New Barrick Group kuinunua Acacia

New Barrick Group kuinunua Acacia

Kuna watu walifikiri Magufuli akiingia madarakani hakutokuwa na vipindi vigumu vya kupitia.....sasa mambo yanaanza kukaa sawa na Mungu amjalie afya njema na Moyo Wa ujasiri zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo.
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Nyumbu wafuasi wa tundu za risasi hawatakuelewa

Lisu kwa nini ulitudanganya kwamba tutashitakiwa MIGA ?

Ulikuwa unataka tuogope tuwaache Acacia waendelee kutunyonya?

Kwa hali hiyo Lisu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya watu
Haya ndo yale niliyokuwa nayasema wakati ule! Hata baada ya "merger", New Barrick Group ndo hapo ina thamani ya USD 18.3 Billion.

Kitoto kimoja cha old Barrick tunakidai USD 190 Billion halafu bado kuna mtu anaendelea kuamini ipo siku tutakuja kulipwa! Bado kuna mtu anaamini data za akina Profesa Mruma!!

Technically, endapo Tanzania tutaweza ku-prove tunaibiwa na hivyo kuwa na haki ya kuzi-abuse a known world gold data, kinachoweza kufanyika katika kutenda haki labda Acacia kuwa dissolved kwa sababu audited books za Acacia na Barrick zinaonesha hazina hiyo thamani!

Malcom Lumumba
 
Kwa macho yetu tunaona kama hawa watu hawajuani na wanafanya biashara, lakini ukweli inaonesha wanaichezea nchi yetu kwa kubadili badili majina tu kwa nia ya kutuchuna madini yetu na mambo yakiwafika pabaya wachache kati yao wanarudi kwao kubadili jina na kurudi kama kampuni nyingne kuinunua iliyopo lakni ukweli ni kwamba hawa jamaa wakianza kupitia wakati mgumu wanabadili majina ya kampuni yao na wafanyakazi kubadilishana vituo nchi hadi nchi lakini sisi tunaona kuwa wameuziana ila lengo ni kuua matatizo na changamoto wanazokuwa wanazipitia.

Hapo kabla, ktk miaka ya 1985-90 kampuni hii ilikuwa na jina jingne (nimelisahau kidogo), baadae ndo likaaja barick gold mining, baadae tena likapita na kuja Acacia gold mine,sasa eti inarudi ile ile kwa muondoko mpya wa Barick group.
Daaaaahhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
Hapa shamba litaendelea kuwa la bibi tu hata tukivinba namna gani.
Habari ndiyo hiyo.... badili jina piga kazi, kwani watalaam wetu si wanajua? Mikataba si wanatia saini wao? Mbona makampuni mengi yanabadili majina? Shida ni kwa vikampuni vyetu vya kibongo..
 
Acha hasira ...hatulipwi sasa ...ukitaka ukufe
Unanisaidia kulisha familia mpaka uniambie nifanye kazi?
Akili zenu sijui mmezigawa wapi?Kwani tunahoji juu ya deni la taifa,kwani hizo pesa nitakuja kulipa mimi moja kwa moja?Hapana,ni kodi ninayokatwa ndio itakuja kulipa!Hivyo hata shughuli za maendeleo zikifanyika ni faida kwangu,wengine baadhi ya miradi ikifanyika tunaingiza pesa kupitia tenda tunazopata!!!
So lazima tufuatilie,tunalipwa lini?Au kama hatulipwi tujue!
 
Baada ya Kampuni ya Barrick Gold kuungana na Kampuni ya Randgold Resources na kuwa kampuni inayoitwa New Barrick Group yenye thamani ya US$18.3 bilioni. Kwa sasa kuna taratibu zinazofanyika ili kuzinunua hisa zilizobakia za Acacia ambazo ni asilimia 36 zenye thamani ya US$303 milioni kwa hesabu iliyofanya Jumanne wiki hii.

‘’Baada ya kukamilisha kazi ya kuziunganisha kampuni za Barrick Gold na Randgold Resource, tutakaa na Acacia na Serikali ya Tanzania ili kumaliza tofauti zilizopo’’, Alisema Mark Bristow ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa New Barrick Group.

