Ngao Kwenye Gari ni kosa kisheria

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,912
Poleni na Majukumu ya Jumapili.

Wakuu Jana katika zungukazunguka yangu Mjini hapa nilisimamishwa na Askari Traffic Baada ya Kunikagua alivyoweza yeye Mwishoni alinipa uzoefu ambao sikuwahi kujua kama nikosa.

Aliniuliza kwa nini Gari yako Ina Ngao. Nikamwambia kuwa hiyo Ngao ilikuwa na Spot light lakini nilitoa. Akasema Ngao ni kosa Magari hayapashwi kuwa na Ngao. Naamini mumeshawahi kuona zile Ngao za Rav4.

Wakuu baada ya kuachana naye nilibaki najiuliza kuwa sasa hii imekuwa too Much kweli Ngao ambao haina madhara yoyote leo hii ni kosa kuwepo kwenye Gari?

Mwenye uzoefu na Utalaam zaidi naomba nisaidiwe kueleweshwa kweli Ngao Hazitakiwi.
 
Ngao za jua kali za kuchonga ndiyo hazitakiwi, Lakini zile special za kuja na gari hazina madhara na si haramu.

Kama alikomaa ni njaa kali tu iliyoleta shida.
 
Ngao za jua kali za kuchonga ndiyo hazitakiwi, Lakini zile special za kuja na gari hazina madhara na si haramu.

Kama alikomaa ni njaa kali tu iliyoleta shida.
Siendeshi gari isiyo na bullbar ni kosa lipi kisheria nitakuwa nimefanya?
 
Ngao za jua kali za kuchonga ndiyo hazitakiwi, Lakini zile special za kuja na gari hazina madhara na si haramu.

Kama alikomaa ni njaa kali tu iliyoleta shida.

Mkuu ni hiz ngao zinakuja na Gari ambazo hata dukani zipo
Mimi ilikuja na Gari
 
Madereva wanaoendesha magari yenye ngao huwa wana kiburi sana barabarani, ndio wanaongoza kwa kuwapiga pasi madereva wasiokuwa nazo hah hah hakuna la zaidi mkuu!
 
Huyo umemkosea, ilitakiwa umuulize akupe maelezo ya kutosheleza ni makosa gani kisheria kwa gari ikiwa na hiyo ngao
 
Kama ni hizi zipigwe tu marufuku hamna namna.....
6a0153924291c1970b01543635324d970c-800wi
 
Back
Top Bottom