New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

TUMWOMBEE RAIS MWENYEZI MUNGU AMPE BUSARA YA KUWAAMINI WATANZANIA NDIYO MUAROBAINI WA CHANGAMOTO ZETU.



Wakati sasa umefika wa kufutilia mbali Azimio la bunge turudi njia kuu na tutoke kwenye huu mchepuko wa kujidhalilisha wenyewe wakati kila kitu tunaweza kuwashinda wawekezaji wote waliopo duniani


Kama hamniamini nipeni nchi mwone kama hawa hawa watanzania sitawajengea mazingira madhubuti ya uwajibikaji na kuwapa malengo na anayeshindwa anachukuliwa hatua.


Tunachokosa ni uwajibikaji pale watu wanaharibu kazi.


Sasa mapungufu ya kiuwajibikaji haimaanishi tumeshindwa bali wachache wetu wameboronga fursa tulizowapa wakazitumia vibaya. Na hawakuwajibishwa hilo ndilo tatizo letu hatuna tatizo jingine.

Mama alikuwa analiendesha basi vizuri tu hadi mzee wa Msoga na genge lake wakamharibia rekodi yake nzuri ya uchapaji kazi.

Tunalaumu kwa kuwafungulia mlango sasa hii migawanyiko ya kimasilahi, dini, ukanda n.k inadai kafara moja tu kurejesha amani yetu.

Kutengua Azimio la bunge na kupitia upya mpango wa miaka 5 ya uendelezaji wa bandari zetu ikifika mahali tukiona tunahitaji wataalamu kutoka nje na mitambo tuchukue hatua na kuboresha.

Itapendeza kuona watanzania tukijiendeshea mambo yetu wenyewe kama malengo ya kujitawala yalivyokuwa

Mungu Ibariki Tanzanian Mungu mbariki Rais wetu aone busara ya kutembea na wengi hata kama ni mwendo wa konokono


Ukitaka mwendo wa kasi nenda pekee yako halafu uone umbali utakaoenda.
PSX_20230701_222811.jpg
 
WALIOSHINDWA KAZI NI WANASIASA SIYO RAIA!



Hii hutokea mwanadamu anapothamini kazi za mikono ya wanadamu na kudharau kazi za mikono ya Mwenyezi Mungu.

Kazi za mikono ya wanadamu kama ufanisi, mapato n.k ni za muda tu lakini kazi za mikono ya Mwenyezi Mungu kama bandari ni za milele.

Bandari ni kazi ya mikono ya Mwenyezi Mungu na itadumu milele wakati mwarabu chochote atakachotufanyia ni kazi ya mikono ya mwanadamu na inapita tu.

Tunazikana kazi za milele za Mwenyezi Mungu na kuthamini kazi za mikono ya wanadamu ambazo ni za muda tu kwa sababu tumemkataa Mwenyezi Mungu.

Ukiona mkataba una vipengele huwezi kuuvunja kwenye mazingira yoyote ujue fika mshiriki wako wa mkataba lengo lake ni kukudhulumu.

Tumeacha mbachao kwa msala upitao. Tekinolojia inabadilika kila siku kwa hiyo kuhalalisha kuwaamini wageni kwa kigezo hicho ni kujisaliti. Ni vigumu kujiamini kama kila siku unajikumbusha HUWEZI.
IMG-20230702-WA0001.jpg
 
MWINYI MZANZIBARA ALIWAUZIA WAARABU WA DUBAI KILOMITA 4, 000 ZA MRABA (kilometa za mraba elfu nne) ZA LOLIONDO NA HAWAJAWAHI KUCHANGIA UCHUMI WA NCHI HII SASA WAZANZIBARA WA TATU WAMEUZA NCHI YOTE KWA WAARABU HAO HAO WA DUBAI KUNA NINI????????!!!!!!!



Wanasema Mkapa alibinafsisha ni kweli lakini hakuuza nchi. Maeneo yote aliyoyabinafsisha bado yalikuwa yakiwajibika chini ya katiba ya JMT lakini huu mkataba wa Dubai Ports World hauwajibiki kwenye katiba ya JMT! Ndiyo maana tunasema nchi imeuzwa kwa sababu maeneo yatakayohusika na mradi hayatawajibika na katiba ya JMT. Maeneo tajwa yatakuwa ni nchi inayojitegemea ndani ya JMT! Hata upatikanaji wa wawekezaji hawa katiba ya JMT ilikiukwa kwa sababu hakuna ushindani katika mchakato wa upatikanaji wa Kampuni ya Dubai Ports World na hivyo kuleta ubaguzi na upendeleo. Pia, sheria za manunuzi, ardhi, mazingira, kodi na ushirikishwaji wa wananchi kujiamulia mambo yetu wenyewe zilikiukwa na hili azimio la bunge.


Wazanzibara wana historia ya kuuza bara lakini kwao hawauzi. Wanatuuza hawa Wazanzibara kwa sababu hawana uzalendo na Tanganyika.


