Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,806
- 11,968
Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainabu Telack akiwa kwenye kikao cha utekelezaji wa mpango wa kuboresha usimamizi wa huduma za ugani kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani, ameagiza kuteketezwa kwa korosho tani 24 zilizopo ghala kuu la Mtama, lililopo halmashauri ya Mtama wilayani Lindi.
Hayo yamejiri baada ya Korosho hizo kupelekwa kwenye ghala kuu la hazina zikiwa na Grade One na Grade Two na baadae zikapoteza ubora na kushindwa kuuzika kwenye minada.
Sambamba na hilo Telack amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa wa Lindi kuwawezesha maafisa ugani ili weweze kuwasaidia wakulima kwenye zao la korosho.
Chanzo cha habari Mashujaa FM