New Barrick Group kuinunua Acacia

Kuna watu walifikiri Magufuli akiingia madarakani hakutokuwa na vipindi vigumu vya kupitia.....sasa mambo yanaanza kukaa sawa na Mungu amjalie afya njema na Moyo Wa ujasiri zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo.
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Nyumbu wafuasi wa tundu za risasi hawatakuelewa
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Lisu kwa nini ulitudanganya kwamba tutashitakiwa MIGA ?

Ulikuwa unataka tuogope tuwaache Acacia waendelee kutunyonya?

Kwa hali hiyo Lisu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya watu
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Habari ndiyo hiyo.... badili jina piga kazi, kwani watalaam wetu si wanajua? Mikataba si wanatia saini wao? Mbona makampuni mengi yanabadili majina? Shida ni kwa vikampuni vyetu vya kibongo..
 
Acha hasira ...hatulipwi sasa ...ukitaka ukufe
 
Kwani wanakatazwa?
 
Habari ndiyo hiyo.... badili jina piga kazi, kwani watalaam wetu si wanajua? Mikataba si wanatia saini wao? Mbona makampuni mengi yanabadili majina? Shida ni kwa vikampuni vyetu vya kibongo..
Kumbe
 

Unajua tatizo la elimu ya bongo kwenye masuala ya logic na kuhoji wanafanywa mazezeta kwenye kila kitu na hawa wanasiasa. Hizi kampuni ni listed na taarifa zipo wazi. Lakini bado watu wanalishwa uongo na kushangilia.

Tulipinga hapa data za maprofessa na ripoti zao feki tukaitwa majina kibao na matusi. Kuna vitu ni beyond common sense.

Sasa mwenye nyumba kashtuka kujua zile ripoti ni feki ameanza kubambikia wafanyakazi wa kampuni kesi hazina mbele wala nyuma ili mradi tu kukomoa watu. Hajali hawa kuharibu majina ya watu watanzania wazawa waliobahatika kufanya kazi kwenye multinationals. Anafikiri kwenye multinational MD anaweza kubeba sanduku la pesa na kwenda kuhonga tu na kampuni ipo listed London na New York.

Zile ripoti kwa nini asiende nazo mahakamani? Hapo ndiyo watu wataelewa Lissu alikua sawa kusema zile ni professorial rubbish.

Wale maprofessa wameiabisha nchi na kutufanya watu wote tuonekane wajinga. Kwa macho ya juujuu tunaona poa tu lakini kwenye ulimwengu unaojali akili tumeshusha dhamani yetu sana. Wale wanastahili kuomba radhi au wafungwe.
 
Zile ripoti kwa nini asiende nazo mahakamani? Hapo ndiyo watu wataelewa Lissu alikua sawa kusema zile ni professorial rubbish.
Ukienda mahakamani na taarifa za kupikwa lazima ukalishwe chini na ukishindwa itakubidi ulipe gharama za kesi, sidhani kama tuko katika hali hiyo kwasasa. Kisheria mikataba ni halali kabisa hata kama inasema tulipwe elfu 1000 halafu wao wabebe mabilioni siyo kosa maadam tulikubali wenyewe. Hoja hapa ngumu ambayo watu wengi hawajaitaja ni kwamba ni kwamba tufanye nini ili tuondokane na kadhia hii kama nchi ?

Eti Mkuu chige naomba tutafuta Empirical Solution kwenye hili...........
Tufanye nini ili tuondokane na hii kadhia ambayo nchi yetu imegubikwa nayo ???
 
Yaani wale jamaa walikuwa wetu kabisa kama tusingeweka mihemuko mbele! Kwamba wanaiba, hilo halina mjadala!!

Tulikuwa na uwezo wa kujenga mazingira ya kitakwimu na kisheria ambayo wasingeweza kuchomoka hata kidogo. Endapo tungekuwa systematic, hivi sasa wale jamaa ingekuwa wameshaomba poo tofauti na hali iliyopo ambayo kuna kila dalili ni sisi ndio tutaomba poo ili angalau tupate chochote kitu kutoka kwa kile tunachodai!