Sasa hizi siyo hoja za kuugawa Muungano lakini ni hoja za kubaini mapungufu ya Muungano.

Haiwezekani Wazanzibara wakawa ni nchi lakini bado wanaweza kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sasa hivi tuna marais wawili na hakuna hata mmoja anatoka Tanganyika na hili ni pungufu kubwa la kimuungano.


Haiwezekani Tanganyika iwe nchi huru huku inatawaliwa na Wazanzibara. Kama kweli sisi ni nchi moja mbona wao kwenye katiba yao wanajitambua kama nchi na hawatupi watanganyika nafasi ya kuwatawala lakini sisi tunawapa kila mwanya wakutukamatia chini. Huu ni mushkeli. Wengi wape au watajinyakulia wenyewe ndiyo ukweli.


Wao hawako tayari sisi kuwatawala na kamwe Rais wao hajawahi kumteua mtanganyika kuwa waziri, mkuu wa mkoa au wa wilaya kwenye serikali yao lakini sisi wanatupora ajira kwenye maeneo yasiyo ya Muungano.


Haiingii akilini kisiasa hata kama kisheria inawezekana Rais, waziri na katibu mkuu wote Wazanzibara waingie mkataba wa kuuza Tanganyika bila kupata kibali cha watanganyika! Na hata watanganyika wengi wao wakiridhia bado watakuwa wanakiuka katiba ya nchi hii inayokataza kuuza eneo lolote la nchi hii. Tunajua nchi imeuzwa pale mwekezaji kaondolewa kuwajibika kwenye katiba ya nchi hii na sheria za nchi hii na kulifanya eneo analolimiki kutokuwa sehemu ya JMT!


Sura ya wizara nyeti kama ya Miundombinu na uchukuzi ilipaswa iwe na sura ya Muungano lakini inapokuwa maeneo nyeti haya Tanganyika na visiwani yanasimamiwa na Wazanzibara tu inabidi tuone hii sasa ni kero ya Muungano.


Kutatua kero za Muungano inabidi tukiri kwenye katiba ya JMT Zanzibar ni nchi na itakuwa na serikali yake na serikali ya JMT itaongozwa na Mtanganyika ili watanganyika wasije kukosa nchi wanayoiongoza maana Wazanzibara tayari wana nchi yao.


Hata UK tulikodabua huu muundo wa Muungano hakuna nafasi ya waxiri mkuu ambaye ni mkuu wa serikali anatoka Scotland, Northern Ireland, Ireland au Wales lazima atoke England.


Pia sisi tulipaswa kuliona hilo kuwa watanganyika hivi sasa wamekuwa wakiwa na wasaka tonge kupigia debe kupoteza uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe.


Hivi sasa watanganyika tumekuwa ni koloni la Zanzibar jambo ambalo waasisi wa Muungano hawakuliona kwa sababu Nyerere alikuwa Mtanganyika na sasa hayupo.



Moja ya sababu kuu ya kulitengua Azimio la bunge ni watanganyika hawakushirikishwa kabla ya Wazanzibara hawajitia sahihi kuuza Tanganyika kwa waarabu na katiba ilikiuka katika mchakato mzima wa kumpata mwekezaji wa kampuni binafsi ya DUBAI PORTS WORLD.

Hizi ni hoja za kisheria na pia ni hoja nzito ya kisiasa na zikipuuzwa mjue kuna siku nchi itaparanganyika.


Waarabu tunawakumbuka kwa kututeka na kutuuza utumwani sasa Wazanzibara waliwafukuzwa kwao wakidai hawawafai lakini inashangaza wanawaamini kusimamia njia kuu za uchumi za watanganyika!


KWANINI TUNASEMA NCHI IMEUZWA.

Kuuzwa nchi siyo lazima yawepo malipo ya wazi ya kuuzwa yanaweza kuwa yamejificha kama kuhongwa na hela kuwekwa nje ya nchi.

Huko ni kuhamisha utajiri wa nchi kwa manufaa ya wachache.


Nchi iliyouzwa in sifa zifuatazo:-


1) Katiba ya hiyo nchi na sheria zake zinatenguliwa hivyo hazitasimamia zoezi la uuzwaji au uendeshaji na usimamizi wake pamoja hilo eneo lipo ndani ya mipaka ya hiyo nchi.

2) Vyombo vya dola ikiwemo mahakama hazina sauti juu ya shughuli zinazoendelea kwenye eneo hilo.

3) Mazingira ya kuuvunja mkataba ni magumu sana na hayana vigezo vilivyo wazi.

4) Hakuna mchango unaoweza kuhakikika wanunuzi wa hilo eneo watautoa kwenye pato la taifa.

5) Hata kama kuna vipengele vya kufuta mkataba bado hutenguliwa kwa kurefushwa kwa mkataba tena kwa muda mrefu. Hata pale mkataba umevunjwa bado mwekezaji huwezeshwa kuendelea ma eneo husika.

