MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,451
- 69,319
Kwanza, takwimu hizi japokuwa tunaona inatusaidia sisi kusingizia watu wizi inahatarisha uwekezaji kwani investors wengine wakiona maprofessa wasomi, TRA na Serikali zinatumia takwimu za kupikwa basi si sehemu salama kuwekeza. Kwa hiyo hii inaathiri uwekezaji moja kwa moja.
Pili, inaathiri muonekano wetu nje ya nchi na kwenye international organizations kwamba nyie elimu yenu ni mbovu kiasi kwamba maprofessa wanapika data? Tunaonekana hili ni taifa la watu ambao si waaminifu. Uaminifu/Trust ni currency yenye nguvu katika biashara yoyote ile.
Hizi hoja zote mbili ni kitu kimoja kwasababu katika UWEKEZAJI NI JINA ZURI LINA SEHEMU KUBWA SANA. Hivyo Barrick/Accacia kachafuka lakini pia Tanzania imechafuka sana. Kwasababu kuna mwingine kasema juzi hili deni tunalodai ni gharama ya safari ya kwenda mwezini na kurudi.
Ukweli mwingine ni kwamba mwenye nyumba anataka kupata political points kwenye hili lakini njia aliyotumia haikuwa sawa na bado mpaka sasa si sawa. Hii kwenda kuwakamata wafanyakazi wa hizi kampuni ni kukomoa tu lakini inazidi kutupaka matope kama nchi.
Hapa nakubaliana na wewe nusu-nusu. Kweli mzee alikurupuka kutaka sifa za kisiasa lakini ilikuwa ni kwa fiada ya nani hata kama angepata sifa za kisiasa na kufanikiwa ? Jibu ni faida yetu sote. Japo itabidi abadilike na aache tabia za kukurupuka kwasababu ana hiyo rekodi mbovu kuanzia kwenye Samaki hadi Bombardier.
Tatu, kama tunasema hawa watu wanatuibia kwa sababu huko nyuma tuliingia mikataba mibovu, basi wale walioingia hii mikataba mibovu wakamatwe na wajieleze. Ni rahisi kusema mikataba mibovu lakini tunaelewa nchi ilikua katika nafasi gani huko nyuma? Nitakupa mfano katika kujadili mikataba ya kibiashara kama nchi yako haina teknolojia, utaalamu wa skilled workforce n.k. bargaining power ya mfanyabiashara inakuwa kubwa.
Hoja ambayo ninabisha na vijana wengi hapa siyo kuhusu uhalali wa mikataba. Hata kama tunapata asilimua 5% kama tulisaini huo mkataba basi makosa ni yetu sisi na mkataba utaendelea kuwa halali. Hoja ya msingi ni hizi zifuatazo: Je, tuendelee kuibiwa kisa mikataba ni halali ?
Hiyo hoja yako pia ya kutokuwa na skilled workforce, teknolojia, miundombinu n.k nakubaliana nayo. Hata Baba wa Taifa aliliona hili
Pia, tunasema hawa watu wanatuibia, tunapika ripoti kuonyesha huo wizi sasa hii si hisia zaidi ya uhalisia? Kama tunaibiwa ni kitu gani haswa tunaibiwa? Tuna ripoti inayoonyesha uhalisia wa tunachoibiwa ukiachilia hizi ripoti feki? Kama hamna ni kipi hasa tunaibiwa.
Ni kiasi gani tunataka kupata kama nchi ili tusiwetunaibiwa. Mpaka sasa naona watu wanasema tunaibiwa lakini ni kiasi gani haswa tunaibiwa? Pia tuelewe hii ni biashara ambayo mtu kaweka mtaji wake apate faida.
Mwisho wa siku isijekuwa hatujui tunachotaka kiasi kwamba hata tukipewa kiasi fulani cha pesa bado tunasema hawa watu wanatuibia. Kama hujui unachoibiwa ukienda kwenye majadiliano unajuaje bado huibiwi?
Nakubaliana na wewe kwenye kushindwa pale unapotumia takwimu za kupikwa.
Kwanza, takwimu hizi japokuwa tunaona inatusaidia sisi kusingizia watu wizi inahatarisha uwekezaji kwani investors wengine wakiona maprofessa wasomi, TRA na Serikali zinatumia takwimu za kupikwa basi si sehemu salama kuwekeza. Kwa hiyo hii inaathiri uwekezaji moja kwa moja.
Pili, inaathiri muonekano wetu nje ya nchi na kwenye international organizations kwamba nyie elimu yenu ni mbovu kiasi kwamba maprofessa wanapika data? Tunaonekana hili ni taifa la watu ambao si waaminifu. Uaminifu/Trust ni currency yenye nguvu katika biashara yoyote ile.
Ukweli mwingine ni kwamba mwenye nyumba anataka kupata political points kwenye hili lakini njia aliyotumia haikuwa sawa na bado mpaka sasa si sawa. Hii kwenda kuwakamata wafanyakazi wa hizi kampuni ni kukomoa tu lakini inazidi kutupaka matope kama nchi.
Tatu, kama tunasema hawa watu wanatuibia kwa sababu huko nyuma tuliingia mikataba mibovu, basi wale walioingia hii mikataba mibovu wakamatwe na wajieleze. Ni rahisi kusema mikataba mibovu lakini tunaelewa nchi ilikua katika nafasi gani huko nyuma? Nitakupa mfano katika kujadili mikataba ya kibiashara kama nchi yako haina teknolojia, utaalamu wa skilled workforce n.k. bargaining power ya mfanyabiashara inakuwa kubwa.
Pia, tunasema hawa watu wanatuibia, tunapika ripoti kuonyesha huo wizi sasa hii si hisia zaidi ya uhalisia? Kama tunaibiwa ni kitu gani haswa tunaibiwa? Tuna ripoti inayoonyesha uhalisia wa tunachoibiwa ukiachilia hizi ripoti feki? Kama hamna ni kipi hasa tunaibiwa.
Ni kiasi gani tunataka kupata kama nchi ili tusiwetunaibiwa. Mpaka sasa naona watu wanasema tunaibiwa lakini ni kiasi gani haswa tunaibiwa? Pia tuelewe hii ni biashara ambayo mtu kaweka mtaji wake apate faida.
Mwisho wa siku isijekuwa hatujui tunachotaka kiasi kwamba hata tukipewa kiasi fulani cha pesa bado tunasema hawa watu wanatuibia. Kama hujui unachoibiwa ukienda kwenye majadiliano unajuaje bado huibiwi?
Mkuu ngoja nimalizie kazi ya muhimu halafu ntakuja kuchangia!