Ngasa ajiunga el marreikh

Ngasa kacheza simba miezi 3 kapata timu nje lakini alicheza yanga 3 na azam 2 hatukuona..samatta nae alicheza miezi 3 akapata timu..hongera simba
 
haya ndiyo malezi ya kikwete kwa vijana wake. Tangia ajiingize kusaidia taifa star, kweli vijana wetu wameanza kuvuma sana . Huyu Ngasa lazima atapata wasaa wa kujulikana Ulaya kisoma mara moja. Kila la kheri Ngasaa.

zile bilion alizo wapa brazil angechukua vijana akawaweka huko hata mwaka ingesaidia zaidi..
 
hii nayo shoo nyingine Rage anasimamia baada ya kuvurunda ya Mbuyu na Yondani. Mwenyekiti huyu simba wamchukulie hatua manake ni wa mwisho kujua siku zote. Mchezaji kesha sign, yeye keshatunga uongo kwa wanachama.
 
Ngasa kacheza simba miezi 3 kapata timu nje lakini alicheza yanga 3 na azam 2 hatukuona..samatta nae alicheza miezi 3 akapata timu..hongera simba
haya yote yametokana na yeye kubusu jezi ya Yanga ,si unaona bahati ilivyomfikia kwa hiyo mchezaji yeyote anayetaka kwenda kucheza soka la kulipwa kwanza unatakiwa kuiheshimu yanga na kuibusu jezi yake mambo yataiva.

 

MPALU aka mwanaume(mume) je ni sahihi klabu ikachukua ada ya usajili kabla ya mchezaji hajakubaliana na timu yake mpya mshahara?

SASA IKITOKEA MCHEZAJI AKAGOMA KWENDA TIMU MPYA INAKUAJE?
mambo bongo kukomoana taarifa zisizo rasmi zinadai jamaa wasudani walifuata simba na dau la dola laki moja na nusu ila simba si unajua wazee wa mauzo makubwa wakadai laki mbili na nusu....inavyoelekea wajanja fulani wakawatonya kwamba yupo simba kwa mkopo basi wakaenda azam wakazungumza ndani ya saa mbili wakukubaliana........huu ni mwendelezo wa kukomoana kibongobongo maana kiuhalisia dau waliochukua dogo sana ilitakiwa wachukue dau kubwa zaidi...
 
Ci ndio magoli aliyowafunga wasomali..! au..?
hapana magoli yake toka aanze kuchezea STARS ukilinganisha wachezaji ambao bado wanacheza mpaka sasa yeye ndo mwenye magoli meni
 
haya yote yametokana na yeye kubusu jezi ya yanga ,si unaona bahati ilivyomfikia kwa hiyo mchezaji yeyote anayetaka kwenda kucheza soka la kulipwa kwanza unatakiwa kuiheshimu yanga na kuibusu jezi yake mambo yataiva.

niyonzima naye mambo yake yaive
 
Verosa ya Rage vp atairudisha show room?
plus Simba ilifanikiwa kumalizana na Ngassa jana na kusaini naye mkataba wa miaka miwili, ambao umemfanya aondoke na zaidi ya Sh. Milioni 35, Milioni 12 akipewa taslimu na nyingine akipewa gari (Milioni 18), wakati mpenzi mwingine wa Simba amemuongezea Milioni 5.
 
Mzee wa kulala reception sasa hivi atalala kwenye Banda la kuku
 
[h=5]Edo Kumwembe[/h]16 minutes ago

Mrisho Ngassa amejiunga El Marreikh kwa dola 70,000 kutoka Azam......mshahara atajijua mwenyewe!!....ikumbukwe kuwa Ngassa ni mali ya Azam sio Simba...

si mali ya simba?si nilisikia kalamba gari na milioni kadhaa kutoka simba?fafanua pls
 
si mali ya simba?si nilisikia kalamba gari na milioni kadhaa kutoka simba?fafanua pls
AZAM WANASEMA HIVI.........Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Mengi yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.
Imetolewa na Utawala
 
mchezaji yupo kwa mkopo simba?means analipwa mshahara/nusu ya mshahara na Azam?kama hivyo ndivyo basi hiyo ni sawa,otherwise ni utapeli wa kutupa!
 
Jana kuna mchangiaji kwenye radio moja amenichekesha sana!

Jamaa anasema, " Mtumaini cha ndugu hufa masikini na hamna dhambi kwa mtu kuuza kilicho chake"

hahahahaha:becky: Poleni Simba
 
Kwenye huu uzi nimeshindwa hata niandike nini aise. Anyway ngoja nijaribu, kama hii habari ni ya kweli basi club ya Simba kuna haja kubadili uongozi tukianza na mwanasheria wa timu.
 
Back
Top Bottom