6) Wanasiasa na watendaji serikalini huwa wepesi kuutetea kwa vigezo vya ufanisi, tija, mapato lakini hawako tayari kutoa takwimu za kila mwaka za hiyo michango bali hukimbilia kujificha kwenye kichaka cha muda mrefu kama miaka 10 bila kuelezea mchango wa mfumuko wa bei katika kukuza mapato ambayo yameshuka.

Ukiangalia hivyo vigezo 6 tu utaona Mwinyi aliuza kilometa 4, 000 za mraba kwa waarabu wa Loliondo na hakuna lolote la maana nchi hii imepata lakini wasaliti wetu akina Kinana na wenzie ndiye hali zao zimeboreshwa.

Tungelitgemea angalau Kinana asingepewa nafasi yoyote ya utumishi wa umma la kusikitisha sana watu wenye hulka ya kuuza nchi kwa wageni na kufukarisha watu wetu kwa kuwapora maeneo yao ya lishe, vyanzo vya maji na shughuli za makaazi, mila n.k ndiye Mheshimiwa Rais anaona ni jembe la kutegemewa ndani ya CCM hata kumteua kuwa makamu Mwenyekitiwa CCM taifa ma mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM!!!!!! Haya ni mazingira ya kuwawezesha wezi na wabadhirifu wauze nchi yote na kuwa kichocheo cha machafuko ndani ya nchi. Penye dhuluma kamwe hapawezi kuwa na amani.

Something is very wrong with this Madam President na ndiyo maana kwa kuwakumbatia wezi wa mali ya umma kajijengea mazingira ya kuingizwa mkenge na sasa hachahuliki kabisa.
 
TBC1 JANA WAMEKWEPA KWA MAKUSUDI KUTAMKA BOTSWANA ITANUFUIKA ASILIMIA 50% ZA MAPATO YA MIGODI YAO.


Katika hali ya kushangaza jana TBC1 walipata kigugumizi kutaja BOTSWANA kwenye mikataba ya migodi nchini kwao wakaishia kusema watanufaika sana.


Hii inathibitisha wanajua mikataba ya migodi ya nchi hii ni ya kifisadi na hailinufaishi taifa bali inawanufaisha viongozi wachache ndani ya CCM.


Kutuficha habari nyeti kama hii, TBC1 inajivua jukumu lake la kuelimisha jamii mambo nyeti kama ya ulinganishi wa nchi nyingine zimefanikiwa kwenye migodi na sisi hatujafanikiwa kwa malengo ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza.
 
TBC1 JANA HAWAKUGUSA HABARI ZA KATIBU MKUU WA CHADEMA KWENYE MKUTANO WAKE (MANZESE) WA KUELIMISHA JAMII JUU YA KUUZWA KWA NCHI.


Ni aibu kwa chombo cha kitaifa kuwa kimya kwenye mikutano ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa kama CHADEMA kwenye mkutano wao wa jana, Manzese, ambapo walifanya kazi kubwa kuielimisha jamii juu ya tuhuma za nchi imeuzwa kwa waarabu wa Dubai.


Swali la kujiuliza kama kuuza nchi kuna manufaa kwanini wanaopinga hawapewi nafasi kwenye vyombo vya umma nao kutoa maoni yao.


Imefika mahali tukakiri TBC1 inahitaji kiongozi mpya ambaye ataweka masilahi ya nchi mbele badala ya huyu aliyepo ambaye anaweka masilahi ya wezi na wabadhirifu wa mali ya umma mbele.

Huyu mkurugenzi wa TBC1 kwa kutotii maagizo ya serikali aliyoyatoa Rais Magufuli ya kuwatendea haki wa Tanzania kwa kufanya kazi bila upendeleo ni dhahiri tunamtia hatiani kwa utovu wa nidhamu na huu ni wakati mwafaka atimuliwe.


Kama hoja za kuiuza nchi zina mashiko mbona hamuwapi wenye mtazamo tofauti nao wakasikika?

Penye ukweli uongo hujitenga.
 
KWANINI MADAM PRESIDENT KAMWONGEZEA MUDA JAJI MKUU KINYUME NA KATIBA?


Ukomo wa kikatiba wa utumishi wa majaji wa mahakama ya Rufaa ni miaka 65. Mheshimiwa Rais kavunja katiba pale alipomwongezea muda Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuongoza mahakama zetu hata baada ya kuvuka umri wa kustaafu.

Swali la kujiuliza ni kwanini?


Uzoefu tulionao Jaji Mkuu ana nafasi pana ya kubinya haki za wananchi na ndiyo maana anaweza kuteuliwa au kulindwa kwa udi ma uvumbi kwa minajili hiyo.

