Ngeleja kujiuzulu ni lazima

Asipoondolewa au kujiondoa kitatokea nini?

Tutaishia kupiga kelele tu

Sadly hamna chochote kitakachotokea.
China waziri aliekuwa na dhamana ya usafirishaji imetokea ajali ya treni - kitu ambacho hana uwezo wa moja kwa moja kukizuia lakini amejiuzulu mwenyewe kwa hiari. Not in Tanzania
 
Shida kubwa inatokana na aliyemteua,huyu atakuwa waziri wa tatu kukumbana na kashafa lukiki kwa kipindi cha utawala wa JK.Kama ameshindwa kumpata mwenye uwezo wa kuiongoza wizara hiyo basi asisite kuomba nje ya CCM wako wananchi wengi wanaoweza kuleta mabadiliko ya maendeleo.Lakini kama ni urafiki na mambo kadhaa ambayo hayana kichwa safari ya kupata nishati itakuwa ndevu sana.
 
Tutasema sanaaaaaa, lakini hawatasikia. Tutapiga keleleeeeeeeeeeeeeee sana wala hawaogopi, tutatukanaaaaaaaaaa hawa jamaa masikio yao yamezibwa pamba.
Tupige magoti tumuombe muumba wetu ambaye aliwaumba wao pia atuondolee adha hii na mateso tunayoyapata waja wake. Ikibidi awaondoe hawa jamaa katika utawala lakini atupe hekima kupata warithi wazuri.
Pamoja na kuandikwa na maandiko yote kuwa Tiini mamlaka zilizopo duniani maana hizo zimewekwa na MUNGU, napata shida kidogo kuamini kama mamlaka inayoongoza Tanzania nayo ni ya mlengo huo, yawezekana tunaongozwa na mamlaka ya kishetani na ndiyo tupatapo mateso. Nungu atuepoushie mbali laana hii na kizazi chao
 
Ngeleja,
Hakuna cha kusubiri, uongozi ni ridhaa. Ili uongoze inatakiwa unaowaongoza waridhie na uongozi wako.

Kwa sasa hakuna mtanzania anaefurahishwa na mwenendo wa wizara unayoiongoza. Hakuna zuri la kufurahisha kwenye wizara yako, hakuja hata kimoja kwako cha kujivunia, hakuna jipya. Umepwaya, umeshindwa, umeanguka. Umemsononesha hata yule aliyekuteua kukupa majukumu hayo!

Nishati ya umeme ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa. Hukufaham umuhim wake, ukafuruhia kupata nafasi hiyo, ukajisahau, sasa umetusababishia janga la kitaifa, huna majibu sahihi ya hatma ya janga hili, huna cha kusubiri, ondoka.

JK ametembea dunia nzima kutafuta wawekezaji, kusini, kaskazini, mashariki na magharibi, imekuwa bure, hasara kwa taifa na upotevu wa bure wa kodi zetu, kwani hakuna uwekezaji kwenye kiza, hakuna uwekezaji kwenye umeme unaotegemea hatma ya mungu kuleta mvua.
Ondoka, umeleta siasa kwenye umeme, huku ukifahamu siasa haziwashi umeme.

Ondoka. Umesababisha mauaji kwa kukata umeme na kusababisha joto kali kwenye maghala ya kuhifadhia mabomu gongo la mboto na kuua halaiki ya watu, kusababisha mayatima, vilema na homeless innocent civilians.

Huna haja ya kuendelea kuwepo. Hila zako zote zimegonga mwamba. Wewe na company yako. Kila uongo umebainika, kuanzia mikataba ya uongo, wamiliki wa kufoji wa dowans, hadi hila dhaifu za kupitisha bajeti yako kwa hongo.

Huna mvuto kwa watanzania kama waziri. Una force tu kuendelea na wizara hiyo. Hakuna kinachoendelea kukuweka hapo, zaidi ya ubinafsi, ung'ang'anizi na ukibaraka.

Hii issue mpaka JK anahusika, hapa la muhimu ni kuandamana kama Malawi
 
285587_224280750941126_100000776075386_556463_2312589_n.jpg
 
Ngeleja achia wizara watanzania tumehoka gizani nenda kapumzike ingawa wewe ni kama mbuzi wa kafara tuuuuuu
 
Ngeleja, richone, RA, mkuu wa kaya, wote ni kampuni moja, itabaki kubebana tu hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom