Ngeleja anastahili hili kwa uwezo wake

Ngeleja anastahili hili kwa uwezo wake

Ngereja anatufaa sanaa kwenye uraisi alishatufanyia mengi sana watanzania natunajivunia uwongozi wake uliotukuka, lakini mti wenyematunda mema ndiyo unaopigwa mawe mungu azidi kumlinda ngereja.
 
Watu wengine ni ngumu sana hata kuwauza kwa wapiga kura. Mleta maada umejitahidi kumpamba mtu wako lakini sidhani kama anastahili na kama anaweza kupitishwa na magamba wenzake. Anyway endelea kukamata fursa kama anakupa za kumfanyia promo zipige!!

Nadhani mleta mada za Ngeleja ni yeye mwenyewe,anapima kina
 
Ngeleja anastali kuongoza nchi, kwanza hakurupuki anapoamua kufanya maamuzi. Ni mtu makini sana. Jambo moja muhimu ambalo napenda kuwakumbusha wanatanzania na wazalendo wenzangu kuhusu Ngeleja ni kwamba Ngeleja ndiye aliyeasisi mradi wa bomba la gesi kutoka mtwara mpaka dar es salaam na hatimaye kusambazwa nchi nzima. Mradi ambao ndiyo muarobaini wa Tatizo la umeme Tanzania, pia ,mradi ambao utaiwezesha nchi kuzalisha zaidi ya MW 10000, na kuiwezesha nchi kuuza nje ya nchi zaidi ya mega watt 7000 baada ya kukizi matumizi ya ndani ya megawatt 3000.
Akiwa kama kijana shupavu mzalendo na mpenda maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla anatosha kuongoza nchi kama rais ajaye 2015.
Hongera kwa kupata fursa. Naamin unachoeleza hapa hata nafsi yako haiamin hvyo bali njaa ndzo znakufanya hvyo. Na kwa taarifa yako hata ubunge huku SENGEREMA hapati. Ana kashfa kibao sna haja ya kuzisema hapa watu wanajua na wew pia unajua.
 
Kwa kashfa ya Escrow bado tu mnamuuza?ama kweli tumbo litawaua
zuma ,kenyata ,clinton,mwinyi wote walipitia vipindi vigumi vya kashfa lakini wamekuwa maraisi ,Wiliamu Mganga Ngereja nichaguo la watanzania we kataa hadi mishipa ya shingo ikutoke huwezi zuia mafuriko kwa vidore.
 
Hiyo ni Sifa au kushindwa?

Kila kitu hovyo hovyo usimpe bichwa kwa Sifa za kijinga au waswahili husema usimvike kilemba cha ukoka!!!

Kwa mwenye kufikiri, hiyo ni sifa kubwa sana.

Kila mjuzi hufanya mambo yake yakaonekana myepesi na rahisi sana, nenda kajaribu kufanya, hapo ndiyo utaelewa urahisi wake.
 
Kwi! kwi! kwi! kwi!,Safari hii hata ubunge huku Sengerema atausikia kwenye Breaking News za ITV sembuse Urais.Unaota wewe mleta mada.
 
Hebu niambie halimashauri ya mji mdogo sengerema inaongozwa na chama gani? then linganisha na kipindi kile ngereja wako anaingia madarakani! kamwambie km kakutuma kutafuta kick huku mitandaoni basis wanasengerema tulishamdelete zamani sana.

T WMN na watz wazalendo wa nchi yetu hatukubali KASHFA ZA KUTENGENEZWA! Hatukubali kuendeshwa na wafitni wachache wanaowazushia kashfa za kutengeneza dhidi ya makada wenye uwezo kama Ngeleja. Na tuna uhakika Ngeleja atakapozungumza rasmi na watz kuhusu NIA yake ya kugombea urais nchi itazizima,huyu ni kifaa cha uhakika. Tunawaomba watz wawatafakari wagombea kwa legacy na vision,kwa vigezo hivyo hakuna wa kumshinda Ngeleja,ila kwa fitna watamshinda!
 
Hongera kwa kupata fursa. Naamin unachoeleza hapa hata nafsi yako haiamin hvyo bali njaa ndzo znakufanya hvyo. Na kwa taarifa yako hata ubunge huku SENGEREMA hapati. Ana kashfa kibao sna haja ya kuzisema hapa watu wanajua na wew pia unajua.

Acha kutokwa povu, Ngeleja ana kashfa ipi, ingekuwa hivyo CCM serikali za mitaa sengerema isingeshinda kwa 83% licha ya kadhia pandikizi ya Escrow, Magufuli ambaye hata Escrow hakutajwa jimboni kwake CCM ilipata 79% na kitongoji chake pale nyumbani kilienda upinzani...leta hoja acha kubwabwaja tuu
 
Kwi! kwi! kwi! kwi!,Safari hii hata ubunge huku Sengerema atausikia kwenye Breaking News za ITV sembuse Urais.Unaota wewe mleta mada.

