Ngeleja kujiuzulu ni lazima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja kujiuzulu ni lazima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mizizi, Jul 25, 2011.

 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ngeleja,
  Hakuna cha kusubiri, uongozi ni ridhaa. Ili uongoze inatakiwa unaowaongoza waridhie na uongozi wako.

  Kwa sasa hakuna mtanzania anaefurahishwa na mwenendo wa wizara unayoiongoza. Hakuna zuri la kufurahisha kwenye wizara yako, hakuja hata kimoja kwako cha kujivunia, hakuna jipya. Umepwaya, umeshindwa, umeanguka. Umemsononesha hata yule aliyekuteua kukupa majukumu hayo!

  Nishati ya umeme ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa. Hukufaham umuhim wake, ukafuruhia kupata nafasi hiyo, ukajisahau, sasa umetusababishia janga la kitaifa, huna majibu sahihi ya hatma ya janga hili, huna cha kusubiri, ondoka.

  JK ametembea dunia nzima kutafuta wawekezaji, kusini, kaskazini, mashariki na magharibi, imekuwa bure, hasara kwa taifa na upotevu wa bure wa kodi zetu, kwani hakuna uwekezaji kwenye kiza, hakuna uwekezaji kwenye umeme unaotegemea hatma ya mungu kuleta mvua.
  Ondoka, umeleta siasa kwenye umeme, huku ukifahamu siasa haziwashi umeme.

  Ondoka. Umesababisha mauaji kwa kukata umeme na kusababisha joto kali kwenye maghala ya kuhifadhia mabomu gongo la mboto na kuua halaiki ya watu, kusababisha mayatima, vilema na homeless innocent civilians.

  Huna haja ya kuendelea kuwepo. Hila zako zote zimegonga mwamba. Wewe na company yako. Kila uongo umebainika, kuanzia mikataba ya uongo, wamiliki wa kufoji wa dowans, hadi hila dhaifu za kupitisha bajeti yako kwa hongo.

  Huna mvuto kwa watanzania kama waziri. Una force tu kuendelea na wizara hiyo. Hakuna kinachoendelea kukuweka hapo, zaidi ya ubinafsi, ung'ang'anizi na ukibaraka.
   
 2. O

  OBWERE Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Maoni yako yanaelekea japo hayana uzito
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Lakini lazima tujue ya kuwa january makamba naye hawezi nafasi hiyo
   
 4. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kwakuwa wewe huathiriki na tatizo la kukatika kwa umeme, si una standby generator na pesa nyingi za kununulia mafuta? Huwezi kuona uzito wa tatizo la wizara hii
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jairo aliyekamatwa na mkia kapewa likizo (ya malipo!) kwa hiyo Ngeleja ni salama kabisa - hakuna 'ushahidi' wa kumfukuzisha kazi!
   
 6. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Asipoondolewa au kujiondoa kitatokea nini?

  Tutaishia kupiga kelele tu
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mtamuonea tu Ngeleja wa watu,huyu ni waziri wa tatu wizara hii katika awamu hii,tatizo tunaishi 'kidharura dharura' tu, hata akikabidhiwa nani bila serikali yote kuamua Umeme ni tatizo na kulekeza juhudi na hela kulitatua wizara hii itakuwa siti ya daladala kashuka huyu kapanda huyu.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa kawaida Bajeti ikitolewa Shilingi either Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anapoteza kazi yake; kwasababu lazima iandikwe upya

  Ni Juu ya Rais Kikwete kuamua... Yeye ni Mpole Sidhani kama atamuondoa Ngeleja
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa trend ya nchi hii Ngeleja ataendelea kula bata mwanzo mwisho
   
 10. b

  binti ashura Senior Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  alivyo pata ndivyo atakavo ondoka
   
 11. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,261
  Likes Received: 3,095
  Trophy Points: 280
  Na akitoka tu akutane na pingu zinamsubiri apelekwe mahakamani akajibu kesi yake hiyo!
   
 12. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,261
  Likes Received: 3,095
  Trophy Points: 280
  Asipojiondoa ataondolewa aliyemuweka.... akishidwa kumuondoa aliyemuweka basi yeye aliyemuweka itabidi ajiondoe na yeye asipojiondoa basi SISI (UMMA) tutamuondoa......... tutampa siku 90
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Nani amekuambia kuwa huyo ni kiongozi wa wananchi?Huyo aliteuliwa mpaka aliemteua anune ndo atatoka nduki!
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Ngoja asome hiyo bajeti then tumtoe, nafikiri serikali ya CCM tuanze kuiwajibisha sisi wenyewe sababu viongozi wake ni weak. hatuwezi kukaa gizani 18 hrs per day then waziri anakuja na mipango lukuki ya kwenye makaratasi isiyotekelezeka - hatutaki wote tunaonekane wazezeta.
   
