Engager
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 1,595
- 3,425
Generation Z (Zoomers/ Gen Z) ni kundi la watu ambao wamekulia katika mazingira tofauti kidogo na Generations zingine za nyuma yao (Generation Y kurudi nyuma)
Kwa asiye jua, Generation Z ni kundi la vijana waliozaliwa kati ya 1997 hadi 2012.
Gen Z ndilo kundi kubwa la watu waliokulia katika mapinduzi ya teknolojia. Wamekuwa wakautanana na social media zipo. Yaani mitandao ya kijamii ndio maisha yao.
Na isivyo bahati, Gen Z ndio kundi kubwa la watu wamesoma ila hawa kazi. Ofisi nyingi za serikali na binafsi zimekaliwa na Gen Y kurudi nyuma. Kuna Gen Alpha kwenda juu hawa wengi bado wadogo. wapo shule, vyuo etc...
Kitu kikubwa ambacho watawala wanashindwa kung'amua ni kwamba, mitandao ndio maisha ya Gen Z. Maana mitandao ndio imewakuza.
Gen Z akitaka kujua jambo kuhusu kiongozi wake, team yake ya mpira, msanii wake, chochote yani, ni mtandaoni.
Kuanzia Gen Z kuja huku mbele hakuna mtu anahangaika kununua gazeti, sijui kutune bbc asikilize mambo ya nani sijui amefanya nini, mitandao ya kijamii inawapa kila wanachohitaji na wasichohitaji kwa gharama ndogo.
Wameenda mbali zaidi na kuifanya mitandao ya kijamii kuwa ndio jamii yao. Huko wana interact katika mambo mengi tu hadi biashara zinafanyika huko kwa ufanisi kabisa. Ndo maisha yao. Kwani hamuoni "We are open" zilivyo nyingi huko mitandaoni? Hamuoni "Mikoani tunatuma kwa uaminifu"? Au mnafikiri hayo ni maigizo?!
Watawala mtabagaza na kubananga serika, Gen Z watawatazama kama hawoni. Wataendelea na mambo yao.
Mtateka watu, mtaua, mtafanya ufisadi, rushwa na kila ovu. Watu wataangalia kama kunguru waoga. Wataishia kulalamika nyuma ya key board mtaona hawa ni wa hivi hivi. Nothing the can do.
Malalamiko na kelele zao mitandaoni mtaanza kuziona kero. Badala ya kujirekebisha ninyi, mnaamua kuwazimiwa wao mitandao yao. Ili mabaya yenu yasianikwe. Hapo ndio kosa kubwa lilipo kwa dunia ya sasa.
Mtu amekulia kwenye mitandao ya kijamii, anamarafiki huko, tunawaita followers, anafanya biashara nao, anapiga umbea nao kila akiamka, wanabishana kuhusu soka na mambo mengine ya kijamii. Leo anaamka tu ghafla insta haipo imefungiwa.
Hapo ndipo hasira inapolipuka. Wanaona hawana cha kupoteza tena. Liwalo na liwe. Ndo hayoo maandamano mnayoyaona. Na wakianza kuandamana yanajumuishwa maovu yenu yooote kwenye hasira zao. Ndio maana hata nepal pamoja na mambo mengine ishu ya mitandao 26 ya kijamii kufungiwa imetajwa kama sababu ya Gen Z kuingia road.
Tena mnaanzaga taratibu. Unafungia site za ngono. Tunalalamika tunazoea vpn zetu. Unafungia mtandao wa X, hatujakaa sawa unafungia Jamiiforum. Tena huko Gen Z sio wengi sana.
Kwa sababu ukila nyama ya mtu huwezi kuacha, ipo siku akili zenu zinawatuma kufungia Tiktok na instagram ili mjisonsomole kwa uhuru. Anguko lenu linaanzia hapo.