Video ya Boko Haram yaonesha wasichana wa Chibok

Video ya Boko Haram yaonesha wasichana wa Chibok

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Wanachama wa vuguvugu la Bring Back Our Girls waliandamana mjini Lagos Jumatano kutetea kuachiliwa kwa wasichana hao kanda ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram inaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wako hai.



Ni miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok.

BB.jpg


Ni wasichana 15 wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya Krismasi.

Video hiyo imepeperushwa hewani na shirika la utangazaji la marekani la CNN.

Maafisa wa Nigeria wamesema mashauriano kati ya serikali na wapiganaji hao wa Kiislamu yanaendelea lakini yatasalia kuwa siri kwa sababu za kiusalama na ili kuzuia wanaofanikisha wazungumzo hayo wasitambulike.

MMM.jpg

Mamake mmoja wa wasichana waliotekwa

Mwandishi wa BBC aliyeko Abuja anasema video hiyo imewapa matumaini baadhi ya raia wa Nigeria kwa sababu inaonesha baadhi ya wasichana wako hai.

Lakini baadhi wanasema hali kwamba ni wasichana wachache sana waliooneshwa kwenye video hiyo inaibua wasiwasi kuhusu hatima ya wasichana hao wengine walioonekana kwenye video hiyo.



Kanda hiyo ya video ndiyo ya kwanza kutolewa ikiwaonesha wasichana hao tangu mwezi Mei mwaka 2014.


Serikali ya Nigeria imekosolewa kwa kushindwa kuwakomboa wasichana hao.

Shule ya Chibok inapatikana jimbo la Borno
Kwa muda mrefu, kitambulisha mada #BringBackOurGirls (Turejeshee wasichana wetu) kilivuma sana mtandao wa Twitter.

SSS.jpg


Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni mmoja wa watu mashuhuri walioshiriki katika kampeni ya kupigania kukombolewa kwa wasichana hao.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom