News Alert: Mwangunga aliangukia Bunge; asamehewa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News Alert: Mwangunga aliangukia Bunge; asamehewa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 30, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  KLHN International

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Shamsa Mwangunga amekuwa Waziri mwingine wa serikali ya Rais Kikwete kuomba radhi Bungeni kufuatia kile ambacho kimeelezewa kuwa ni kudharau Bunge kwa kuchukua maamuzi ambayo hayakuzingatia hoja ambayo iko mbele ya Bunge. Mhe. Mwangunga ameliangukia Bunge leo hii baada ya Mbunge wa Kwera Mhe. Chrisant Mzindaka kuona kuwa Waziri huyo amedharau hoja yake ambayo ilikuwa inasubiriwa kutolewa maamuzi Bungeni kuhusu suala la vitalu vya uwindaji.

  Mwaka jana Bw. Mzindakaya alitoa hoja Bungeni ili serikali isitishe kutoa leseni kwa wawindaji wa nje ambao muda wao unamalizika mwaka huu mpaka taarifa itakapotolewa na Waziri juu ya mapendekezo yaliyotolewa kuboresha sekta hiyo ya uwindaji. Hata hivyo imekuja kugundulika kuwa Waziri Mwangunga ameshatoa maamuzi hayo na kuwaongezea leseni wawindaji hao kitu ambacho "kilimkorofisha" Mhe. Mzindakaya. Endapo Bunge lingeamua kupitia hoja hiyo na kumchukulia hatua Mhe. Mwangunga basi angekutwa na dharau ya Bunge (Contempt of parliament) kosa ambalo linalingana na lile la kudharau Mahakama (Contempt of court). Adhabu ya kosa hilo ni siku saba jela.

  Vyanzo vyetu kutoka Dodoma vinasema kuwa baada ya kuona kuwa upepo hauendi upendo wake Mhe. Mwangunga akifuata njia iliyotengenezwa na Waziri Mkuu Pinda jana ambaye aliomba msamaha kwa wale wa Tanzania wanaoona amekosea naye mama Mwangunga aliona hana njia nyingine isipokuwa kuomba msamaha kwa Wabunge. Inaonekana Bungeni kumekuwa na hali ya huruma na baadhi ya wabunge wa CCM na hata wale wa upinzani wametangaza kumsamehe.

  Hata hivyo haijulikani huko mbeleni ni kiongozi gani mwingine naye atakuwa tayari kuomba msamaha kwa mtindo huu na hivyo kukwepa kuwajibishwa. Maoni ya watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifuatilia masuala haya wanaona kuwa itakuwa vigumu sana huko mbeleni kumwajibisha mtu yeyote kwani wotesasa watakuwa wanasimama kuomba samahani na wengine kumwaga machozi kwa "uchungu".
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Utamaduni wa kusameheana ni mzuri,
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi UKIUWA na wewe ni MBUNGE, tena kwa KUKUSUDIA yaani UNAPANGA na kwenda kufanya kitendo. Mbunge huyu akienda bungeni (kama Dito vile) na kuomba msamaha, basi asamehewe? Kwa kesi ya Pinda naweza kusema ni HASIRA ambayo ilipanda bila kupanga na KUROPOKA. Ila huyu Waziri, aliyepokea maombi, akaweka sahihi na huku akijua alishaahidi kuwa HATAFANYA HIVYO, sidhani kama anastahili msamaha. Ni sawa na kesho, ikitokea PINDA aropoke tena, nitakuwa wa kwanza kumvalia BANGO.
  Huyu kweli wapinzani ndiyo walitakiwa kulala naye mbele. Wakati anafanya maovu hayo alikuwa na akili timamu. Alijua anafanya nini. Na kama alikuwa hajui/kasahau maneno ambayo mwenyewe aliahidi na hayo wala si mengi kama katiba basi huyu wakomae naye.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na yule mwindaji wa Loliondo kutoka Arabuni muda wake wa mawindo unamalizika lini?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nasikia Lowassa naye anataka kupata nafasi ya kuomba msamaha!
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naye alilia?, manake sasa nikiona nataka kufungiwa na JF, naanza kusema huku nikilia "pengine kwa kuwa Invisible hujawahi kuandikwa vibaya, mmhhh, mtaniwia radhi, mmhhh..."
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu kinapikwa hapa........
   
