Newala, Mtwara: Tani 68 za Korosho zarudishwa kwa Wakulima zikidaiwa hazina ubora

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Zaidi ya tani 68 za Korosho zilizokuwa zimepimwa na wakulima katika vyama vya Msingi Chemana na China kata ya Chitekete Halmashauri ya wilaya Newala Mkoani Mtwara, zimerejeshwa kwa wakulima baada ya kukataliwa na Meneja wa maghala kuingizwa kwenye maghala makuu ya TANECU- Newala kwa kinachodaiwa kukosa ubora.

Mwenyekiti wa chama cha Msingi Chemana Abilahi Ibadi, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima ni tani 15.6.

Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi wa chama cha Msingi China Juma Samli, amesema Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima walio chini yake ni Tani 53

Viongozi hao wa vyama vya msingi wamesema licha ya kufanyika kwa jitahada mbalimbali za kuzichagua na kuzianika ili zikubaliwe kuingizwa kwenye maghala makuu kuuzwa,lakini juhudi zao hizo zimegonga mwamba.

Wakizungumza kwa nyakati tofuati, wakulima hao wameelezea kusikitishwa na hali hiyo,kwani mategemeo yao yalikuwa ni Korosho hizo kuuzwa ili wajipatie kipato kitakachowawezesha kujikimu na kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kununua pembejeo za kilimo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

"Wahindi walikuwa wanasafisha korosho mpaka wanazitafuta na kumaliza zote, Korosho zetu siyo chafu ni nzuri,ukiziangalia ni kavu, hazina unyevunyevu, lakini zimerudi watunza maghala wanazikataa, hivi mkulima ana soko uko nyumbani!?, lengo la mkulima ni kuuza atatue matatizo yake watoto waende shule" amesema Fakihi Ahmadi Mpwato maarufu Mr.Kamunga, Mkulima wa Kijiji cha Chitekete.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
149738.jpeg
 
Back
Top Bottom