Mheshimiwa Augustine (kama alivyokuwa Jaji Mkuu)alikiuka kanuni za mahakama ya Rufaa na kuwapora jopo la majaji 3 wa mahakama hiyo kulisikiliza shauri la mgombea binafsi na akaunda jopo la majaji 7 aliloliongoza kutengua uamuzi wa mahakama kuu ulioturudishia haki ya kikatiba ya mgombea huru. Kwa ukiukwaji huu Mheshimiwa Augustine aliwapora wadaawa haki ya marejeo (Review) kama kanuni za mahakama hiyo zinavyoruhusu. Mbaya zaidi, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliutengua uamuzi wa majaji 7 wa mahakama ya rufaa pale iliposema uamuzi wao ulikuka sheria za kimataifa juu ya haki za kidemokrasia. Uamuzi huu hadi leo serikali ya CCM imeghairi kuutekeleza kwa kufuta ibara zote kwenye katiba zinazofuta haki ya mgombea binafsi.


Tuna kila sababu ya kuona Mheshimiwa Rais kakiuka katiba na kumwongezea muda Jaji Mkuu ili amsaidie kutupilia mbali haki ya kutengua Azimio la bunge ambalo limekiuka katiba.


Tunaamini Mheshimiwa Rais kavunja katiba ili jopo ambalo litateuliwa na Jaji Mkuu litasheheni majaji ambao huwa wanajulikana kwa kutoa maamuzi ya kuipendelea serikali na hata kesi haijatinga mahakama ya rufani tayari tuna orodha ya majaji ambao huenda wataisikiliza hiyo kesi ya rufani utakapowafikia.


Bila ya kuwataja majina ya hawa waheshimiwa tuna uhakika walioamua kesi zifuatazo wanaweza kupewa nafasi ya kuisikiliza rufani ya kupinga azimio la bunge:-

a) Waheshimiwa (katika hatua ya rufani na marejeo (Review) walioamua rufani ya kupinga sheria ya mafao na kusema mafao siyo mishahara na hivyo hailindwi na katiba!


b) Waheshimiwa (katika hatua ya rufani na marejeo (Review) walioamua rufani ya kupinga wakurugenzi wa manispaaa kusimamia chaguzi kinyume na katiba na uamuzi wa rufani ukaamua hakuna makosa wakisimamia ni dhahiri watakuwa kwenye jopo la kuilinda serikali ituuze mchana kweupe!


Mheshimiwa Rais kaiuka katiba ili Mheshimiwa Jaji Mkuu atumike kutupilia mbali rufani utakayofika mahakamani hapo siku za usoni yenye kuhoji ukiukwaji wa katiba katika mchakato wa kumpata mwekezaji ambaye ni kampuni binafsi ya Dubai kuwa ulikuwa wa kibaguzi na upendeleo, wananchi hawakushirikishwa na katiba yetu na sheria zake zimetenguliwa na kufanya zoezi zima ni kuunda mchi mpya ndani ya JMT ma hivyo kuuzwa kwa nchi.

Jaji Mkuu huteua jopo la kusikilizwa rufani na anaweza kuteua majaji wenye historia ya kufinya haki za raia na kubariki dhuluma za serikali dhidi ya raia wake au anaweza kuliongoza jopo la majaji 7 ili kuhakikisha dhuluma tajwa haiwezi kuhojiwa ma kuwajibishwa ma chombo chochote cha nchi hii isipokuwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu.
 
KWANINI MADAM PRESIDENT KAMWONGEZEA MUDA JAJI MKUU KINYUME NA KATIBA?


Ukomo wa kikatiba wa utumishi wa majaji wa mahakama ya Rufaa ni miaka 65. Mheshimiwa Rais kavunja katiba pale alipomwongezea muda Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuongoza mahakama zetu hata baada ya kuvuka umri wa kustaafu.

Swali la kujiuliza ni kwanini?


Uzoefu tulionao Jaji Mkuu ana nafasi pana ya kubinya haki za wananchi na ndiyo maana anaweza kuteuliwa au kulindwa kwa udi ma uvumbi kwa minajili hiyo.

Mheshimiwa Augustine (kama alivyokuwa Jaji Mkuu)alikiuka kanuni za mahakama ya Rufaa na kuwapora jopo la majaji 3 wa mahakama hiyo kulisikiliza shauri la mgombea binafsi na akaunda jopo la majaji 7 aliloliongoza kutengua uamuzi wa mahakama kuu ulioturudishia haki ya kikatiba ya mgombea huru. Kwa ukiukwaji huu Mheshimiwa Augustine aliwapora wadaawa haki ya marejeo (Review) kama kanuni za mahakama hiyo zinavyoruhusu. Mbaya zaidi, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliutengua uamuzi wa majaji 7 wa mahakama ya rufaa pale iliposema uamuzi wao ulikuka sheria za kimataifa juu ya haki za kidemokrasia. Uamuzi huu hadi leo serikali ya CCM imeghairi kuutekeleza kwa kufuta ibara zote kwenye katiba zinazofuta haki ya mgombea binafsi.


Tuna kila sababu ya kuona Mheshimiwa Rais kakiuka katiba na kumwongezea muda Jaji Mkuu ili amsaidie kutupilia mbali haki ya kutengua Azimio la bunge ambalo limekiuka katiba.