Hoja cyo UKAWA kuchukua baadhi ya vitongoji,walivyopata ndo viliwapa ushindi wa 17 percent. Ila kitongoji cha centre Sengerema mjini kiko chini ya CCM,kikiongozwa na kamanda Kongeja! Hata centres za Chato,Bunda,n.k wapinzani wamebahatisha lakini kinacho matter,ni ushindi overall!
 
Kati ya mtu alie haribu uchumi wa nchi kwa mgao Hatari ambao haujawahi kutokea tena ni William Ngeleja.

Pia wakati akiwa madarakani alituchomekea Richmond. Mgao kapata 40.4 M. Huyu ni bora hata ya J. Makamba.

Naona bado una usingizi ndg, hebu fuatilia hili, usiongeee usichokijua. Kuhusu tuhuma za kwamba mgawo wa umeme ulikuwa unapangwa si unakumbuka kauli hiyo ilimfanya Prof Muhongo ndani ya miezi miwili tu tangu ateuliwe akatiwa hatiani kwa kusema uwongo Bungeni? Muhongo alitaka kutumia kero ya umeme kupata cheap popularity,lakini akaishia kuaibika baada ya Bunge kuunda Kamati Maalum kuchunguza madai yake,baada ya hapa aliufyata kabsaa! Pili tangu Muhongo aingie wizarani kila siku Serikali ilikuwa ikipeleka ruzuku Tanesco kiasi cha Shs 2.4 bil ili kudhibiti mgawo wa umeme,jambo ambalo ni zuri ila limechangia Govt budgetary deficit ya zaidi ya 1 trilioni na ndiyo maana Serikali imekaukiwa! Enzi za Ngeleja Serikali haikuwa na fedha za kupeleka ruzuku Tanesco,ndiyo maana Ngeleja alikuwa anapambana sana.
 
T WMN na watz wazalendo wa nchi yetu hatukubali KASHFA ZA KUTENGENEZWA! Hatukubali kuendeshwa na wafitni wachache wanaowazushia kashfa za kutengeneza dhidi ya makada wenye uwezo kama Ngeleja. Na tuna uhakika Ngeleja atakapozungumza rasmi na watz kuhusu NIA yake ya kugombea urais nchi itazizima,huyu ni kifaa cha uhakika. Tunawaomba watz wawatafakari wagombea kwa legacy na vision,kwa vigezo hivyo hakuna wa kumshinda Ngeleja,ila kwa fitna watamshinda!

Mkuu kuna upotoshaji wa hali ya juu kuwa Sengerema mjini UKAWA ndio walishinda
Mimi Ni mkazi wa Sengerema. Na nilipiga kura ya s/mitaa. Hapo Sengerema centre CCM ndo inaongoza Na ilishinda kwa kishindo
 
Kwa mwenye kufikiri, hiyo ni sifa kubwa sana.

Kila mjuzi hufanya mambo yake yakaonekana myepesi na rahisi sana, nenda kajaribu kufanya, hapo ndiyo utaelewa urahisi wake.

Karibu tushangilie kufufuka kwa bwana wetu Yesu Kristo.
 
Bw Bill Clinton alipingwa alipotangaza nia ya urais Na baadaye akashinda. Mzee Mwinyi naye akipingwa kabla ya kugombea urais kuwa ana kashfa Na hana uwezo ila mwisho wa siku akashinda. Rais Barack Obama naye alipingwa mno eti Ni mweusi Na hafai kuongoza ila mwisho wa siku akashinda. Uhuru Kenyata naye ilikuwa hivi hivi ila baadaye mambo yakawa imara na maadui zake akawafunga mdomo. Sishangai hata mwaka huu maneni yatasemwa dhidi ya WMN Na mwisho atapita. Watu hawaangalii vioja vya wizi n.k watu wanaangalia je kiongozi wao atawasaidia nini?

Mkuu wote uliotajwa walipingwa kwa sababu ambazo sio za kijinai na kukosa maadili ya uongozi. Hizo ndio tofauti zao na huyo unayemtaja. Anyway, waweza kuendelea kuamini utakavyo kwa vile cheo hicho kwa sasa hapa kwetu kimeonekana anaweza mtu yeyote na maisha yakasonga tuu.
 
Karibu tushangilie kufufuka kwa bwana wetu Yesu Kristo.

Kabla ya kumruhusu kuingia ndani umkague kwa kina. Naogopa sana mambo yale ya "kujitoa muhanga" maana huyo naye haeleweki eleweki.
 
Kabla ya kumruhusu kuingia ndani umkague kwa kina. Naogopa sana mambo yale ya "kujitoa muhanga" maana huyo naye haeleweki eleweki.

Ha ha ha ha don't worry kamanda situation will be under control!!!
 
Back
Top Bottom