Acacia ilinukuliwa ikisema kuwa ilikuwa ikisubiri kupewa taarifa rasmi na Barrick kuhusu mazungumzo yake na serikali ya Tanzania.

Serikali ya Tanzania imekataa kukutana na Acacia kutokana na suala la ukwepaji wa kodi.

"Kama ilivyoshauriwa hapo awali, Barrick bado haijaipa Acacia mapendekezo ya ufumbuzi kamili wa migogoro ambayo Barrick ameweza kukubaliana na Serikali ya Tanzania licha ya majadiliano yao ya moja kwa moja yalifanywa mnamo Oktoba 2017," ilisema Acacia.

Katika mahojiano na Globe and Mail mnamo Septemba John Thornton, mwenyekiti mtendaji wa Barrick Gold, alisema Acacia "hakuwahi kulipia kodi ya mapato" kwa serikali ya Tanzania na njia bora ya kukabiliana na tatizo hili ilikuwa kupitia majadiliano na serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Randgold Resources ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa New Barrick Group, Mark Bristow aliliambia gazeti la Miningmx mnamo Oktoba 1 kwamba alikuwa na nia ya kuwekeza Tanzania. Alisema, "Je, sisi, kama Randgold, tunaenda Tanzania? Kabisa. Je! Tumefanya kazi na serikali ya Tanzania kama Randgold? Ndio, tumefanya "alisema.

Habari kwa lugha ya Kiingereza:

SOURCE: Bloomberg and Financial Times newspaper.
Kwani wanakatazwa?
 
Habari ndiyo hiyo.... badili jina piga kazi, kwani watalaam wetu si wanajua? Mikataba si wanatia saini wao? Mbona makampuni mengi yanabadili majina? Shida ni kwa vikampuni vyetu vya kibongo..
Kumbe
 
Nimecheka kama nilikuwepo!!

Mkuu Malcom, endapo serikali na timu yake wangekuwa makini na kuweka pembeni mihemuko, hili la mkanganyiko wala lisingetokea na kama lingetokea basi ungekuwa ni mkanganyiko unaokubalika hata kisayansi kwa sababu margin error ingekuwa within or not VERY VERY far from acceptable limit!

Unapoleta findings ambazo error ni above 100% hicho ni kiroja unless kama umejiandaa vya kutosha ku-defend hizo findings ambazo zina-underestimate all past findings duniani!

A moment Profesa Mruma alipotoa ile ripoti ya kwanza, nikazichakata data zake kisha nikaingia kwenye WORLD KNOWN DATA!

Hapo nimeandika kwa msisitizo kwa sababu nilijua no matter what, kuwa na logical demand ni lazima demand hiyo iendane na takwimu zinazofahamika duniani kinyume chake, tutatakiwa ku-prove otherwise!

Ilinichukua less than 30 minutes tangu wakati Mruma asome ile ripoti kugundua kwamba, kama ripoti yake ni sahihi basi maana yake Tanzania itakuwa among top 3 world gold producers wakati takwimu za dunia zinaonesha hatupo hata among top 10 !!!

Inawezekana ni kweli tupo among top 3 against world known statistics lakini hizo ni new findings known nowhere else except kwenye makarabrasha yetu au ya wale "wanaopika takwimu za uzalishaji dhahabu duniani"

Mbaya zaidi, wakati ripoti ile ingemaanisha world gold production statistics hazipo sahihi, ripoti yenyewe tulikuwa tumeiandaa wenyewe bila kushirkisha upande wa pili! Kwamba, tunatarajia ku-argue against official world gold statistics kwa kutumia data tulizotengeneza wenyewe not from new geological findings but from makontena ya makinikia!

Kuja ripoti ya Profesa Mrosso na USD 190 Billion, nikakuta hata Market Cap ya Barick Gold yenye kampuni 7 ndani yake including Acacia, haifiki hata $40 Billion (at least kwa wakati ule). Ukija kwenye annual revenue ya Barrick Gold yenye kampuni 7 ndani yake ilikuwa haifiki hata $10 na net income haifiki hata $ 5 Billion.