Tunaamini Mheshimiwa Rais kavunja katiba ili jopo ambalo litateuliwa na Jaji Mkuu litasheheni majaji ambao huwa wanajulikana kwa kutoa maamuzi ya kuipendelea serikali na hata kesi haijatinga mahakama ya rufani tayari tuna orodha ya majaji ambao huenda wataisikiliza hiyo kesi ya rufani utakapowafikia.


Bila ya kuwataja majina ya hawa waheshimiwa tuna uhakika walioamua kesi zifuatazo wanaweza kupewa nafasi ya kuisikiliza rufani ya kupinga azimio la bunge:-

a) Waheshimiwa (katika hatua ya rufani na marejeo (Review) walioamua rufani ya kupinga sheria ya mafao na kusema mafao siyo mishahara na hivyo hailindwi na katiba!


b) Waheshimiwa (katika hatua ya rufani na marejeo (Review) walioamua rufani ya kupinga wakurugenzi wa manispaaa kusimamia chaguzi kinyume na katiba na uamuzi wa rufani ukaamua hakuna makosa wakisimamia ni dhahiri watakuwa kwenye jopo la kuilinda serikali ituuze mchana kweupe!


Mheshimiwa Rais kaiuka katiba ili Mheshimiwa Jaji Mkuu atumike kutupilia mbali rufani utakayofika mahakamani hapo siku za mbeleni yenye kuhoji ukiukwaji wa katiba katika mchakato wa kumpata mwekezaji ambaye ni kampuni binafsi ya Dubai kuwa ulikuwa wa kibaguzi na upendeleo, wananchi hawakushirikishwa na katiba yetu na sheria zake zimetenguliwa na kufanya zoezi zima ni kuunda mchi mpya ndani ya JMT ma hivyo kuuzwa kwa nchi.
Mwaka 2007 Jaji Barnabas Samatta alistaafu akiwa na miaka 67 mara baada ya kuongezewa miaka 2.
 
Mwaka 2007 Jaji Barnabas Samatta alistaafu akiwa na miaka 67 mara baada ya kuongezewa miaka 2.
Mnamo mwaka 2005 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba, Sheria Na. 1 ya mwaka 2005, Ibara yote ya 118 ilifutwa na kutungwa upya.

Mabadiliko hayo yaliridhiwa (assent) na Mhe Rais tarehe 6 Aprili, 2005.


Kwa minajili ya waraka huu nitanukuu ibara ya 118 (1), (2) na (3) zinazosomeka kama ifuatavyo:


“ (1) Kutakuwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani (ambaye katika Ibara zifuatazo kwenye Katiba hii atatajwa tu kwa kifupi kama "Jaji Mkuu") na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani wasiopungua wanne, isipokuwa kwamba kikao maalum cha Mahakama nzima kitakuwa kamili kukiwa na Majaji Rufani wasiopungua watano.



(2) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuwa Jaji wa Rufani na atakuwa ndiye Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 116 ya Katiba na atashika madaraka mpaka atakapotimiza umri wa kustaafu kama Jaji wa Rufani, isipokuwa kama: (a) atajiuzulu; au (b) kiti chake kitakuwa wazi kutokana na maradhi au kifo, au (c) atavuliwa wadhifa wa Jaji Mkuu na Rais.


(3) Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano zilivyoanishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua kumi miaka na tano.” [Msisitizo]



5. Kama msisitizo unavyodhihirisha, tofauti na ilivyokuwa kabla ya mwaka 2005, Ibara ya 118 (2) ya Katiba ya nchi imeweka ukomo kuwa Jaji Mkuu atastaafu atakapotimiza umri wa miaka 65 ambao ni umri wa kustaafu Jaji wa Rufani na hilo ndio kusudi la Bunge kufanya mabadiliko na si vinginevyo.


6. Ikumbukwe kuwa ibara ya 118 (2) ya Katiba inajitegemea na kusimama yenyewe au kwa maneno mengine it is a stand alone provision katika ukomo uliotajwa. Kwa hiyo, cross reference ya umri wa kustaafu kwa Jaji wa Rufani uliotajwa katika ibara ya 120 (1) ya Katiba ndicho kitu pekee kinachotakiwa kuangaliwa ili kufahamu umri wa kustaafu Jaji Mkuu ambao ni miaka 65 tu. na kwa sababu hiyo, nyongeza ya muda kwa Jaji wa Rufani haimhusu Jaji Mkuu asilani.


7. Ni bayana kuwa ukomo wa umri wa miaka 65 uliwekwa kwa makusudi ili kuondoa dhana potofu ya uchifu au usultani katika nafasi hiyo. Hivyo kwa kuwa Bunge lilimaanisha kilichomo katika Ibara ya 118 (2) ya Katiba na si vinginevyo, kitendo cha kumuongezea muda Prof. Ibrahim Hamis Juma baada ya miaka 65 kuendelea kuhudumu kama Jaji Mkuu ni sawa na kuliwekea Bunge mdomoni maneno ambayo halikusema wala kukusudia na ni uvunjaji wa Katiba.