 8. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kwa kuwa amekiri alikosea, ina maana alitakiwa kufuta hivyo vibari na kupisha hoja ya Wabunge indelee na mkondo wake sio?

  Samahani bila kurekebisha makosa ina manufaa gani kwa Watanzania?
   
 9. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hata mimi natumai hivyo vibali vimefutwa, sio mtu anaomba Msamaha halafu kila kitu kinabaki vile vile, huo utakuwa ujinga wa hali wa juu kwa wabunge wote wanaokubali hiyo misamaha. Kama anaomba msamaha basi akubaliwe kwa sharti la kuvifuta vibali vyote na si vinginevyo.

  Atakuja Chenge nae ataomba msamaha na kubaki na vijisenti vyake, kesho yake utasikia Karamagi anaomba msamaha kuhusiana na kusaini mkataba hotelini, atakuja Mramba ataomba msamaha na kesi yake ili ifutwe.

  Sheria ni msumeno inabidi muwasamehe baada ya kutumikia adhabu. Hatutaki Taifa la viongozi watoa machozi wakati wakiomba misamaha.
   
 10. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni lini watawajibika au kuwajibishwa? msamaha maana yake umekubali makosa na kaa pembeni wengine wafanye kazi. lakini muda bado upo itabidi waangaliwe.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ngoja nifuatilie matokeo yake yalikuwa nini maana Mzindakaya alikuwa amepania kweli.. sasa uwaziri utakuwa ni mzigo ambao anayetaka kuchuchumaa kuubeba itabidi afikirie mara mbili.. siyo ujiko tena!
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Mi sina ttaizo na yeye kuomba msamaha. Suala ni kwamba je amebatilisha uamuzi alioufanya kinyume na maamuzi ya Bunge? amerevoke hizo licence?
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jibu ni ndiyo with some kind of technicality. Leseni zote zitasitishwa baada ya mwaka huu hivyo ilinyongeza iliyotolewa inaondolewa. Leseni zote zitatolewa upya mwakani na msisitizo utakuwa kwa "wazawa" (sorry sielewi hilo neno hadi leo hii).
   
 14. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wabunge wamchachafya Mwangunga
  Halima Mlacha, Dodoma
  Daily News; Friday,January 30, 2009 @21:15

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, amejikuta katika kitimoto bungeni, kutokana na uamuzi wa wizara yake kuongeza muda wa ugawaji vitalu vya uwindaji kutoka mwaka mmoja hadi mitatu jambo ambalo linadaiwa kuwa ni ukiukaji wa haki na Azimio la Bunge hilo.

  Kutokana na hali hiyo, Bunge hilo jana lilipitisha mapendekezo ya kufuta muda ulioongezwa na serikali na kutaka sasa vitalu hivyo vianze kugawiwa mwaka 2010 ili wamiliki wapya waanze kuvitumia rasmi mwaka 2011 badala ya kugawiwa mwaka 2012 na kuanza kutumiwa rasmi 2013.

  Akiwasilisha hoja yake binafsi bungeni Dodoma jana, Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya, alisema kitendo cha wizara hiyo kuongeza muda wa umiliki wa vitalu hivyo, pamoja na kukiuka Azimio la Bunge na kulitia hasara taifa kiasi cha Sh milioni 12.3, pia kilitokana na shinikizo la wamiliki wa vitalu.

  Alisema katika vikao vyake, Bunge hilo liliazimia kuwa kwa kuzingatia muda wa umiliki vitalu unaokoma mwaka huu, serikali iweke mikakati maalumu ya kukamilisha utekelezaji wa Azimio la Bunge katika muda uliobaki. “Kimsingi azimio hilo lilikusudia kuwa vitalu vyote vya uwindaji wanyamapori, vigawiwe upya ili wamiliki wapya waanze kuvitumia mwakani.”

