New Delhi: Tembea ujionee

mkuu especialy Greater Noida pia wana appartments nyingi sana, asee wewe umeishi Delhi miaka ipi mkuu ? mimi nilikaa Hauz Khas, Padmini Enclave , hata Noida nimeishi
dah we jamaa umenikumbusha mbali aise mi nlikaa greenpark main nlikuwa napanda yelow line
 
mkuu umenikumbusha mbali sana nliwai ishi huo mji kipindi fulani kuna sehemu inaitwa INA dah kuna jamaa mmoja anaitwa vicky pale ni maarufu kushona suti balaa ukiwa mwafrika lazma ufike pale
Good experience. Mimi kwa upande wa suti, tulipelekwa DILLIHAAT
 
dah we jamaa umenikumbusha mbali aise mi nlikaa greenpark main nlikuwa napanda yelow line
Aaah. Aaah. Aaaah. Yellow line. Blue line.
 
Namba 14 ni kweli na wala sio Delhi tuu hata mumbai hali sio nzuri ni kuchafu sana hasa maeneo ya andheri East hali sio nzuri mitaa inanuka sana
 
kwahiyo mkuu wewe papuchi ya kiindi hukuiguza
 
Nipo New Delhi. Hivi mliowahi kuishi huju mlizoeaje hiki chakula chenye pilipili?

Naishi kwa mkate na chai.


Fileni kuna ujenzi wa metro yaani tren imepunguza kiaina.
Mkuu na mimi hiyo shida ninayo hapa, tatizo kwangu sio pilipili tuu ila viungo vimezidi hadi inakua kero
 
Hiyo namba 7 kama ni kweli basi ina maana wakaazi wa New Delhi wote wana kansa?!

Namba 9 upo sahihi kabisa,India madereva wengi wanaendesha Magari huku wanapiga honi hovyo tu! Niliwahi kumuuliza Muhindi mmoja "kwanini mnapiga honi hovyo?" Akanijibu hata yeye hajui!! Amezaliwa nae amekuta tu hiyo tabia ipo!!

Namba 10 hizo Bajaj miji mingi India wanaziita "Rikshoo"

Kingine ambacho mgeni atapata tabu ni jinsi ya kupata chakula ambacho hakijatiwa pilipili!! Muhindi hata ukimwambia "usiweke pilipili" lazima ataweka tu coz ya mazowea yao,

Ila wahindi wengi wanatilia sana mkazo masomi,wengi wako bussy kuitafuta elimu,pia ni watu wenye "Akili" sana na ni wepesi wa kuelewa jambo.
 
India ukiingia maduka yao ya mitaani,mengi yamejaa bidhaa zao tu/local product,tena zimeandikwa na bei yake/Price tag toka kiwandani,mfano ukitaka kununu Sabuni inakua imeshaandikwa bei kabisa toka kiwandani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…