Ngeleja, Karamagi, Kigoda, Kalemani watajwa madudu mikataba ya uvuvi na gesi

Ukimsikiliza lissu najiuliza kwa nini anachukiwa wakati anaongea ukweli walikataa sheria hizi kipind cha jk kuzipitisha wakatoka nje wapinzani wote, ccm ina wabunge na viongozi dhaifu sana hadi sasa maana uzalendo kwa wao ni kusema uongo.

Kuna watu kwenye taifa letu hawamuelewi Lissu hata kidogo.

Lissu huwa anasema ukweli mchungu unaotishia maslahi ya watu kwa wakati husika, hivyo huishia kuonekana msaliti ila baada ya muda huibuka kuwa shujaa.
 
Walipokuwa wanasema Lowasa ndio fisadi mbona simuoni kwenye hizo ripoti zao?
Ila mara nyingi wanaopenda kusingizia wenzao ndio vinara wa ukwapuzi, 1.5 T imekwapuliwa na wakwapuzi wakatunisha vifua ili wasihojiwe
 
Nani msafi? Kama yupo awe wa kwanza kurusha jiwe kuwapiga hao watuhumiwa. Sijui kwanini watu walioaminiwa na wananchi wanajinajisi kwa rushwa na ufisadi. Inafikirisha sana
 
Wanaweza wakawekwa kiporo hadi 2020 wakafikishwa mahakamani kisha wakapewa dhamana halafu uchaguzi ukiisha na kesi ndio bye bye!!

Hakuna cha kupambana na ufisadi bwana kwa maana nani atupe jiwe la kwanza? Kamwe aliyekuloga, katu hawezi kukuagua.
 
hahahaaaaaaaaaaa...hapo hakuna cha kuchukuliwa hatua aseeeh..hv ngeleja si alikuwepo kwenye escrow au????? halafu alivyokuwa muhuni akaturudishia pesa kiduchu kutufumba macho halafu akatulia kama hayupo..wizi ni sera ya chama wakuu hivyo tuendelee kuwavumilia hawa wana lumumba wanapo timiza hii sera ya chama..amen
 
william Mganga Ngeleja. .. Moja ya vijana waliotumiwa na mtandao kulinda maslahi ya mtandao kwenye sekta na nishati na madini sasa anakwenda kuanguka "ajali ya kisiasa" . Na mbaya zaidi upepo wake kwa mzee baba hausomi
 
Back
Top Bottom