Elisa,
Aliyewasaidia waTz kupata maji ya Victoria si Lowasa, ni rais Mkapa kwenye ahadi yake ya 2000 kwa mkoa wa shinyanga. Wakati huo Lowasa alikuwa kama sio bench ni ofisi tofauti kabisa. Baada ya uchaguzi wa 2000 ndipo Lowasa na Dk Limbu wakaingia wizara hiyo.
Utekelezaji wa mradi wa maji ulianza 2001 wakati wa Lowassa na Diallo kama NW.
Kama nilivyosema awali, wengi mnaompigia jalamba huyu Mhe ni adui zake (kwa kujua au kutokujua) au ni wapinzani wa ccm (kwa kujua au kutojua. Kama ccm wakamteua Lowasa kugombea urais ataanguka asubuhi tu! Madhambi aliyowafanyia watanzania ni mengi afadhali wakuweke wewe Elisa hauna historia ya kuwakosea waTz.
Sifa mnazompa lowasa hanazo, alibahatika kuwa kufanya kazi na wasaidizi makini na pia Rais makini. Wengi wetu tunasahau au hatujui Lowasa na matatizo yake ya nyuma: alipokuwa tume ya Loliondo, na alivyokula hela za waarabu na kuwaacha hadi leo wapo Loliondo badala ya ilivyotarajiwa na waTz (soma tume teule ya Bunge kuhusu Loliondo) ipo hansard za bunge. Pia alipokuwa AICC kama CEO alivyopoteza fedha za ujenzi wa staff na baada ya hapo alivyojinyakulia ardhi ya AICC na baadae kuuziwa Themi Hill Suites, na wengine walio jirani ardhi iliyokuwa ya AICC!
Pia msaada wa ujenzi wa kiwanda cha vyandarua Sunflag, Sumitomo waliwekeza na serikali ya Japan na WB wakatoa grant, lowasa akalazimisha kuuziwa hisa kiwanda hicho bila kutoa hata senti kumi.
Alipokuwa wizara ya ardhi, mnakumbuka alivyokusanya fedha kwa kuuza maeneo na haraka haraka kajenga majengo masaki ambayo yalileta skandali kubwa. Ubalozi wa Afrika kusini walipangisha jengo lake kwa gharama kubwa na dili hiyo ilifanyika yeye akiwa waziri wa ardhi.
Nyerere alimuona kama mwizi tu huyo, akamchomoa kutogombea urais 1995. Wizi wa mali ya umma kaanza miaka mingi.
Hata unapodai kuwa mchapa kazi sikuelewi. Ungesema ana maamuzi ya pupa tu. Mfano, alipoamuru jengo moja karibu na mess ya polisi livunjwe kwavile wahindi walikataa kumlipa fedha; maamuzi yake yamegharimu wizara na serikali mabilioni kwa amri ya mahakama.
Leo tunalia elimu kuanguka; kisa kimojawapo ni ujenzi wa pupa wa shule za kata! Aliacha mpango wa WB na Nordic countries na kutaka utekelezwe kwa jazba! Mradi wa kuyelekezwa kwa miaka 10 yeye kaamua ufanyike miaka 2! Matokeo yake, hakuna waalimu, vifaa, maabara, uwezo kukosekana wa kuwachukua wanafunzi kuelndelea na kidato cha 5 na sita! Leo mnaunda tume kutafuta mchawi! Mchawi ni Lowassa na maamuzi yake ya pupa.
Madhambi yatoikanayo na uamuzi wa hovyo alioufanya huyo ndugu yako ni mengi na pia utajiri alio nao wa kugawa fedha kwenye makanisa hauelezeki. Anatoa fedha kwa wakristo akidhani watamsaidia. Hajasaidia msikiti hata mmoja kama kweli angekuwa na nia ya kusaidia jamii ya nchi hii. Anafanya akijua eti zamu ya mgombea kutoka kwenye ukristo ndilo linalofuata! Anasikitisha kwa kuona karibu na kijinga hivyo! Ni kati ya wanaochochea mgawanyiko wa dini nchini!
Hana maana wala sababu ya kuendelea kuhadaa waTz. Ngoja ufike muda uone kivumbi. Kajitahidi kuwanyamazisha wahariri wa magazeti mengi, hajui wakati wa chaguzi magazeti yote huhuishwa na mengine kufuka kwa kazi moja tu ya uchaguzi! Kuhonga kuna mwisho wake.
Leo wahariri wanadhuriwa na kulalamika kunyamazishwa! Ni wao wameyatafuta hayo, unakula fedha ya mtu halafu unafanya kinyume na matakwa yake unatarajia nini? Kwenye fedha mtu atakufanyia lolote akiona unataka kumdhulumu kinyume na matarajio yake.
Huu ni mchango ulioandikwa jana kwenye Jukwaa la Wanabidii na bwana Tony PT. Nitaendelea kutoa muendelezo wa sifa, wajihi na uozo wa watu mbalimbali waliojitokeza kuutaka Urais.