Ngao Ya Jamii, 2019: Simba SC yaichakaza Azam FC goli 4-2 kuchukua Ngao hiyo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kuelekea kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii leo Agosti 17, 2019 Ni mnyukano kati ya bingwa wa TPL, Simba SC na bingwa ASFC, Azam FC, ni mechi mzuri ya aina yake yenye burudani nyingi za soka na ladha ya aina yake uwanjani, ni mchezo utakaovuta hisia za wapenda soka.

Mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ni kuashiria kufungua pazia la kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Premier League TPL.

Simba SC,
inaelekea kwenye mchezo wa leo ikisaka kombe la sita huku Azam FC, wakisaka kombe la pili katika historia ya Azam na Simba Ngao ya Jamii tangu mwaka 2009.

•••Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

Mwanachama, Mshabiki wa Simba SC pamoja na Mdau wa kandanda nchini, unakosaje Taifa kushuhudia Show ya hatari ya Next Level Iga Ufe kutoka kwa Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, Klabu yenye wachezaji wenye vipaji, mahiri uwanjani katika kusakata kandanda la viwango vya juu ambavyo vilivyothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika.

Kutana na Cloutis Chota Chama Triple C, kiumbe mnyumbulifu mwenye udambwi udambwi na makorokoro kibao uwanjani, sambamba na Chuma kutoka Sudan, Sharaf Eldin Ali Abdulrahman Shiboub fundi wa mpira huyu mwenye uwezo kutema kushoto na kufukia kulia, mwenye uwezo wa kugusa na kuachia mpira.

kutana na Mshambuliaji matata Deo Kanda, anayeteleza mithiri ya samaki kambale, ambaye kazi yake ni kuwachukua wapinzani na kuwatambaliza huku wakibaki wanagaa gaa mithiri ya nyoka mweusi aliyemwagiwa mafuta ya taa..!

WanaSimba tukutane Taifa kazi ndo imeanza tunachukua tena This Is Simba SC Next Level Iga Ufe Nguvu Moja..Tukutane Taifa Usikose Ukaambiwa..!
IMG_20190817_112642_009.jpeg

IMG_20190817_062556_444.jpeg

********

MECHI ya 12 leo Uwanja wa Taifa imekamilika na umezalisha mabao mengi kuliko mchezo wowote tangu kuanza kwa michuano hii mwaka 2001.

Sasa Simba imefikia hatua ya Yanga ambao walitwaa mataji hayo mara tano na leo wamefikia hatua ya kutwaa mataji matano.

Azam ambayo imecheza michuano hii mara sita imetwaa taji hilo mara moja sawa na Mtibwa Sugar na iliifunga Yanga kwa penalti.

Hivyo kwa sasa ni rasmi Pazia la Ligi Kuu Bara limefunguliwa kwa Simba kutwaa ngao yao ya jamii ambayo msimu uliopita walitwaa mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Simba yamefungwa na Sharaf Shiboub ambaye alipachika mabao 2 dakika ya 17 na 21 la tatu limepachikwa na Chama dakika ya 56 na msumari wa mwisho umepachikwa na Kahata dakika ya 78.

Yale ya Azam yamepachikwa na Idd Chilunda dakika ya 13 na Frank Domayo dakika ya 78.

231AB761-7DD1-441D-980B-163B47E3B465.jpeg
 
Kuelekea kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii leo Agosti 17, 2019 Ni mnyukano kati ya bingwa wa TPL, Simba SC na bingwa ASFC, Azam FC, ni mechi mzuri ya aina yake yenye burudani nyingi za soka na ladha ya aina yake uwanjani, ni mchezo utakaovuta hisia za wapenda soka.

Mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ni kuashiria kufungua pazia la kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Premier League TPL.

Simba SC,
inaelekea kwenye mchezo wa leo ikisaka kombe la sita huku Azam FC, wakisaka kombe la pili katika historia ya Azam na Simba Ngao ya Jamii tangu mwaka 2009.

•••Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

Mwanachama, Mshabiki wa Simba SC pamoja na Mdau wa kandanda nchini, unakosaje Taifa kushuhudia Show ya hatari ya Next Level Iga Ufe kutoka kwa Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, Klabu yenye wachezaji wenye vipaji, mahiri uwanjani katika kusakata kandanda la viwango vya juu ambavyo vilivyothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika.

Kutana na Cloutis Chota Chama Triple C, kiumbe mnyumbulifu mwenye udambwi udambwi na makorokoro kibao uwanjani, sambamba na Chuma kutoka Sudan, Sharaf Eldin Ali Abdulrahman Shiboub fundi wa mpira huyu mwenye uwezo kutema kushoto na kufukia kulia, mwenye uwezo wa kugusa na kuachia mpira.

kutana na Mshambuliaji matata Deo Kanda, anayeteleza mithiri ya samaki kambale, ambaye kazi yake ni kuwachukua wapinzani na kuwatambaliza huku wakibaki wanagaa gaa mithiri ya nyoka mweusi aliyemwagiwa mafuta ya taa..!

WanaSimba tukutane Taifa kazi ndo imeanza tunachukua tena This Is Simba SC Next Level Iga Ufe Nguvu Moja..Tukutane Taifa Usikose Ukaambiwa..!
View attachment 1183559View attachment 1183560
Azam itamkosa kiungo wao Mudathir Yahaya Abass
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom