New Series I: Madudu na sifa za Edward Lowassa!

New Series I: Madudu na sifa za Edward Lowassa!

Le Grand Alexei

Senior Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
116
Reaction score
83
Elisa,

Aliyewasaidia waTz kupata maji ya Victoria si Lowasa, ni rais Mkapa kwenye ahadi yake ya 2000 kwa mkoa wa shinyanga. Wakati huo Lowasa alikuwa kama sio bench ni ofisi tofauti kabisa. Baada ya uchaguzi wa 2000 ndipo Lowasa na Dk Limbu wakaingia wizara hiyo.

Utekelezaji wa mradi wa maji ulianza 2001 wakati wa Lowassa na Diallo kama NW.

Kama nilivyosema awali, wengi mnaompigia jalamba huyu Mhe ni adui zake (kwa kujua au kutokujua) au ni wapinzani wa ccm (kwa kujua au kutojua. Kama ccm wakamteua Lowasa kugombea urais ataanguka asubuhi tu! Madhambi aliyowafanyia watanzania ni mengi afadhali wakuweke wewe Elisa hauna historia ya kuwakosea waTz.

Sifa mnazompa lowasa hanazo, alibahatika kuwa kufanya kazi na wasaidizi makini na pia Rais makini. Wengi wetu tunasahau au hatujui Lowasa na matatizo yake ya nyuma: alipokuwa tume ya Loliondo, na alivyokula hela za waarabu na kuwaacha hadi leo wapo Loliondo badala ya ilivyotarajiwa na waTz (soma tume teule ya Bunge kuhusu Loliondo) ipo hansard za bunge. Pia alipokuwa AICC kama CEO alivyopoteza fedha za ujenzi wa staff na baada ya hapo alivyojinyakulia ardhi ya AICC na baadae kuuziwa Themi Hill Suites, na wengine walio jirani ardhi iliyokuwa ya AICC!

Pia msaada wa ujenzi wa kiwanda cha vyandarua Sunflag, Sumitomo waliwekeza na serikali ya Japan na WB wakatoa grant, lowasa akalazimisha kuuziwa hisa kiwanda hicho bila kutoa hata senti kumi.

Alipokuwa wizara ya ardhi, mnakumbuka alivyokusanya fedha kwa kuuza maeneo na haraka haraka kajenga majengo masaki ambayo yalileta skandali kubwa. Ubalozi wa Afrika kusini walipangisha jengo lake kwa gharama kubwa na dili hiyo ilifanyika yeye akiwa waziri wa ardhi.
Nyerere alimuona kama mwizi tu huyo, akamchomoa kutogombea urais 1995. Wizi wa mali ya umma kaanza miaka mingi.

Hata unapodai kuwa mchapa kazi sikuelewi. Ungesema ana maamuzi ya pupa tu. Mfano, alipoamuru jengo moja karibu na mess ya polisi livunjwe kwavile wahindi walikataa kumlipa fedha; maamuzi yake yamegharimu wizara na serikali mabilioni kwa amri ya mahakama.

Leo tunalia elimu kuanguka; kisa kimojawapo ni ujenzi wa pupa wa shule za kata! Aliacha mpango wa WB na Nordic countries na kutaka utekelezwe kwa jazba! Mradi wa kuyelekezwa kwa miaka 10 yeye kaamua ufanyike miaka 2! Matokeo yake, hakuna waalimu, vifaa, maabara, uwezo kukosekana wa kuwachukua wanafunzi kuelndelea na kidato cha 5 na sita! Leo mnaunda tume kutafuta mchawi! Mchawi ni Lowassa na maamuzi yake ya pupa.
Madhambi yatoikanayo na uamuzi wa hovyo alioufanya huyo ndugu yako ni mengi na pia utajiri alio nao wa kugawa fedha kwenye makanisa hauelezeki. Anatoa fedha kwa wakristo akidhani watamsaidia. Hajasaidia msikiti hata mmoja kama kweli angekuwa na nia ya kusaidia jamii ya nchi hii. Anafanya akijua eti zamu ya mgombea kutoka kwenye ukristo ndilo linalofuata! Anasikitisha kwa kuona karibu na kijinga hivyo! Ni kati ya wanaochochea mgawanyiko wa dini nchini!