 15. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ''am very secured so don't expect me to leave this position''
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Mkuu,Ngeleja anaongoza wafanyakazi wa wizara yake sasa unaposema anawaowaongoza hawajaridhia basi lazima uje na ushahidi wa akina nani hawajaridika ana utendaji wake .  watu hawaridhiki na mwenendo wa miradi ya umeme na siyo wizara hivyo jitahidi kujenga hoja na siyo kukurupuka tu.Yapo mazuri kama wizara ambayo yamefanyika na yanahitaji kupewa sifa.suala la Umeme ni tatizo ambalo hata mimi mwenyewe linanikera ila sidhani kama waziri ndiyo anasababisha kuwapo huu mgao

  Nishati ya umeme ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa. Hukufaham umuhim wake, ukafuruhia kupata nafasi hiyo, ukajisahau, sasa umetusababishia janga la kitaifa, huna majibu sahihi ya hatma ya janga hili, huna cha kusubiri, ondoka.
  Hapa JK ameingiaje?uwekezaji wa symbion unadhani umekuja hivi hivi?ule wa Kiwira je?Miradi mingine mipya imekuja hivi hivi tu...come on


  ona unaleta viroja,Mauaji gani ambayo yamefanyika na yamefanywa na waziri?kweli mabomu yalilipuka kutokana na joto?kuna AC pale..au unaongea kama kijana wa kijiweni tu...ha ha ha  Mikataba ipi ni ya uongo?wamiliki wa kufoji ni wakinani hao?


  Sikuwahi kujua kama mvuto ni sifa ya mtu kuwa waziri...


  You know JF ni sehemu ya kukata issue na kumkoma nyani giladi..issue hizi za kimajungu majungu hazina nafasi na hapa si maali pake..

  wabunge wana nafasi kubwa ya kuamua kuhusu suala la umeme..Yes na mawazo yote yapo hapa


  https://www.jamiiforums.com/hoja-nzito/155834-utetezi-wangu-wa-wazi-wa-william-ngeleja-the-use-of-emergency-powers-act-1986-a.html


  na kama kweli wabunge wanataka wanachokitaka waidhinishe fedha za kutosha ili mradi wa Stielger's Gorge uanze
   
 17. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ametembea dunia nzima kutafuta wawekezaji, kusini, kaskazini, mashariki na magharibi, imekuwa bure, hasara kwa taifa na upotevu wa bure wa kodi zetu, kwani hakuna uwekezaji kwenye kiza, hakuna uwekezaji kwenye umeme unaotegemea hatma ya mungu kuleta mvua.
  Ondoka, umeleta siasa kwenye umeme, huku ukifahamu siasa haziwashi umeme.

  Hapo kwenye redi ndo pameniacha hoi, hakika mimi nakwambia mpaka siku ambayo JK atatembelea Nyamongo na Ryorya ndo Umeme utawaka. Ngereja hawezi kujiuzuru hadi CCM ishinde Igunga.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa swala la mabagara na gombss,,,,nadhan MWINY NDO WA KUONDOKA,HATA KAMA HAKUKUWA NA UMEME WANGEWEZA KUZUIA,,,KWAN YALIPOLIPUKA MBAGARA KULIKUA NA MGAO????,,,,,
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Huyo ameshapeta,hamna cha kujiuzulu wala nini.
   
 20. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  upuuuzi mtupu!!! Unataka ushahid gani kuonyesha watz walimchoka ngeleja na baadhi ya mawaziri wengine wa jk??
  Unataka ushahid gani kujua mikataba mobovu iliyoingiwa ktk sekta ya umeme??
  Unata ushajid gani kuona kuhusika kwa jk ktk hii hali tuliyonayo??
  Unataka ushahid gani kuona safari za jk zinavyozid kutuumiza kama taifa??
  Kama hujauona ushahid mpakasasa hautaweza kuuoona milele!!
  Maana akili zako zipo tumboni na machoyako yapo mfuko. ...nyie ndio vibaraka mnaouza nchi kwa mlo wa siku moja, watu kama nyinyi uarabuni ni kitanz tu.
   
Loading...