Ngeleja,
Hakuna cha kusubiri, uongozi ni ridhaa. Ili uongoze inatakiwa unaowaongoza waridhie na uongozi wako.
Kwa sasa hakuna mtanzania anaefurahishwa na mwenendo wa wizara unayoiongoza. Hakuna zuri la kufurahisha kwenye wizara yako, hakuja hata kimoja kwako cha kujivunia, hakuna jipya. Umepwaya, umeshindwa, umeanguka. Umemsononesha hata yule aliyekuteua kukupa majukumu hayo!
Nishati ya umeme ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa. Hukufaham umuhim wake, ukafuruhia kupata nafasi hiyo, ukajisahau, sasa umetusababishia janga la kitaifa, huna majibu sahihi ya hatma ya janga hili, huna cha kusubiri, ondoka.
JK ametembea dunia nzima kutafuta wawekezaji, kusini, kaskazini, mashariki na magharibi, imekuwa bure, hasara kwa taifa na upotevu wa bure wa kodi zetu, kwani hakuna uwekezaji kwenye kiza, hakuna uwekezaji kwenye umeme unaotegemea hatma ya mungu kuleta mvua.
Ondoka, umeleta siasa kwenye umeme, huku ukifahamu siasa haziwashi umeme.
Ondoka. Umesababisha mauaji kwa kukata umeme na kusababisha joto kali kwenye maghala ya kuhifadhia mabomu gongo la mboto na kuua halaiki ya watu, kusababisha mayatima, vilema na homeless innocent civilians.
Huna haja ya kuendelea kuwepo. Hila zako zote zimegonga mwamba. Wewe na company yako. Kila uongo umebainika, kuanzia mikataba ya uongo, wamiliki wa kufoji wa dowans, hadi hila dhaifu za kupitisha bajeti yako kwa hongo.
Huna mvuto kwa watanzania kama waziri. Una force tu kuendelea na wizara hiyo. Hakuna kinachoendelea kukuweka hapo, zaidi ya ubinafsi, ung'ang'anizi na ukibaraka.