Hana maana wala sababu ya kuendelea kuhadaa waTz. Ngoja ufike muda uone kivumbi. Kajitahidi kuwanyamazisha wahariri wa magazeti mengi, hajui wakati wa chaguzi magazeti yote huhuishwa na mengine kufuka kwa kazi moja tu ya uchaguzi! Kuhonga kuna mwisho wake.

Leo wahariri wanadhuriwa na kulalamika kunyamazishwa! Ni wao wameyatafuta hayo, unakula fedha ya mtu halafu unafanya kinyume na matakwa yake unatarajia nini? Kwenye fedha mtu atakufanyia lolote akiona unataka kumdhulumu kinyume na matarajio yake.

Huu ni mchango ulioandikwa jana kwenye Jukwaa la Wanabidii na bwana Tony PT. Nitaendelea kutoa muendelezo wa sifa, wajihi na uozo wa watu mbalimbali waliojitokeza kuutaka Urais.
 
Siasa za bongo!

Maandalizi ya 2015 yanazidi kushika kasi miongoni mwa magamba!

Hakuna anaetufaa kati yao!
 
Edward Lowassa, huyu jamaa ana utaka urais kwa gharama yoyote ile iwayo. Yuko tayari kuingia ikulu kwa kutumia njia zozote zile, ziwe halali au hata za kimafia.

CCM wenyewe (wenye CCM) wanahofu kubwa sana juu ya nini kitatokea iwapo hawatompitisha Lowassa kuwa mgombea wa kiti cha urais.
 
Nimeelewa kidogo sana kutokana mwandishi hajaandika vizuri.lakini kama nihivyo bas hu bwana hafai ila siasa za tz usishangae akawa rais.
 
Kuna wapiganaji wengi sana wameweka silaha chini! kuna watu ni kama wamekatishwa tamaa na hulka za Watanzania hasa mwitikio wao kwenye mambo nyeti Invisible anaangukia hapa pia.

Kwa namna wapiganaji walivyotawanyika bila mipango maalum,kwa namna majemadari wetu wengi kukosa mbinu za kuwaamsha Watanzania ili reaction zao zibadilike.

Sidhani kama tunaelekea kuzuri,zimetumika juhudi kubwa kuunga mkono upinzani lakini juhudi hizo zinashuka kwa rate ya kutisha!

Mwisho kabisa dakika hii kuna fisadi ktk wale waliovuliwa nguo miaka kadhaa iliyopita anaona aibu kusimama popote?
nguvu zao zimetoka wapi? Tumefaidika nini tulipowataja kama Taifa? Kama hakuna kilichofanyika plan B ilikuwa nini? au plan B ndio hii ya kumsusia ngedere shamba?
 
Last edited by a moderator:

pole sana kwa kukata tamaa. mkono mtupu haulambwi. lowasa ametoa hela nyingi sana alizotuibia watanzania makanisani na sasa hivi haya unayoyaona ni matunda yake tu. kwangu hilo sio tatizo ila the most interesting ni jinsi huyo mungu anayetolewa hizo hala anavyopenda na kushabikia/kuchekelea hela za kudhulumu
 
Tumechoka na habari za Lowasa ndani ya jf, why don't we talk of issues instead of people. Najua kuna watu wameajiliwa kupamba na kubomoa kupitia jf lakini nisingependelea jukwaa letu liwe ndo battleground.
 
