NGARA ni Tanzania ama?

we kijijini kwenu wanajua kiswahili?basi kama walikosea nenda kapime vizuri wewe!mbona hamuwasemi wamasi walioko Namanga au wajaluo wa Sirali?sijui mnatumia kitu gani kufikiri siamini kama mnatumia ubongo
 
si uongelee kwenu,Ngara panakuhusu nini,ujinga tu ndy unakusumbua,mtu mzima hovyooooo!
 
Ngara kwa asili haina tofauti na Rwanda NA Burundi na mashariki ya Congo. Ngara kuna Clan kubwa tatu. Watutsi, wahutu na watwa. Kwahiyo unapowaona watutsi Ngara wapo kwao na kuhusu kuwepo kwa wanyarwanda Ngara na warundi sidhani km ni tatizo so long as wapo kihalali na idara ya uhamiaji ipo kwa ajili hiyo.
 
Wee bi tch unacheza makida makida relini, subiri treni 'ikupitie'
Aliyekwambia mtutsi kwao sio Ngara ni nani? Watawala wa asili wa Ngara unadhani ni Nani kama sio watutsi? Kasome upya historia
 
Kila sehemu ina utaratibu wake na radio Kwizera huwa wanaongea lugha tatu kiswahili Kirundi na kinyarwanda kwa sababu inasikika mpaka Rwanda na Burundi. Na kirundi na kinyarwanda kinashabihiana na kihangaza kwahiyo hakuna kisichoeleweka kwa watu wa ngara
 
 
Basi kama ingelikuwa sio dermacation za wazungu, Ngara kiuhalisia ingelikwenda Burundi. Full stop!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu vipi sehemu inaitwa kyaka....huko jamaa wakule hawajui kiswahili ni kiganda kwa kwenda....vipi kundi hili nalo tuliite vipi?
 
Shida ni nn mi sijaelewa hapo. Utamaduni wa Ngara unakukera?
Hapana, ni ndugu zangu tu wazuri. Ila wako karibu sana na Burundi kwa lugha, kama wahaya walivyokaribu na waganda. Ukimuuliza Mhaya (hasa waziba) anataka kuwa wapi atakwambia Buganda ( siyo Uganda)
 
Mkuu vipi sehemu inaitwa kyaka....huko jamaa wakule hawajui kiswahili ni kiganda kwa kwenda....vipi kundi hili nalo tuliite vipi?
Hao wanaitwa BagandaKyaka- wanakuwa na wanajihisi wao ni waganda ila walitenganishwa na mipaka. Ni kweli Kiswahili hawajui, mpaka mtu afundishwa shuleni!
 
Haya usemayo yapo sana, nimekaa sana national housing pale.

Wanyarwanda ni wengi mno na wengine wanafanya kazi hadi kwenye taasisi kubwa tu.
 
Unakereka nini? Si ndiyo kuimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Warundi na Wanyarwanda hoyeeeeee! It is too late maana wilaya za Sengerema na za mkoa wa Geita wamejaa, wananunua mashamba kama hawana akili nzuri, wameleta ng'ombe maelfu kwa maelfu na sasa ili tupate kura kwenye chama chetu, baadhi ni viongozi wa CCM. Tunadeal na watu wenye uraia wa nchi mbili
 
Kuna jamaa mmoja aliwahi Kua RPC Iringa kama sijasahau, siku moja nimeenda Rwanda nikashangaa ana walinzi kama 10 hivi wamemzunguka kumbe amekua sijui general.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…