  Mzindakaya alisema pia mwaka 2006 iliundwa kamati maalumu kuchunguza suala la ugawaji vitalu na kamati hiyo ilitoa mapendekezo yake na moja likiwa ni vitalu hivyo kugawiwa mapema. “Mabadiliko haya ya ghafla ni msukumo tu wa wamiliki wa vitalu hivi, napata shida sana pale nchi yetu inaposukumwa na Wazungu.”

  Alisema pamoja na azimio hilo, kamati maalumu na kikosi kazi kilichoundwa na kutoa mapendekezo yaliyofanana, ikiwa ni pamoja na Waziri kuahidi bungeni kuwa serikali ingezingatia na kutekeleza maazimio hayo na kuandaa Muswada wa Sheria mpya ya wanyamapori, bado serikali iliamua kuongeza muda wa umiliki wa vitalu hivyo kwa miaka mitatu kwa kufuata utaratibu wa zamani.

  “Kitendo hiki cha kuongeza muda wa umiliki wa vitalu kinakiuka na kutozingatia Azimio la Bunge na kinaingilia madaraka ya Bunge... na maelezo aliyotoa Waziri kwamba serikali ina makubaliano na Chama cha Wawindaji (TAHOA), hayana msingi wowote kwa kuwa makubaliano yalifanywa miaka 10 iliyopita,” alisema.

  Alisema kwa uamuzi huo, Bunge limeazimia kuwa barua iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori namba HD 204/401/100 Januari 16, mwaka huu ya kuongeza muda wa umiliki vitalu kwa kampuni za uwindaji, ifutwe mara moja kwa kuwa inakwenda kinyume na Azimio la Bunge.

  Pia alisema kwa kuwa Waziri hakujenga ushirikiano wa mihimili miwili ya Bunge na Utawala kwa kuwasiliana na Bunge kwanza kabla ya kuongeza muda, Bunge hilo linakemea tabia hiyo ambayo ni ishara ya kudharau uamuzi wake. Hata hivyo baadaye alifuta kifungu hicho baada ya Waziri kuomba radhi.

  Akijibu hoja, Waziri Mwangunga, kwanza aliomba radhi kwa kitendo cha wizara yake kuongeza muda wa umiliki wa vitalu hivyo vya uwindaji wanyamapori na kuongeza kuwa hawakufanya hivyo kwa ushawishi wa mtu wala dharau kwa Bunge, bali ilitokana na mazingira halisi.

  Alisema baada ya kuunda Kikundi Kazi cha kuangalia suala hilo la ugawaji, kiliishauri wizara ianze kugawa vitalu hivyo 2010, lakini baadaye wizara ilibaini kuwa katika muda wa kusubiri wamiliki wapya waanze rasmi kutumia vitalu hivyo, serikali itapoteza mapato mengi, hivyo waliomba ushauri kwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, juu ya kuongeza muda wa ugawaji vitalu hivyo.

  Hata hivyo, alisema wizara yake haina tatizo na mapendekezo ya kufuta muda ulioongezwa katika ugawaji wa vitalu hivyo, ila alitahadharisha athari zinazoweza kujitokeza ambazo ni pamoja na wadau wa uwindaji kwenda mahakamani kutokana na sheria kukiukwa, watalii wawindaji kususia Tanzania na ujangili kuongezeka.

  Naye Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), alisema hakuna sekta ambayo inalitia hasara taifa kama ya utalii, kutokana na fedha zake nyingi kuishia mikononi mwa wageni. “Kwa hili wizara imekiuka, haikutekeleza Azimio la Bunge na imetekeleza kwa maslahi ya wengine ... ni lazima viongozi wawe makini.”

  Alishukuru hatua ya Waziri kukiri kuwa amekosea kwa kuongeza muda wa umiliki wa vitalu hivyo bila kushauriana na Bunge. “Ila kipindi kinachokuja kiongozi akikiuka madaraka na Haki za Bunge, bora aje na barua yake ya kujiuzulu.” Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alitaka barua iliyoandikwa ya kuongeza muda huo ifikishwe kwanza kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa kuwa kitendo cha kwenda kinyume na maagizo ya Bunge ni kosa kubwa.

