutimbwirika kwa Madaha, Maringo, Majivuno, Mapozi, Mishebeduo, Kujiskia n.k
 
Back
Top Bottom