Kinyume chake, ilikuwa ukitafsiri ripoti ya Profesa Mrosso, unakuta Acacia peke yake walikuwa wanatuibia annual tax ya about USD 4 Billion... hiyo ni kodi tu!! Kama kodi ingekuwa ni 40% ya mapato, ina maana mapato ya Accacia peke yake ni USD 10 Billion!

Kwamba, mapato ya Acacia peke yake yanazidi mapato yote ya Barrick Gold ambayo ndani yake kuna hiyo Acacia!

Argument yetu ilikuwa simple and clear kwamba, "hizo takwimu za akina Barrick ni za uongo kwa sababu ni wezi!" Na inawezekana kabisa kwamba ni za uongo lakini tulisahau kwamba, kisheria hizo hizo takwimu za uongo ndizo zitakazotumika kwa sababu ndizo official financial statisticts zinazotumika hata kwenye masoko makubwa duniani kama New York and London Stock Exchange including NASDAQ!

Tahadhali yangu hapa ilikuwa, tusipojua tunadai nini basi itakuwa ngumu sana ku-defend madai yetu. Na haya yalitokea kwa sababu zoezi zima lilitawaliwa na mihemuko ya kisiasa!

Unajua tatizo la elimu ya bongo kwenye masuala ya logic na kuhoji wanafanywa mazezeta kwenye kila kitu na hawa wanasiasa. Hizi kampuni ni listed na taarifa zipo wazi. Lakini bado watu wanalishwa uongo na kushangilia.

Tulipinga hapa data za maprofessa na ripoti zao feki tukaitwa majina kibao na matusi. Kuna vitu ni beyond common sense.

Sasa mwenye nyumba kashtuka kujua zile ripoti ni feki ameanza kubambikia wafanyakazi wa kampuni kesi hazina mbele wala nyuma ili mradi tu kukomoa watu. Hajali hawa kuharibu majina ya watu watanzania wazawa waliobahatika kufanya kazi kwenye multinationals. Anafikiri kwenye multinational MD anaweza kubeba sanduku la pesa na kwenda kuhonga tu na kampuni ipo listed London na New York.

Zile ripoti kwa nini asiende nazo mahakamani? Hapo ndiyo watu wataelewa Lissu alikua sawa kusema zile ni professorial rubbish.

Wale maprofessa wameiabisha nchi na kutufanya watu wote tuonekane wajinga. Kwa macho ya juujuu tunaona poa tu lakini kwenye ulimwengu unaojali akili tumeshusha dhamani yetu sana. Wale wanastahili kuomba radhi au wafungwe.
 
Zile ripoti kwa nini asiende nazo mahakamani? Hapo ndiyo watu wataelewa Lissu alikua sawa kusema zile ni professorial rubbish.
Ukienda mahakamani na taarifa za kupikwa lazima ukalishwe chini na ukishindwa itakubidi ulipe gharama za kesi, sidhani kama tuko katika hali hiyo kwasasa. Kisheria mikataba ni halali kabisa hata kama inasema tulipwe elfu 1000 halafu wao wabebe mabilioni siyo kosa maadam tulikubali wenyewe. Hoja hapa ngumu ambayo watu wengi hawajaitaja ni kwamba ni kwamba tufanye nini ili tuondokane na kadhia hii kama nchi ?

Eti Mkuu chige naomba tutafuta Empirical Solution kwenye hili...........
Tufanye nini ili tuondokane na hii kadhia ambayo nchi yetu imegubikwa nayo ???
 
Mkuu Chige umesema ukweli kabisa tatizo la serikali ni kwenda mbele halafu kurudi nyuma kitakwimu na kurekebisha ile idadi ya mwanzoni. Japo sasa uthibitisho wa wizi kisheria ulikuwepo, kwasababu kuendesha biashara kubwa kama ile bila usajili ni ukwepaji mkubwa sana wa kodi.
Lakini pia kutumia mwanya kuchukua madini mengine ambayo hayakuanishwa kwenye mikataba hili nalo ni tatizo kubwa.

Yote tisa, siku nyingine mzee aende taratibu, ili kuzuia mkanganyiko wa namna hii. Pia wanasiasa wasitunishiane misuli kwasababu tunahitaji sana umoja wa kitaifa kwenye mambo kama haya. Leo hii watu wengi wanashindwa kukubali ukweli kama Barrick wametupiga kwasababu ni CHADEMA tu au hata wengine wanaunga mkono kila kinachosemwa na serikali bila kuchambua vizuri kwasababu tu wako CCM.

Tufike mahali tubadilike ili twende mbele.
Yaani wale jamaa walikuwa wetu kabisa kama tusingeweka mihemuko mbele! Kwamba wanaiba, hilo halina mjadala!!

Tulikuwa na uwezo wa kujenga mazingira ya kitakwimu na kisheria ambayo wasingeweza kuchomoka hata kidogo. Endapo tungekuwa systematic, hivi sasa wale jamaa ingekuwa wameshaomba poo tofauti na hali iliyopo ambayo kuna kila dalili ni sisi ndio tutaomba poo ili angalau tupate chochote kitu kutoka kwa kile tunachodai!

Kwa mfano, hadi sasa sijaona logic yoyote ya kwanini kwenye ile tume ya Mruma hapakuwa na mtu wa Acacia at least wa ku-confirm samples zinazochukuliwa. Kama tuna uhakika na takwimu zetu, tungeweza hata kuwaambia wateue mtu wanayemwamini wenyewe ambae angekuwa begwa kwa begwa na uchunguzi wa Tume ya Profesa Mruma katika kutafuta ukweli!

Hapa ilikuwa tukizungumzia suala la tume kuwa inclussive in one way or another, watu walikuwa wanakejeli kwamba huwezi kuwashirikisha wezi matokeo yake ripoti inaonekana ni ya upande mmoja ambayo sidhani kama inaweza kuwa na nguvu za kisheria au angalau uhalali wa kimantiki.

Endapo Acacia wangekuwa included, wasingeweza kuikataa ripoti ambayo na wenyewe walikuwepo! Na kama wangeikataa, wao ndo wangeonekana stupid... unaikataa vipi ripoti ambayo uchunguzi wake umeshiriki?!

Na kwavile ripoti ingekuwa haikatiliki kwa sababu ilikuwa na uhalali wa ushiriki wa pande mbili, basi hata madai ya Trilioni 450 endapo yangetokana na hiyo ripoti, nayo wasingeweza kuyakataa, au tuseme yasingekatalika kwa sababu trilioni 450 imetokana na ripoti ambayo na wenyewe walishirikishwa katika kutafut ukweli!

Hata zile Western media zinazotukejeli kudai pesa ambayo ni bajeti yetu ya zaidi ya miaka 10, nao wangekosa cha kuongea kwa sababu ingeonekana ni Trilion 450 zilizokuwa "verified" na mdaiwa!!

Kama ripoti ile ya Mruma haina hitilafu basi hiyo ingekuwa ni scandal mbaya sana kwa Barrick Gold na wasingeweza kuchomoka lakini kwa sasa kila mwenye akili yake anatupuuza kwa sababu ni ripoti ilioyotengenezwa na upande mmoja
 
Unajua tatizo la elimu ya bongo kwenye masuala ya logic na kuhoji wanafanywa mazezeta kwenye kila kitu na hawa wanasiasa. Hizi kampuni ni listed na taarifa zipo wazi. Lakini bado watu wanalishwa uongo na kushangilia.

Tulipinga hapa data za maprofessa na ripoti zao feki tukaitwa majina kibao na matusi. Kuna vitu ni beyond common sense.