  “Kwa kitendo hiki cha leo kwa mujibu wa kanuni za Bunge hili, Waziri Mwangunga angeweza kwenda Keko kwa siku saba, ila jamani tukiri uungwana, kwa kuwa ameshaomba radhi basi yaishe,” alisema. Awali Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alisema hakuna haja kwa wabunge kulumbana, kwa kuwa hoja ya msingi ni ugawaji wa vitalu kufanyika 2012 na kuanza kutumika 2013, hivyo ipunguzwe na vigawiwe 2010 na kutumika 2011. “Mawaziri hili liwe fundisho, Bunge liko makini sana, muwe makini tusifike hapa tena.”

  Akifunga mjadala huo, Mzindakaya alizitahadharisha Kamati za Bunge kutovuka mipaka na kuchukua uamuzi ambao unakwenda kinyume na ambao umewekwa na Bunge, kwani hazina mamlaka ya kutengua maazimio yoyote ya Bunge. Mwangunga pia aliwasilisha rasmi na kusoma kwa mara ya pili Muswada wa Wanyamapori wa mwaka 2008 ambao Kambi ya Upinzani bungeni imejipanga kutouunga mkono na utajadiliwa kwa siku mbili na uamuzi wa kupitishwa kwake utatolewa keshokutwa.
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280

  Unaweza usilielewe lakini hilo linaakisi kuchoshwa kwa kwa wananchi
  na hili suala la uchumi mzima kumilikiwa na wageni huku wazawa wakiangalia tu. Pole, kama hulielewi, nenda kidogo Bolivia pale utajua mzee mzima Ivo Morales anamaanisha nini. Ni mapambano tu kama mengine!
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Bunge linaingiliaje utendaji wa serikali? Hivi si vyombo viwili tofauti? Bunge litaitoleaje maamuzi serikali nje ya kupitisha sheria?
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi naona hawa wabunge wanajisahau. Serikali ni watendaji na si watekelezaji wa maazimio ya bunge. Hao wanaopigia kelele hivyo vitalu wengi wao wanatafuta nafasi ya ulaji wala si kuangalia maslahi ya taifa!

  Amandla............
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Yale yale. Tutaishia mahakamani. Badala ya kuangalia uwezo na kuweka sheria zitakazohakikisha sustainability ya maeneo hayo sisi tunang'ang'ania ulaji kwa msingi wa rangi yetu!
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wazawa ni mimi mlala hoi, ninayepata mlo mmoja kwa siku, ninayepinda mgongo shambani/kazini kutwa kwa malipo kiduchu ni mimi ngozi nyeusi ambaye baba, babu, baba ya babu na babu ya babu yangu mzaa mama na mzaa babu walizaliwa kamachumu muleba na kufia muleba, na mimi ningali Tanzania na wale wengine wote wanaofanana na mie ndio wazawa, usipoelewa hilo basi kammulize Simba
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Akiomba kusamehewa, Mwangunga alisema yote yalifanywa kwa nia njema. Naona nia njema imekuwa utamaduni na uhalali wa maovu yote tunayofanyiwa na wakubwa hawa. Alianza Lowasa akasema serikali kusaini mkataba na Richmond ilikuwa kwa nia nzuri ya kuliepusha taifa na giza baada ya mtera kukauka, juzi Pinda kaangua kilio barazani akidai kauli aliyotoa usukumani aliitoa kwa nia nzuri ya kuwatisha wauuaji wa ndugu zetu Albino, Lipumba naye akaja na yake kutaka kubebwa na chadema huko Mbeya kwa madai kuwa walimuwekea pingamizi Shitambala kwa nia nzuri ili upinzani uchukue kiti cha ubunge. Sitashangaa kesho akisimama Mzindakaya na kusema pesa alizokwapua BOT ilkuwa kwa nia nzuri ya kuwawezesha wananchi wa jimbo lake kupata maziwa!
   
Loading...