Atasubiri sn , hakuna mtu aliyekuwa waziri mkuu akawa rais toka tupate uhuru , muulize Raila Odinga kilichomkuta . tupo 45 million tunataka Sura mpya , mawazo mpya . Acha copy & pest
 
Ukiniletea mtu ambae hajawahi kufanya makosa ntakuonesha Papo hapo mtu ambae hajawahi kufanya Chochote- Mzee Maganga Songoro (1938-2009)
 
pole sana kwa kukata tamaa. mkono mtupu haulambwi. lowasa ametoa hela nyingi sana alizotuibia watanzania makanisani na sasa hivi haya unayoyaona ni matunda yake tu. kwangu hilo sio tatizo ila the most interesting ni jinsi huyo mungu anayetolewa hizo hala anavyopenda na kushabikia/kuchekelea hela za kudhulumu[/color[

Dah! Maneno hayooo.

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
pole sana kwa kukata tamaa. mkono mtupu haulambwi. lowasa ametoa hela nyingi sana alizotuibia watanzania makanisani na sasa hivi haya unayoyaona ni matunda yake tu. kwangu hilo sio tatizo ila the most interesting ni jinsi huyo mungu anayetolewa hizo hala anavyopenda na kushabikia/kuchekelea hela za kudhulumu

Sent from my GT-S7562 using Tapatalk 2
 
Kujua tunajua, lakini tunatakiwa kutumia vizuri taarifa tunayoijua. Haitoshi kujua tu halafu full stop. Hapana, lazima tuende zaidi ya kujua. Ukiwa na mke mzuri chumbani halafu full stop, hautaelweka.
Kuna watu wengi hawakuelewa kuwa maji ya ziwa Victoria kuletwa Shinyanga sio mpango wa EL. Wakampa sifa lukuki kama vile wasivyoelewa kuwa wazo la kujenga UDOM sio la JK, wanaendele kumpa sifa feki JK.
Kuna watanzania wanadhani pupa ndiyo kazi bila kuja gharama zake kwa Taifa. Utendaji wa EL haujapata kutafsiriwa kama ni PUPA badala yake ikasadikika kama mwenye uwezo wa kutoa maamuzi magumu. Lazima tujue tutafsiri tunachojua na kisha tutumie talifa tunazojua kwa busara. Lakini busara ni nini? Kila mtu hufanya mambo tofauti akiwa na hakika kuwa akifanyacho ndiyo busara. Pia wenye busara katika jamii yoyote duniani ni wachache kuliko walionayo. Mbaya zaidi katika Tanzania wajuvi wa mambo hujikomba kwa wakubwa wakidhani hiyo ndiyo busara. Wachache wenye uthubutu wa kumwambia 'Hiiii, Mfalme uko uchi'. Ndiyo hao wanaong'olewa meno kucha macho na kutupwa majalalani wakikosa hata mtetesi.
we all know lowasa ni mwizi. full stop.
 
nimekuona huna maana baada ya kukutana na huu upuuzi wako. huwezi kusema watu wanampa sija feki kikwete. mtu ambaye ameanzia from the scretch na kusimamia kila alichokianzisha mpaka kufikia hapa tulipo na kuona UDOM ikisimama. kuwa na wazo na utekelezaji ni vitu viwili tofauti kabisa. by the way how many mawazo are out there? hata wewe unaweza kuwa na wazo la kujenga kanisa hapo ulipo, na linabaki kuwa wazo tu na halina garama yoyote zaidi ya kuwaza. hivi unajua hata muasisi wa wazo la serikali ya majimbo ni Idd Simba? NAONA MNAJARIBU KUTWIST KILA ZURI ALILOFANYA KIKWETE. SHAME ON YOU.
 
CCM ni machizi lakini kumteua LoWaSsa kugombea urais kwa Tiket ya CCM hawawezi fanya hivyo!
Lowassa ndo injinia wa kuivuruga CCM
Lowassa ndo mzee alie zalisha makundi
Lowassa ndo alifanya juu chini kumwaribia PM pinda iliaonekane ovyo
Lowassa ndo mpikaji udini nchini kwa kutumia Dini kuivuruga serikali lakini ndani ya Bunge kimyaaaaaa
Lowassa ndo Mr Dowans aka Richmond maumivu yake tunayabeba mpaka kesho
Lowassa ni silent killer anaeutaka urais kwa cost yoyote But we will be very kin on that
 
Back
Top Bottom