New hit song: Parapanda ya kwao ROSTAM

New hit song: Parapanda ya kwao ROSTAM

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
26,534
Reaction score
61,962
Wasanii.wanaounda kundi la ROSTAM, Roma Mkatoliki pamoja na Stamina wameachia song lao jipya liitwalo Parapanda, ni habari ya mjini kwasasa itafute uthibitishe.

NB
Nimeshindwa kui-upload kwakuwa sio mjuvi wa teknolojia
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu sio ya dunia hii...
Baada ya kuua mbwa kwa ngoma ya "now you know ' na khaligraph jons
Sasa wameamua kuisimamisha dunia na kuiweka nchi katika hali ya tahadhari na hii ngoma ya parapanda..

Sasa hivi kila kona ni parapanda tu.
Nchi nzima ni mwendo wa mateka tu huku tukiimba parapanda
 
PARAPANDA...
Lyrics1:
NYERERE:Karibu Mzee kingunge,kwenye makazi ya milele
Mi huku na mji wangu,tayari unaitwa Nyerere
Nimeshtuka kukuona huku,nini chanzo cha msiba?
KINGUNGE:Ni mipango ya mungu,na nmekumiss swahiba
NYERERE:Vipi nchi yangu mtawala ni chama gani?
KINGUNGE:Bado CCM ingawa kuna upinzani
NYERERE: Unamaana gani,kwani Rais ni nani?
KINGUNGE:Rais ni John,ndo anaongoza usukani
NYERERE: John Mallecela?
KINGUNGE:No, Magufuli, ulimwacha mbunge wa chato sijui unamkumbuka vizuri?
NYERERE: Aaah! ngoja kwanza,unajua haya mambo haya,
Mi nlidhani alipotoka Mkapa angefata Jakaya
KINGUNGE:Jakaya alitawala,akaja akaretire
Nimeacha mambo mengi,yani mambo ni moto, mambo ni fire
NYERERE: Aa'aaa! mbona naskia mambo si sawa
Na ni akina nani wanaojiita hawa,ambao wanajiita ukawa?
KINGUNGE:Ni wapinzani waloungana, lakini hawakumshinda magu
Wengine chama walihama,na bado wakapata tabu (sana)
Kakomesha ufisadi,kaongeza ukusanyaji kodi,hakika wamepata mkombozi ambae atawafikisha nchi ya ahadi
NYERERE: Niliskia skuizi bunge halioneshwi kwenye TV
Inamaana hoja za viongozi wananchi hawaziskii
Mitandao ya kijamii je? vipi inasaidia?
KINGUNGE: Kuna dada anaitwa Mange,please hide my ID
Lyrics2:
NYERERE: Je vipi kaburi langu,tayari wamelijengea?
Na vipi kuhusu mke wangu,Maria wanamtembelea?
KINGUNGE: Kuhusu kumtembelea, hilo toa shaka
Wanamjali na kumlea,tena kwa heshima ya mamlaka
NYERERE: Nimemuona shemeji yangu,ama kweli mnapendana
Penzi la kweli kufa na kuzikana
Vipi mwanangu Makongoro,analinda mali zangu?
KINGUNGE:Bora wakwako mwenzie yupo busy na Tunda
Hivi Julias ulikua simba au yanga?
NYERERE: Kiukweli niliipenda yanga, ila simba ni kisanga
KINGUNGE:hahaa! mwalimu unajua hadi kisanga
NYERERE: Acha hilo naskia mengi, kibamia hadi kudanga
KINGUNGE: HahaHAa
NYERERE:Namuona komba huku,nyimbo za chama anatunga nani?
KINGUNGE:Mi naskia wataisoma namba ila sijui ametunga nani?
NYERERE: Sijakuelewa kwani anaesimamia baraza nani?
KINGUNGE: lipo baraza ila wasanii wanaishi uani
Chorus
Wanamiliki vicent,
Mambo yamebuma mipango haielewekii
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda
Lyrics3:
NYERERE: vipi kuhusu muungano upo au umechuja?
KINGUNGE: Mpemba anauza kariakoo, mzaramo anamiliki duka unguja
NYERERE:vUjinga, Maradhi, Umaskinu bado maadui wataifa? nipe taarifa
KINGUNGE: Ujinga angalau, hao wengine janga la taifa
NYERERE: Kuhusu barabara?
KINGUNGE: zipo
NYERERE: Madaraja?
KINGUNGE: Yapo
NYERERE: kama ni hivyo uchumi umepanda
KINGUNGE: Wanadai cherehani mbili ukiwanazo ni kiwanda
Vyuma bado vipo still na hospitali hakuna vitanda
NYERERE: Bado nina maswali mengi vipi mwenendo wa katiba
KINGUNGE: Mchakato waliusitisha inasemekana walimpiga
NYERERE: Walimpiga nani? na ni akina nani,na ni nini alifanya?
KINGUNGE: Mwalimu sijui ila ni watu wasiojulikana
NYERERE: walompiga risasi Lissu?
KINGUNGE: ni watu wasiojulikana
NYERERE:na ni akina nani waliomteka Roma?
KINGUNGE: ni watu wasiojulikana
NYERERE: na wanaoteka waandishi wa habari
KINGUNGE: E eeh!sijui ni watu wasiojulikana, hahahaa..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom