News Alert: Masha awasalimia Keko.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News Alert: Masha awasalimia Keko..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 26, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kutoka mwanakijiji.com

  Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha leo ametembelea gereza la Keko ambapo mawaziri wawili wa zamani wanashikiliwa rumande wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 13 dhidi yao kutokana na matumizi mabaya ya madaraka yaliyoisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi. Mawaziri hao wa zamani Bw. Basil Mramba (Rombo - CCM) na Daniel Yona walishindwa kupata dhamana jana baada ya kila mmoja wao kutakiwa kuweka dhamani ya karibu shilingi bilioni 3.

  Bw. Masha aliyeenda gereza hilo kwa gari lake la binafsi na ambaye hakuwa ameonekana kuvaa "kiofisi" alishindwa kueleza ni kwanini kama amekwenda kule kikazi aende kwa kutumia gari la binafsi na bila ya kutoa taarifa ya awali kwa umma. Bw. Masha alishindwa kuelezea hilo hasa ikizingatiwa kuwa katika eneo la Dar kuna magereza mengine makubwa mawili ya Ukonga na Segerea ambayo angeweza kuyatembelea lakini aliamua kwenda kwenye gereza la Keko ambapo "jamaa" zake wanashikiliwa.

  "Sisi hatujui alizungumza nao nini, kwani alipata nafasi ya kuzungumza nao" kimeelezea chanzo chetu si mbali sana na kuta za gereza hilo maarufu ambalo pia siku ya jana lilipata ugeni wa Dr. Ferdinand Masau ambaye alishindwa dhamana katika kesi iliyofunguliwa dhidi yake na NSSF. Dr. Masau ametimiza masharti leo na sasa yuko nje kwa dhamana.

  "Jinsi alivyokuja kwa kweli aidha alikuwa na ujumbe fulani ambao ni yeye tu angeweza kuutoa au alikuja kuchukua ujumbe kutoka kwa washtakiwa" amesema afisa mmoja ambaye ana uhakika wa anachosema.

  Wakati huo huo Mawakili wa kina Mramba na Yona wamefika tena kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ambapo wameomba kupata mwenendo wa kesi hiyo ili waweze kupitia misingi ya dhamana iliyodaiwa na mahakama hiyo dhidi ya wateja wao. Haki anayesikiliza kesi hiyo Bw. Hezron Mwankenja amewaagiza makarani wa mahakama hiyo kuwapatia mara moja mawikili hao nakala hiyo.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya mahakamana Mawakili wa kina Mramba wanataka kukata rufaa kupinga kiasi kikubwa cha dhamana hiyo ili hatimaye wateja wao waweze kuachiliwa wakingojea kesi yao kutajwa tena Disemba 2. Vyanzo vyetu vimesema kuwa Mramba ni lazima awe nje kabla ya Ijumaa hii ili aweze kuhudhuria harusi ya binti yake anayeolewa na kijana wa Elvis Musiba siku chache zijazo.

  Kama KLHN ilivyoripoti wiki iliyopita, kufikishwa mahakamani kwa mawaziri hao kulicheleweshwa wiki iliyopita kutokana na "send off" ya binti huyo wa Mramba ambayo ilifanyika katika hoteli ya Movenpick na kuhudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  If this report is accurate, there is an appearance of gross impropriety.

  There appears to be a great effort to conceal the visit - or at least make it unofficial-. At a time when there are reports that judicial decisions are being made by remote control by the executive arm of the state, it is troubling to see Mr. Masha meddling in the case.One would be excused for thinking that Mr. Masha is being used as a go between between the powers that be in the Kikwete administration -possibly Kikwete himself- and the accused.If there is a need for this at all, which is rather suspicious, it should be done with full transparency and in official capacity.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Hmmm! Inatia shaka hii. Kenda kuwatoa wasiwasi kwamba dhamana yao itapunguzwa ili warudi majumbani wakale kuku kwa mrija. Hatujawahi hata siku moja kusikia Waziri wa mambo ya ndani anaenda Keko kuwatembelea walala hoi waliowekwa rumande iweje leo akawatembelee vingunge!? Katumwa na nani kwenda kuwatembelea huko Keko? Sidhani kama kaamua mwenyewe kwenda kuwatembelea.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Early signs of trickery..........
   
 5. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi allegiance ya huyu Masha sasa hivi, kwa siasa za makundi ya ccm bado ipo kwa EL au ameshadrift kwa JK.

  Maana kwa siasa za makundi ya ccm hii visit "ya kinyemela" inaweza kua na maana nyingi tofauti.
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yote yanadhibitisha wasiwasi wetu kwamba ufikishwaji wa watuhumiwa hawa mahakamani ni vitendo vya kisanii tu, hakuna 'seriousness.'Tutafika tu hata kwa kusuasua.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Naam wana wasiwasi mkubwa na yatakayojiri 2010 hivyo wanataka kujisafisha kwa kutumwagia changa la macho ili kutuzuga Watanzania na tuanze kuandamana ili kutoa pongezi kwa Wakuu na CCM kwa 'kazi nzuri' ya kupambana na mafisadi na 'kulinda maslahi' ya nchi ili warudi tena madarakani 2010, safari hii tuko macho na hatuko tayari kuzugika na viini macho vilivyojaa usanii wa hali ya juu.
   
 8. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna harufu kali ya usanii.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  ...........ACTION.........kama nilivyohisi huenda sasa tamthilia iliyopangwa kwa muda mrefu kukidaiwa kukusanywa kwa uchunguzi kama ndivyo ndio sasa mchezo umeanza ni hisia tu.
  Ila pengine ameenda kuwambia wajikaze ndio ukubwa.Na huyu jamaa kama anawakumbatia waliotapakaa mivi basi ajue na yeye yatamganda.
   
 10. A

  Alpha JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  This is where the media needs to go all out and continue to run with this story day after day. Make sure people know what has happened and pressure Masha to explain his actions.
   
 11. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Masha ameenda kutumbelea wabunge wenzake na kuwoonea hali... dont read too deep into it, ni kawaida sana kwa hili kutokea...
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani labda kaenda kuangelia tuu hali ilivyo.. It gives a wrong image kwa yeye kama waziri coz its not exactly fair kwa watuhumiwa wengine waliopo rumande lakini....... Sio big deal
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Pundit nakubaliana kwa kiasi flani kuhusu maelezo yako...Ila kwa upande mwingine nakuwa sceptical...Unajuwa mara ya kwanza wengi wetu hapa tulisema hii ni dili imepangwa na ni changa la macho...Lakini tukitumia logic reasoning hapa unaweza kuona kuwa kama kaenda kuwatembelea basi ni kwasababu labda ya urafiki wa kibinadamu na si kwamba eti kuna habari wanapelekewa ama anakwenda kuchukuwa.
  Kama thats the case kwamba Masha alikwenda kupata nyeti na kupeleka habari ama kuchukuwa...Then inawezekana walishtukiziwa na wao walikuwa hawajui kuwa watakamatwa na kufungufuliwa mashataka na hivyo kuondoa ile notion kwamba deal ilishasukwa kuwa wakamatwe lini nk.
  Haki ya kutembelewa wanayo...Lakini Masha kama waziri wa mambo ya ndani kwenda kuwatembelea inaweza kuzua matatizo kutoka kwa wananchi na hili walitakiwa wajuwe.
  Kusema kweli upo pia uwezekano (japo mdogo) wa kwenda kuwaambia kuwa mambo ni mbaya.
  Wakati kauli ya Mramba kuhusu ununuzi wa ndege mimi nilidhani aliwaambia wananchi wale mboga za majani, kumbe alimaanisha wananchi wale majani kama ya ng'ombe na mbuzi? Hili linapelekea wananchi kutokuwa na huruma kwake.

  Pia kama Masha anatumiwa na JK kuwa kama kiunganishi kati ya serikali yake na watuhumiwa...Hili si litakuwa ni kuchemka kwa hali ya juu? Ama si serikali ya jamuhuri inayowafungulia mashataka kina Mramba?
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Matatizo mengine yanatengenezwa na wakubwa wenyewe hawa kwa kuendekeza usiri usio mpango. Watanzania tunajuana ujamaa wetu kwa hiyo swala la mtu kumtembelea colleague wakati wa matatizo si kitu kigeni.

  Lakioni Masha kama waziri, ili ku clear the air, angesimama kwa dakika mbili tu kuwaeleza waandishi wa habari kwamba amekuja kibinafsi kuwajulia hali wabunge wenzake katika kipindi cha matatizo.

  The secrecy and blanket of information starvation gives people a reason to read all sorts of ulterior motives and conspiracy theories.

  One sure way to kill speculation is to provide the truth, in the absence of information people will concoct all kinds of stories.As Niels Bohr aptly put it, nature abhors a vacuum.

  Transparency in every detail is needed now more than ever.
   
 15. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  tangu awali nina mashaka sana na Masha...sielewi kwa nini Kikwete alimjulisha..
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kimaadili hata kama hao watuhumiwa ni marafiki wa Masha haileti picha nzuri kuwatembelea. Hasa ukizingatia Masha ni waziri wa kusimamia magereza. Ni rahisi kufikiri kwamba kuna some favors ambazo ameenda kuzifanyia arrangement, au taarifa nyeti kama wachangiaji wengine walivyodokeza. Kimaadili na kiungwana kabisa angesubiri ile tarehe kesi itasikilizwa tena akaongee nao pale kisutu.

  Note: Maadili sio sheria, hivyo basi hata kama kisheria sio kosa kimaadili inaweza kuwa kosa.
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Kikwete alimjulisha nini?
   
 18. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mtoeni Kikwete kwenye equation. Mnamsingizia sana sasa aaah!

  Inawezekana bwana waziri kaombwa na besti wake Yona Jr, au labda kaamua tu kwenda kumjulia hali baba ya mshikaji wake. That's what friends are for.
   
 19. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  The guy(Masha) need to come with a good reason for that " private visit" he made to that prison. Take note that it does not make sensea minister responsible for among others magereza. Even if it is a private visit on his capacity as an ordinary citizen, the issues is; is it just a mere coincidence or something fishy is going arround? was it an offcial time to visit remandees? or should we treat it as an covert mission? if it is , then who assigned him to do that "fact finding mission"

  Masha you need to come out with clean reason otherwise, we have the right to suspect you and start to draw the dots ...
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ruksa kucheza kila aina ya mchezo wautakao.
  Hata ile siku ya kwanza mlipo kaa na makalio yenu makubwa kwenye viti vikubwa kupanga mbinu za kutugeuza watanzania wote ndondocha aumisukule wenu, mlidhani ni siri kuu inayolindwa kwa nguvu zote na nembo ya Baba na Mama.

  Kende zenu, narudua kende tena zenu wote kwa mpigo.

  Iweje leo kati ya visiki wenye midomo michafu isiyo na adabu kwa watanzania wako kwenye vyumba vya VIP kule jela??
  Nani anakula nyasi?

  Nijuavyo mimi CCM kama chama cha siasa hakina nguvu ya kujisima muda wote in our life time.CCM tayari kinaonja Alamana Za Nyakati, lakini kwa kuwa ni chama dola kinapuuza Alama hizo kwa kudhani kwamba miguvu ya kijeshi kipolisi na kishushushu zina uwezo wa kutudumisha ununda wao dhidi ya AZN.
  Kukalishana kwenye lile Bench tu ni dalili tosha kwamba huko chumbani kwao CCM mambo si shwari hata kidogo.
  Naamini kabisa kila asubuhi kuna watu wanakula pushup za nguvu, makofi mazito ya mashavuni na viboko vya matakoni huku wamechojoa kaputula zao. Subra imewaishia, ushetani ulio asili yao sasa unatawala.

  Kwa muda mrefu CCM wametii kanuni kuu ya Fisi.

  Fisi hata aumwe njaa vipi kamwe hali mzoga wa fisi mwenzie. Pamoja na ufisifisi wake tamaa na hamu ya kumla fisi mwenzie inakula nyongo na kuua hamu ya mlo.
  Kuanza kukalishana kwenye lile benchi ni dalili moja kwamba Fisi hawa wameanza kutamaniana kiasi kwamba hawaoni vibaya kugeuzana kitoweo kwa zamu. Katika jamii ya Mifisi yenye uroho wa kihayawani hiyo si dalili nzuri ya kudumisha umoja wao wa kifisi. Kanuni ya kuto mtamani fisi mwenzio kwa nia ya kumgeuza kitoeo ndiyo msingi mkuu wa umoja wa Mafisi wote duniani.
  Kukiukwa kwa msingi huu mkuu kutaleta hofu kiwewe na MFADHAIKO utakao watia katika Mode ya kutoaminiana na hivyo kumfanya kila Fisi atumie ukali wa meno yake na urefu wa makucha yake kulinda himaya yake bila kujali gharama itakayo ukabiri umoja wao wa kifisi. Jambo hilo ni lazima lilete mvurugano na kusambaratika.

  Bwanamdogo Masha amesahau kwamba wazazi wake waliishi Ughaibuni si kwa kupenda ila ni kwa matokeo ya Uhasama na vita za kiitikadi ndani ya siasa za kale enzi ya TANU.
  KamA anachochoto cha kujifunza si katika historia ya Tanzania bali katika historia ya familia yake mwenyewe.
  Naamini kabisa historia itajirudia,safari hii itakuwa zamu yake Masha mwenyewe kujitoma ughaibuni.
   
Loading...