Kwa mfano, hadi sasa sijaona logic yoyote ya kwanini kwenye ile tume ya Mruma hapakuwa na mtu wa Acacia at least wa ku-confirm samples zinazochukuliwa. Kama tuna uhakika na takwimu zetu, tungeweza hata kuwaambia wateue mtu wanayemwamini wenyewe ambae angekuwa begwa kwa begwa na uchunguzi wa Tume ya Profesa Mruma katika kutafuta ukweli!

Hapa ilikuwa tukizungumzia suala la tume kuwa inclussive in one way or another, watu walikuwa wanakejeli kwamba huwezi kuwashirikisha wezi matokeo yake ripoti inaonekana ni ya upande mmoja ambayo sidhani kama inaweza kuwa na nguvu za kisheria au angalau uhalali wa kimantiki.

Endapo Acacia wangekuwa included, wasingeweza kuikataa ripoti ambayo na wenyewe walikuwepo! Na kama wangeikataa, wao ndo wangeonekana stupid... unaikataa vipi ripoti ambayo uchunguzi wake umeshiriki?!

Na kwavile ripoti ingekuwa haikatiliki kwa sababu ilikuwa na uhalali wa ushiriki wa pande mbili, basi hata madai ya Trilioni 450 endapo yangetokana na hiyo ripoti, nayo wasingeweza kuyakataa, au tuseme yasingekatalika kwa sababu trilioni 450 imetokana na ripoti ambayo na wenyewe walishirikishwa katika kutafut ukweli!

Hata zile Western media zinazotukejeli kudai pesa ambayo ni bajeti yetu ya zaidi ya miaka 10, nao wangekosa cha kuongea kwa sababu ingeonekana ni Trilion 450 zilizokuwa "verified" na mdaiwa!!

Kama ripoti ile ya Mruma haina hitilafu basi hiyo ingekuwa ni scandal mbaya sana kwa Barrick Gold na wasingeweza kuchomoka lakini kwa sasa kila mwenye akili yake anatupuuza kwa sababu ni ripoti ilioyotengenezwa na upande mmoja
 
Leo hii ukiongea tofauti na wanavyoamini au wanavyotaka wao jamii iamini, basi wewe unaonekana ni msaliti huku wenyewe wakijivika uzalendo fake kwa kudhani uzalendo ni kuunga mkono kila kinachofanywa na serikali hata kama ni cha kijinga au hakina maslahi kwa nchi.

Inakera kuona wale wale wanaodhani ni wazalendo ndio washenzi wakubwa wanaoifanya hii nchi iwe hapa halafu likitokea la kuweza kuonekana hata na kipofu, wanataka tulie wote... wtf! Yaani ujinga wafanye wao huku wengine wakitahadhalisha kabisa kwamba mnachofanya ni ujinga wa kiwango cha SGR lakini linapotokea jambo baya kutokana na ujinga ule ule ambao watu walionya, wanataka sote tusikitike... jinga sana hawa watu!

Na kwa hakika, ripoti ile kama inakuwa argued mahakamani, taifa zima tutaonekana mazwazwa! Na ukweli ni kwamba, hata kama inakuwa argued na mahakama zetu, there's no way tunaweza kushinda unless patokee government inteference.
 

Nakubaliana na wewe kwenye kushindwa pale unapotumia takwimu za kupikwa.

Kwanza, takwimu hizi japokuwa tunaona inatusaidia sisi kusingizia watu wizi inahatarisha uwekezaji kwani investors wengine wakiona maprofessa wasomi, TRA na Serikali zinatumia takwimu za kupikwa basi si sehemu salama kuwekeza. Kwa hiyo hii inaathiri uwekezaji moja kwa moja.