Sasa mwenye nyumba kashtuka kujua zile ripoti ni feki ameanza kubambikia wafanyakazi wa kampuni kesi hazina mbele wala nyuma ili mradi tu kukomoa watu. Hajali hawa kuharibu majina ya watu watanzania wazawa waliobahatika kufanya kazi kwenye multinationals. Anafikiri kwenye multinational MD anaweza kubeba sanduku la pesa na kwenda kuhonga tu na kampuni ipo listed London na New York.

Zile ripoti kwa nini asiende nazo mahakamani? Hapo ndiyo watu wataelewa Lissu alikua sawa kusema zile ni professorial rubbish.

Wale maprofessa wameiabisha nchi na kutufanya watu wote tuonekane wajinga. Kwa macho ya juujuu tunaona poa tu lakini kwenye ulimwengu unaojali akili tumeshusha dhamani yetu sana. Wale wanastahili kuomba radhi au wafungwe.
Leo hii ukiongea tofauti na wanavyoamini au wanavyotaka wao jamii iamini, basi wewe unaonekana ni msaliti huku wenyewe wakijivika uzalendo fake kwa kudhani uzalendo ni kuunga mkono kila kinachofanywa na serikali hata kama ni cha kijinga au hakina maslahi kwa nchi.

Inakera kuona wale wale wanaodhani ni wazalendo ndio washenzi wakubwa wanaoifanya hii nchi iwe hapa halafu likitokea la kuweza kuonekana hata na kipofu, wanataka tulie wote... wtf! Yaani ujinga wafanye wao huku wengine wakitahadhalisha kabisa kwamba mnachofanya ni ujinga wa kiwango cha SGR lakini linapotokea jambo baya kutokana na ujinga ule ule ambao watu walionya, wanataka sote tusikitike... jinga sana hawa watu!

Na kwa hakika, ripoti ile kama inakuwa argued mahakamani, taifa zima tutaonekana mazwazwa! Na ukweli ni kwamba, hata kama inakuwa argued na mahakama zetu, there's no way tunaweza kushinda unless patokee government inteference.
 
Ukienda mahakamani na taarifa za kupikwa lazima ukalishwe chini na ukishindwa itakubidi ulipe gharama za kesi, sidhani kama tuko katika hali hiyo kwasasa. Kisheria mikataba ni halali kabisa hata kama inasema tulipwe elfu 1000 halafu wao wabebe mabilioni siyo kosa maadam tulikubali wenyewe. Hoja hapa ngumu ambayo watu wengi hawajaitaja ni kwamba ni kwamba tufanye nini ili tuondokane na kadhia hii kama nchi ??

Nakubaliana na wewe kwenye kushindwa pale unapotumia takwimu za kupikwa.

Kwanza, takwimu hizi japokuwa tunaona inatusaidia sisi kusingizia watu wizi inahatarisha uwekezaji kwani investors wengine wakiona maprofessa wasomi, TRA na Serikali zinatumia takwimu za kupikwa basi si sehemu salama kuwekeza. Kwa hiyo hii inaathiri uwekezaji moja kwa moja.

Pili, inaathiri muonekano wetu nje ya nchi na kwenye international organizations kwamba nyie elimu yenu ni mbovu kiasi kwamba maprofessa wanapika data? Tunaonekana hili ni taifa la watu ambao si waaminifu. Uaminifu/Trust ni currency yenye nguvu katika biashara yoyote ile.

Ukweli mwingine ni kwamba mwenye nyumba anataka kupata political points kwenye hili lakini njia aliyotumia haikuwa sawa na bado mpaka sasa si sawa. Hii kwenda kuwakamata wafanyakazi wa hizi kampuni ni kukomoa tu lakini inazidi kutupaka matope kama nchi.

Tatu, kama tunasema hawa watu wanatuibia kwa sababu huko nyuma tuliingia mikataba mibovu, basi wale walioingia hii mikataba mibovu wakamatwe na wajieleze. Ni rahisi kusema mikataba mibovu lakini tunaelewa nchi ilikua katika nafasi gani huko nyuma? Nitakupa mfano katika kujadili mikataba ya kibiashara kama nchi yako haina teknolojia, utaalamu wa skilled workforce n.k. bargaining power ya mfanyabiashara inakuwa kubwa.

Pia, tunasema hawa watu wanatuibia, tunapika ripoti kuonyesha huo wizi sasa hii si hisia zaidi ya uhalisia? Kama tunaibiwa ni kitu gani haswa tunaibiwa? Tuna ripoti inayoonyesha uhalisia wa tunachoibiwa ukiachilia hizi ripoti feki? Kama hamna ni kipi hasa tunaibiwa.

Ni kiasi gani tunataka kupata kama nchi ili tusiwetunaibiwa. Mpaka sasa naona watu wanasema tunaibiwa lakini ni kiasi gani haswa tunaibiwa? Pia tuelewe hii ni biashara ambayo mtu kaweka mtaji wake apate faida.

Mwisho wa siku isijekuwa hatujui tunachotaka kiasi kwamba hata tukipewa kiasi fulani cha pesa bado tunasema hawa watu wanatuibia. Kama hujui unachoibiwa ukienda kwenye majadiliano unajuaje bado huibiwi?
 
Yaani wale jamaa walikuwa wetu kabisa kama tusingeweka mihemuko mbele! Kwamba wanaiba, hilo halina mjadala!!

Tulikuwa na uwezo wa kujenga mazingira ya kitakwimu na kisheria ambayo wasingeweza kuchomoka hata kidogo. Endapo tungekuwa systematic, hivi sasa wale jamaa ingekuwa wameshaomba poo tofauti na hali iliyopo ambayo kuna kila dalili ni sisi ndio tutaomba poo ili angalau tupate chochote kitu kutoka kwa kile tunachodai!

Kwa mfano, hadi sasa sijaona logic yoyote ya kwanini kwenye ile tume ya Mruma hapakuwa na mtu wa Acacia at least wa ku-confirm samples zinazochukuliwa. Kama tuna uhakika na takwimu zetu, tungeweza hata kuwaambia wateue mtu wanayemwamini wenyewe ambae angekuwa begwa kwa begwa na uchunguzi wa Tume ya Profesa Mruma katika kutafuta ukweli!

Mkuu Chige mimi sitii maneno mingi hapa kwasababu ntaharibu.
Lakini ambacho Raisi wetu anatakiwa ajifunze ni kutofanya mambo for Political Expediency maana ana rekodi hiyo katika utendaji wake. Mimi katika uzoefu wangu mdogo wa kushughulika na kuandaa mikataba mbalimbali sehemu "Clause" ya kupelekana mahakamani au kuanza kuvurugana ni lazima kwanza mkae chini myajenge. Nafikiri wale jamaa wangekubali kwasababu uwekezaji hutegemea sana SIFA NJEMA kwa pande zote mbili.

Pia hata kama ile ripoti ingeandaliwa basi isingetolewa nje kwa haraka vile mpaka mtakapofanya uchunguzi wote wawili kwasababu japo ule mchanga ni wetu lakini kisheria ni mali ya halali ya Barrick/Accacia. Hivyo kama ulivyosema tungewashirikisha katika kufanya uchunguzi lakini nyuma ya pazia tunaendela kuandaa ripoti yetu nyingine: Hili lingesaidia sana katika upatikanaji wa takwimu sahihi ambazo zingetuchafua kama ilivyo leo hii.

Ile kesi ilikuwa wazi kabisa kwasababu kama wangekuwa wanasingiziwa basi wangekuwa washaenda mahakamani muda sana kwa hasara ambayo wameipata mpaka sasa. Ndiyo maana hata bosi anasema suala la kodi linazungumzika kwasababu kweli wamezingua. CCM wakiacha kufanya kila kitu kisiasa basi tungeweza kupata ushindi asubuhi kweupe.......

Nimevaa Shati jipya, boxer mpya, Suruali mpya, soksi mpya na viatu vipya. Naelekea saluni kubadili staili ya kunyoa. Hadi perfume nabadili.

Tushangilieni tuu, Huleeeeeeee. Muda utaamua siku moja.
 
Back
Top Bottom