8. Ikumbukwe kuwa, mara baada ya mabadiliko hayo, kulikuwa na mjadala mkubwa ndani ya Mahakama kuhusu uhalali wa Majaji waliotimiza umri wa kustaafu na wakaongezewa muda wa kuhudumu ikiwa ni pamoja na Jaji Mkuu. Wakati huo Mhe. Jaji Mwarija (Dean) alikuwa ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa na Mtendaji wa Mahakama kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mnamo November, 2006.


9. Mjadala huo pamoja na marekebisho ya Katiba yaliyozaa Ibara ya 118 (2), vilimuibua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika ambaye katika barua yenye Kumb. Na. JC/J.10/24/41 ya tarehe 6 Agosti, 2007 iliyoandikwa kwa Katibu Mkuu, na kunakiliwa kwa Mhe. Augustino Ramadhani (Hyt) pamoja na Ndugu Philemon Luhanjo, Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo. Katika barua hiyo, pamoja na kubainisha kuwa anayestahili kuongezewa muda wa kutumikia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji wa Mahakama Kuu, ilitamkwa bayana kuwa Jaji Mkuu anatakiwa kustaafu atimizapo umri wa miaka 65 na hastahili kuongezewa muda wowote au mkataba wa kuendelea kufanya kazi kama Jaji Mkuu. Vilevile, Mwanasheria Mkuu alieleza yafuatayo:


‘’Rais ametoa mwongozo wa kushughulikia nyongeza ya muda wa kustaafu kama ifuatavyo: Nashauri njia itafutwe kuondoa migongano ya vifungu vya ukomo wa ajira ya mikataba. Ni vema iendelee kuwepo fursa hiyo. Kwa Jaji Mkuu, naafiki pasiwepo na nyongeza ya utumishi na wala sioni haja ya kubaki Jaji wa Rufani wa kawaida, haipendezi.’’ [Msisitizo] Barua husika imeambatishwa.


10. Nilibahatika kupata nakala tajwa kupitia kwa Mhe. Jjaji Mkuu Augustino Ramadhani na ilikuwa hivyo kwa Majaji wengine waliokuwepo wakati huo. Vilevile, katika mkutano wa Majaji wote uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto, Arusha, mnamo Septemba 2007, Mhe. Jaji Mkuu Augustino Ramadhani (Hyt) alibainisha kuwa, yeye mwenyewe atastaafu katika nafasi ya Jaji Mkuu atakapotimiza umri wa miaka 65 na hataongeza hata nusu saa kwa vile Katiba hairuhusu nyongeza na akatuasa tujiandae kuwa na Jaji Mkuu mwingine.



11. Kwa kuzingatia, matakwa ya Ibara ya 118 (2) ya Katiba, ushauri uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mwongozo wa Rais kuhusu umri wa miaka 65 kuwa ni ukomo wa Jaji Mkuu kutumikia katika nafasi hiyo, Majaji Wakuu waliofuatia yaani Mhe. Augustino Ramadhani na Chande Othman Chande ambao kwa uaminifu mkubwa kabisa na kwa kuzingatia viapo vyao, wote wawili, walitii na kuhesimu Katiba na kustaafu kwa heshima walipofikisha umri wa miaka 65.



12. Ikumbukwe kwamba, opinion ya Mwanasheria Mkuu kuhusu ushauri wake hususan jambo tajwa, ndiyo msimamo wa Serikali kama inavyoelezwa na kifungu cha cha 23 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kinachosema:



“ 23 (1) The opinion of the Attorney General given pursuant to the provisions of subsection (2)of this section shall remain the legal position of the Government on the matter unless it is otherwise revised by a court of competent jurisdiction, the
 
Mwaka 2007 Jaji Barnabas Samatta alistaafu akiwa na miaka 67 mara baada ya kuongezewa miaka 2.
Mnamo mwaka 2005 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba, Sheria Na. 1 ya mwaka 2005, Ibara yote ya 118 ilifutwa na kutungwa upya.

Mabadiliko hayo yaliridhiwa (assent) na Mhe Rais tarehe 6 Aprili, 2005.


Sasa tusaidie barua ya kuongezewa miaka 2 ikionyesha tarehe kamili ya kuongezewa mkataba kama ilifanyika kabla ya tarehe 6 Aprili, 2005 wakati mabadiliko tajwa yaliridhiwa na Rais ingawaje hata kama ilikuwa baada ya kuridhiwa na Rais haitengui ukweli ya kuwa Madam President kakiuka katiba na haheshimu utawala wa kisheria kwa kumwongezea muda Jaji Mkuu
 
Mnamo mwaka 2005 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba, Sheria Na. 1 ya mwaka 2005, Ibara yote ya 118 ilifutwa na kutungwa upya.

Mabadiliko hayo yaliridhiwa (assent) na Mhe Rais tarehe 6 Aprili, 2005.


Sasa tusaidie barua ya kuongezewa miaka 2 ikionyesha tarehe kamili ya kuongezewa mkataba kama ilifanyika kabla ya tarehe 6 Aprili, 2005 wakati mabadiliko tajwa yaliridhiwa na Rais ingawaje hata kama ilikuwa baada ya kuridhiwa na Rais haitengui ukweli ya kuwa Madam President kakiuka katiba na haheshimu utawala wa kisheria kwa kumwongezea muda Jaji Mkuu
Mbona unarukaruka? Mabadiliko hayo yamefanyika kabla au baada ya Samatta kuongezewa muda? Usijitoe akili
 
Hizi ni khoja za upotoshaji.

Kwani hatuwezi kuwaondoa wachuuzi wa ICDs na TPA wakasimamia na kuziendesha na kuliongezea taifa hela?



Jambo hili ni zito na wahusika ni wazito na wanaogofya sana ndiyo maana wengi wanaogopa kuwataja na kuwasema hadharani. Wanawaogopa kwa kuwa wana uwezo mkubwa sana wa fedha na kuingilia mambo yao wanaweza kukuuwa! Lakini sisi tunasema hakuna mwamba zaidi ya YESU na leo tunawaletea magwiji ya rushwa na wizi yaliyo nyuma ya vurugu za uwekezaji bandarini.

Wamiliki wa ICDs(Inland Container depots) yaani bandari za nchi kavu ndiyo chanzo cha hizi vurugu wakiongozwa na Kinana, Ally Awadh na GSM.

ICDs zifuatazo zinakwenda kuathirika sana na kufutwa kabisa kwa ujio wa DP World kwa sababu atatumia bandari kavu ya Kwala ambayo ni ya serikali kutunza makontena yote.

1. African Inland Container Depot
2. Said Salim Bakhresa
3. AMI Tanzania Ltd
4.Farion
5.Dar Es Salaam Inland

ICDs hizi ni wanufaika wa karibia jumla ya 4tr TZS kwa mwaka zinazokusanywa kama tozo za kutunza makontena hayo. Hela hiyo inaingia kwenye mifuko ya akina Kinana,GSM ,Ally Awadh na wenzao.

Maamuzi ya kuwandoa TICTS kuendesha bandari yetu hayakuwa rahisi na kwa vyovyote vile upinzani huu ulitarajiwa kwa kuwa hakuna serikali iliwahi kuwa na uthubutu na kufanya maamuzi magumu kiasi hiki ambayo marais wengine wameshindwa kuyafanya kwa miaka 25 ya utendaji mbovu na wa hovyo wa TICTS.

Ikumbukwe TICTS ndiyo wenye kufanya makubaliano na ICDs hizi kutunza makontena hayo ya mizigo na kunyonya watanzania

Tunajua nyuma ya haya wako mapapa kina Karamagi, Kinana, GSM, Bakhresa, AlHushuum, Farion na wamiliki wengine wa ICDs( Inland Container Deports), hawa ndiyo wanufaika wakubwa wa utendaji mbovu wa TICTS hapo bandarini kwa sababu wanachelewesha kuondosha makontena kwa makusudi kwa kushirikiana na maafisa wa TRA na TICTS ili tu wateja watozwe charges za kutolea container (ambazo ni kati ya dola 1,200- dola 1,500 kwa kila kontena moja) zao na ndiko ambako wananyonya watanzania hizo 200bn TZS kwa mwezi

Kwa mwezi hizi ICDs zinalipwa zaidi ya 200bn TZS ambazo ni karibia 4tr TZS kwa mwaka. Hizo ni fedha nyingi sana kwenda kwenye makampuni ya akina Karamagi, GSM, Bakhressa, Farion, Kinana, na AlHushoom na wengine, ndiyo maana hawataki kwa vyovyote vile DP World waje kuwekeza maana wameweka wazi kuwa watatumia depot ya Kwala ICD ambayo ni ya serikali na kubwa kuweza kuhimili makontena idadi yoyote yatakayoshushwa bandari ya Dar Es Salaam na hivyo hakuna haja ya ICDs hizi za akina Kinana na GSM.

Katika hali hii lazima watu hawa waweke upinzani na kukwamisha mambo haya kwa kuwa biashara yao ya ICDs inakwenda kufa na fedha zaidi ya 200bn TZS kwa mwezi zitakuwa zinaingia serikalini na zitakwenda kunufaisha watanzania wengi tofauti na hali ilivyo sana fedha hizo zinaingia kwenye mifuko ya mapapa akina GSM, Karamagi, Kinana, Farion, AlHushoom, na wengine.Kwa vyovyote vile ujio wa DP World hauwezi kuwafurahisha hawa mapapa maana mirija ya unyonyaji wanaoufanya hapo bandarini unakwenda kukatwa milele.

