Ngassa ndani ya uzi mwekundu!

Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,710
291
Unaweza usiamini lkn Mshambuliaji mpya wa Mabingwa wa soka Tanzania Bara Mrisho Khalfani Ngassa leo ameanza mazoezi rasmi na team yake mpya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mbuzi ABC nini sijui pamoja na msimu mpya wa Ligi unaotarajia kuanza mwezi September.
Akinukuliwa na Mtandao mmoja unaojishughulisha na Vijana Teen Tz Ngassa amesema amejipanga kufanya mambo makubwa na ndo maana hajataka kupoteza muda kwa kujiunga na wenzake kuanza mazoezi,aidha Ngassa amewataka mashabiki wa Simba kumpa ushirikiano ili awafanyie mambo ambayo hawatayasahau kwa urahisi


attachment.php


attachment.php


Ama kweli pesa ndo kila kitu,binafsi sikutegemea kumuona Ngassa akiwa katika uzi huu, sisi Yanga kwa kuwa weredi wetu ni mkubwa kuliko mashabiki wa hiyo team uliyoichagua kuichezea tunasema hatuna tatizo na wewe na tunakutakia kilalaheri katika hiyo team yako mpya na kamwe hatutakuzomea uwanjani kama wao wanavyomzomea Yondani wetu,sisi au niseme binafsi mimi nakuunga mkono kwa uamuzi uliochukua wa kutoiacha offer ya kina Kaburu(siku zote Wajinga ndo waliwao) ukichukulia mpira ndo kazi yako na mpira wenyewe ndo unaelekea mwishonimwishoni,wapigie kazi ya maana wasije kukutafutia sababu.
 

Attachments

  • ngasa6.JPG
    ngasa6.JPG
    90.9 KB · Views: 291
  • ngasa3.JPG
    ngasa3.JPG
    61.8 KB · Views: 287
Kwanini mnampaisha ivi wakati anacheza bongo?

Angekua anachezea Barca ingekuaje?

Msitujazia server bila sababu ya msingi.
 
Kwanini mnampaisha ivi wakati anacheza bongo?

Angekua anachezea Barca ingekuaje?

Msitujazia server bila sababu ya msingi.

Unafikiri kwanini kina Kaburu wameamua kumpa Mil 30,Gari na mshahara mkubwa kuliko "MUNGU mchezaji" wao Kaseja? kwanini usiwaambie wasitujazie fedha kwenye mzunguko?
 
Naona kaungana na washikaji zake wa kitambo wakiwa Yanga, Kaseja na Kigi
 
Kwanini mnampaisha ivi wakati anacheza bongo?

Angekua anachezea Barca ingekuaje?

Msitujazia server bila sababu ya msingi.

Uko sawa kabisa, Ngasa ana nini cha zaidi! Lakini ukuwakusanya watu wanaokuwa mwisho darasani wilayani ukawapa mtihani atatokea wa Kwanza. hivyo hivyo, ni wa kwanza kwa wasiojua. Anacheza mpira gani wa kumpa umaarufu hivi.
 
tunasema hatuna tatizo na wewe na tunakutakia kilalaheri katika hiyo team yako mpya na kamwe hatutakuzomea uwanjani kama wao wanavyomzomea Yondani wetu,.

Mkuu na wewe huwa unaandika vitu vingine hata havieleweki, Ngasa hajatoka Yanga kwenda Simba katoka Azam Kwenda Simba, na Kelvin katoka Simba kwenda Yanga, Ingekuwa Ngasa naye katoka Yanga basi ungweza kuweka ulinganifu lakini sasa ni vitu viwili hata havifanani.
 
Huo ndio mwisho wake mkumbukeni Lunyamila alivyoishia. Huo ndio mpira wa kibongo. Giggs anachezxa miaka zaidi ya 20 tz miaka 3 kwishney.
 
Ngasa bado ananafasi ya kujifua na kurudisha mpira wake naamini akijituma mazoezini na kwenye mechi atapata timu ya kucheza ulaya
 
Mkuu na wewe huwa unaandika vitu vingine hata havieleweki, Ngasa hajatoka Yanga kwenda Simba katoka Azam Kwenda Simba, na Kelvin katoka Simba kwenda Yanga, Ingekuwa Ngasa naye katoka Yanga basi ungweza kuweka ulinganifu lakini sasa ni vitu viwili hata havifanani.

Kiongozi usichoelewa hapo ni nini,Ngassa atoke Azam atoke wapi haijalishi,tunachoangalia ni mutual love,Ngassa tulikuwa tunampenda na yeye alikuwa anatupenda...tulikuwa tunamuhitaji sana asimame pale namba 7 ambapo Mt Tom bado anahangaika nako lkn mmetuzidi kete ndo tunasema sisi hatutamzomea,nyie endeleeni kuzomea waliotoka kwenu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom