News Alert: Dira ya Dunia, BBC Kuonekana kwenye Luninga ya Star TV

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Kwa mujibu wa matangazo ya BBC yanayoendelea hewani hivi sasa, kipindi maarufu cha Dira ya Dunia cha BBC Kiswahili Service kitaanza kuonekana kwenye TV kupitia Star TV kuanzia Jtatu ijayo! Bila shaka, hii ni fursa mzuri kwa wale wote tunaopenda kufuatilia habari za BBC! Well Done BBC.....hili ni jambo ambalo nilikuwa nikijuliza zaidi ya miaka mitano iliyopita kwamba ni kwanini BBC Kiswahili haioneshwi kwenye TV!
 
Safi sana BBC angalau tutaweza kupata habari za kina sio hz za kulambishwa na tbccmagamba na vibaraka wao excluding mlimani tv!!!!
 
Hii kitu itakuwa poa sana....na stesheni zetu zina bahati kwani jamaa(BBC) watakuwa wanarusha matangazo yao saa 3 usiku otherwise, habari zao(za local TV) za kuchakachua zinazooneshwa saa 2 ingekuwa ndo bye bye tena!
 
ni hatua nzuri ila bbc kwa ujumla taarifa nyingi za africa wanatoa za matatizo tu mafanikio yetu hawayasemi hata kidogo mpka wananchi wa huko wanafikiri rafiki zetu ni wanyama na kupigana kila siku kidogo CNN.
 
.....Safi sana BBC SWAHILI.... Hatutoangalia tena tv za uchakachuzi wa matukio muhimu....

......Nahisi hapa mkono wa Tido MUHANDO umehusika....
Kwaheri tbccm, cloudsisiem, n.k
 
Mi sijaelewa wadau,je watakuwa wanaunganisha redio na tv au itakuwa tv pekee na redio kivyake
 
Mbona BBC kiswahili nayo kidesign si ya kihivyo katik radio.Huwa ina agenda za hawao weusi walioajiriwa kwa sana.Akina Nkamia si walikuwa huko, sasa wapo wapi?
 
ni hatua nzuri ila bbc kwa ujumla taarifa nyingi za africa wanatoa za matatizo tu mafanikio yetu hawayasemi hata kidogo mpka wananchi wa huko wanafikiri rafiki zetu ni wanyama na kupigana kila siku kidogo CNN.

mafanikio gani mlionayo ninyi?
 
mafanikio gani mlionayo ninyi?

sizungumzii kwa tanganyika tu nazungumzia kwa habari za africa kwa ujumla nakumbuka hata kipindi kile cha kombe la dunia south africa bbc walikuwa wanaonyesha zile sehemu mbaya mbaya tu mpka wananchi waingereza wenyewe wakawa wanashangaa inakuwaje south africa waweze kuandaa kufanya maandalizi wakiwa namna hiyo ila wananchi walivyoenda wenyewe walishangaa ni tofauti na ilivyokuwa inaonyeshwa muulize hata raia wa uingereza atakuambia dont trust bbc kwa international news hilo linajulikana kabisa muulize huto tido akuambie zaid.
 
Back
Top Bottom