Pili, inaathiri muonekano wetu nje ya nchi na kwenye international organizations kwamba nyie elimu yenu ni mbovu kiasi kwamba maprofessa wanapika data? Tunaonekana hili ni taifa la watu ambao si waaminifu. Uaminifu/Trust ni currency yenye nguvu katika biashara yoyote ile.

Ukweli mwingine ni kwamba mwenye nyumba anataka kupata political points kwenye hili lakini njia aliyotumia haikuwa sawa na bado mpaka sasa si sawa. Hii kwenda kuwakamata wafanyakazi wa hizi kampuni ni kukomoa tu lakini inazidi kutupaka matope kama nchi.

Tatu, kama tunasema hawa watu wanatuibia kwa sababu huko nyuma tuliingia mikataba mibovu, basi wale walioingia hii mikataba mibovu wakamatwe na wajieleze. Ni rahisi kusema mikataba mibovu lakini tunaelewa nchi ilikua katika nafasi gani huko nyuma? Nitakupa mfano katika kujadili mikataba ya kibiashara kama nchi yako haina teknolojia, utaalamu wa skilled workforce n.k. bargaining power ya mfanyabiashara inakuwa kubwa.

Pia, tunasema hawa watu wanatuibia, tunapika ripoti kuonyesha huo wizi sasa hii si hisia zaidi ya uhalisia? Kama tunaibiwa ni kitu gani haswa tunaibiwa? Tuna ripoti inayoonyesha uhalisia wa tunachoibiwa ukiachilia hizi ripoti feki? Kama hamna ni kipi hasa tunaibiwa.

Ni kiasi gani tunataka kupata kama nchi ili tusiwetunaibiwa. Mpaka sasa naona watu wanasema tunaibiwa lakini ni kiasi gani haswa tunaibiwa? Pia tuelewe hii ni biashara ambayo mtu kaweka mtaji wake apate faida.

Mwisho wa siku isijekuwa hatujui tunachotaka kiasi kwamba hata tukipewa kiasi fulani cha pesa bado tunasema hawa watu wanatuibia. Kama hujui unachoibiwa ukienda kwenye majadiliano unajuaje bado huibiwi?
 

Mkuu Chige mimi sitii maneno mingi hapa kwasababu ntaharibu.
Lakini ambacho Raisi wetu anatakiwa ajifunze ni kutofanya mambo for Political Expediency maana ana rekodi hiyo katika utendaji wake. Mimi katika uzoefu wangu mdogo wa kushughulika na kuandaa mikataba mbalimbali sehemu "Clause" ya kupelekana mahakamani au kuanza kuvurugana ni lazima kwanza mkae chini myajenge. Nafikiri wale jamaa wangekubali kwasababu uwekezaji hutegemea sana SIFA NJEMA kwa pande zote mbili.


Pia hata kama ile ripoti ingeandaliwa basi isingetolewa nje kwa haraka vile mpaka mtakapofanya uchunguzi wote wawili kwasababu japo ule mchanga ni wetu lakini kisheria ni mali ya halali ya Barrick/Accacia. Hivyo kama ulivyosema tungewashirikisha katika kufanya uchunguzi lakini nyuma ya pazia tunaendela kuandaa ripoti yetu nyingine: Hili lingesaidia sana katika upatikanaji wa takwimu sahihi ambazo zingetuchafua kama ilivyo leo hii.

Ile kesi ilikuwa wazi kabisa kwasababu kama wangekuwa wanasingiziwa basi wangekuwa washaenda mahakamani muda sana kwa hasara ambayo wameipata mpaka sasa. Ndiyo maana hata bosi anasema suala la kodi linazungumzika kwasababu kweli wamezingua. CCM wakiacha kufanya kila kitu kisiasa basi tungeweza kupata ushindi asubuhi kweupe.......

 
Nimevaa Shati jipya, boxer mpya, Suruali mpya, soksi mpya na viatu vipya. Naelekea saluni kubadili staili ya kunyoa. Hadi perfume nabadili.

Tushangilieni tuu, Huleeeeeeee. Muda utaamua siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…