Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo. Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake. [h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]
Mariam mwenye umri wa miaka 27 pia ni mjamzito na pia atapata adhabu ya mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Maafisa wakuu wanasema kuwa icha ya Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake. Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo. Uyu mungu wa waislamu????!!