Ngasa ajiunga el marreikh

mapatano yake yake yeye na na hao wasudani

JUZI OKWI ALIUZWA AZAM KUPITIA HUMU JF LEO KTK GAZETI KASAINI MKATABA MPYA NA SIMBA

MPALU aka mwanaume(mume) je ni sahihi klabu ikachukua ada ya usajili kabla ya mchezaji hajakubaliana na timu yake mpya mshahara?

SASA IKITOKEA MCHEZAJI AKAGOMA KWENDA TIMU MPYA INAKUAJE?
 
hii ishu imekaa kishababi mpaka basi hili ndio soka la bongo kama mbuyi twite vile na yanga...
 
Viongozi wa Simba wanafanya makosa kwenye usajili kila siku
 
EH_Mzalendo Kama si taarifa za redio mbao ni afadhali.....maana uwezo anao ila akiendelea kama alivyo sasa atasahaulika kwenye ulimwengu wa kandanda kabisa
 
Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Mengi yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.
Imetolewa na Utawala

source Ngasa atua Ell Mereikh kwa $75,000 | The Official Website of Azam Football Club
 
$ 70K?? aiseeeee mshahara wa bacary sagna per week......
 
Ili mradi mkataba uheshimiwe...... hatutaki longolongo...... Viongozi wa Simba wawe makini ... watafute replacement ya Ngassa.... hakuna cha ajabu... :clap2::clap2::clap2:
 
Ili mradi mkataba uheshimiwe...... hatutaki longolongo...... Viongozi wa Simba wawe makini ... watafute replacement ya Ngassa.... hakuna cha ajabu... :clap2::clap2::clap2:

kipatio ndio ishu sasa hapo ndio tutakapo chkulia ubingwa na niyonzima wanamtaka..

forza la azam fc:pop2:
 
Mpaka sasa sifahamu Ngasa alikuwa mchezaji halali wa timu ipi kati ya hizi Azam au Simba?
 
Nimemsikia Rage Clauds anadai Ngassa ni mchezaji wa Simba angekuwa wa mkopo angelipwa mshahara na Azam siyo Simba, kwenye swala la pesa Rage yupo tayari amwage chozi mpaka kieleweke.
 
....hizi timu za mafisadi bana, sasa huyu si alishauzwa, inakuwaje sasa wanamuuza tena ??
 
Nimemsikia Rage Clauds anadai Ngassa ni mchezaji wa Simba angekuwa wa mkopo angelipwa mshahara na Azam siyo Simba, kwenye swala la pesa Rage yupo tayari amwage chozi mpaka kieleweke.

Hapa naona movie ya Mbuyi Twite inajirudia kwa mbali......"Mbuyi Twite featuring Mrisho Ngasa & Maha-Rage".
 
haya ndiyo malezi ya kikwete kwa vijana wake. Tangia ajiingize kusaidia taifa star, kweli vijana wetu wameanza kuvuma sana . Huyu Ngasa lazima atapata wasaa wa kujulikana Ulaya kisoma mara moja. Kila la kheri Ngasaa.
 
Kama hamjui, mchezaji yeyote anayechezea Simba huwa anatafutiwa soko nje ya nchi. hiyo ndiyo sera ya Simba/ni kama ile ya Arsene Wenger
 
Back
Top Bottom