Hongereni sana watani zangu kwa kandanda safi la 1st hal(japo siuangalii mpira,TANDARKSCO wamefungulia giza mapema)....Naona(kwa mujibu wa TBC Taifa) Yanga wanakimbiakimbia tu uwanjani......Kila la heri,mnastahili kuchukua 'ubingwa' wa Ngao ya jamii.....Yanga tumeonekana kushindwa hata kabla ya kungia uwanjani(kwa kutishia kutoingiza timu uwanjani)......[/QUOT]a
Sikutegemea kama wewe upo, nashangaa unakuja kujitokea kwenye thread za kizembe kama hii! kwanza nakukosoa hakuna ubingwa wa ngao ya Hisani dunia hii, pili Simba ndio ilikuwa ya kwanza kusema haitoingiza timu uwanjani, lakini hili halifanyi nisikemee upuuzi wowote walioufanya Yamga.
Yeah.....Nipo mkuu.......
Bala is always here.......
Narudia tena: Yanga tulishindwa hata kabla ya mchezo(kwa kutishia kutoingiza timu uwanjani)...
Tatizo lako na umekurupuka.....Kuna tofauti kubwa sana kati ya 'ubingwa' na ubingwa....
Nimewapongeza watani kwa kuchukua 'ubingwa' wa Ngao ya jamii....
Leo Yanga tumezidiwa na Simba kila idara,kubali kataa ila ukweli ndio huo....
Beki ya Simba ilitulia mwanzo mpaka mwisho....Ya kwetu ilipwaya sana leo hasa Fuso na Chacha...
Kiungo cha Simba kilituzidi sana dakika 45 za mwanzo na kipindi cha pili kidogo Yanga tuliibuka kwenye kiungo(hasa baada ya kutoka Kigi Makassy na kuingia Hamis Kiiza na baadae Rashid Gumbo 'Fundi').....
Washambuliaji wetu hakuna lolote walilofanya zaidi ya kukimbiakimbia tu uwanjani na kukosa magoli ya wazi.....Emmanuel Okwi,Felix Sunzu,Haruna Moshi na baadaye Gervais Kago wameisumbua sana beki yetu leo shukrani zimuendee Shaban Kado kwa umahiri wake golini...
Ila kwa Haruna Niyonzima Yanga tumelamba dume......I wish angecheza na Nurudin Bakari mambo pale katikati yangekuwa mswano leo...
Btw.....
Kuna taarifa Rage anapeleka Ngao na timu bungeni ijumaa ili ipongezwe na wahishimiwa.....
Hongereni sana watani........Mlistahili ushindi