Leo mkulima wa parachichi kule Njombe analipa $8,000 kusafirisha container kutoka Njombe kwenda Mombasa ili kusafirisha kwenda Ulaya kuuza kwa kuwa Dar es Salaam hakuna cold storage na TICTS miaka yao 25 yote wameshindwa kujenga hata cold storage moja. Mkulima anayelipa $8,000 kupeleka kontena lake la parachichi Mombasa angelipa $3,500 kama angesafirishia Dar Es Salaam lakini haya yote wakosoaji hawayaoni na hawawezi kuyasema kwa sababu wanajua ukweli wake. Leo anakuja DP World anataka kujenga hizi facilities watu hawataki na wanakomaa na hoja zisizo na maana na msingi kisa tu mapapa akina GSM, Kinana, Karamagi , Bakhressa, Kinana, Farion, AlHushoom wamewapa hela kuvuruga uwekezaji huu.

Nani ambaye hajui miaka ya nyuma wakati wa utawala wa awamu ya 4 kampuni ya Home Shopping Centre sasa GSM yenye ubia na aliyekuwa mke wa Rais huyo walivyokuwa wanapitisha mamia ya makontena bandarini bila kulipa ushuru? Nani hajui hata leo hii ni kiasi gani cha ushuru unakwepa na watu hawa hasa GSM?Nani hajui makontena yanapitishwa na kukwepa ushuru kupitia hizi ICDs zao?

#KigogoMediaUpdates
 
Kama yaliridhiwa 6 APRIL kwanini JULY 20 JAJI SAMATTA HAKUSTAAFU?
Kwa hiyo, khoja yako ni kuwa na pamoja hujatubandikia nakala ya barua kuthibitisha hoja yako unatetea uvunjifu wa katiba kwa sababu ulishawahi kufanyika?


Kama hii ndiyo khoja yako basi tuna tatizo kubwa.

Ukimdaka mwizi leo akijitetea mbona jana mwenzangu aliiba hakumkamata basi mniachie


Nakuona ukiwa hakimu utamwachia
 
DP WORLD debt structure more than $25 Bill mostly owned by western banks.

So, DP WORLD is part of global financial banking system to own global natural resources, and Tanzania is just a paw in this elaborate plan.

No wonder western countries have embraced DP WORLD because it is indebted by their banks whose plans is total control of global natural resources
PSX_20230702_232216.jpg
 
Problem with DP WORLD is losing money, and will use this IGA to borrow even amore, darting hopes of soft landing.
DP WORLD not a cash cow as others have been trumpeting it is looking to poor nations to absorve her colossal losses


And, TZ is more than willing to be part of this sinking TITANIC SHIP.
IMG-20230702-WA0012.jpg
 
Well, it is the way the cookie crumbles.


DP WORLD is broke and needs the cooperation of extremely venal sub saharan politicians to bail it out with these IGAs, which essentially has given the DP WORLD a new lease of commercial relief. Armed to teeth with these IGAs, DP WORLD can pay a courtesy visit to Western lenders and secure more extortionate loans. Otherwise, DP WORLD was looking forward to declaring bankruptcy, but that call is only deferred for now as we shall dilate here.


Survival in this business jungle calls for more borrowing at exorbitant rates since the interest rate regime has skyrocketed in an elusive attempt to lean in on runaway inflation. Honouring loan repayment, particularly outsized interest rates, is the DP WORLD well kept secret. The gospel truth needs revelation: DP WORLD corporate plan falls apart because of the onerous debt payment obligations beyond their means.

Lending huge amounts of cash is unavoidable to anchor new expansionist regimes across sub-Saharan Africa to extend port operation services that may require significant concessions that will erode on revenue sources and associated profits.

Without profits, it means someone has to pick up the rotten end of the stick. The western banks bankrolling DP WORLD will not take any losses, and DP WORLD will shirk away leaving the bewildered host African countries who are at the end of the conveyor belt finding themselves tied to IGAs which are generating losses, and they cannot extricate themselves from this latest slavery without attracting huge penalties of contract termination.

Part of the challenge DP WORLD will have to confront is how either to absorb or eliminate local fiefdom that have already tasted easy money from running dry land ports. These political influence peddlers may make or break DP WORLD ironclad hold on this port operations.


Cooperating with the well politically connected fiefdom means sharing of the meager profits that will strangle DP WORLD and that will be very bad tidings to the Exchequer who is eagerly awaiting to report to the Parliament that the biggest political gamble since independence has worked but regrettably he will have to divulge it had backfired.

Refusal to "pay to play" DP WORLD will find themselves losing political influence to their own detriment. Either way, we see no future for the money guzzling DP WORLD and to those who promoted it as that silver bullet, which is anything else but that!


When everything is looped into the equation, DP WORLD basic problems will not vanish away because they have these IGAs across sub-Saharan Africa knowing debt servicing is well beyond the money generated by these anemic operations ensnaring her even into a more debt trap. The reality will sink in to balance the books these satellite African nations, including empty-headed TZ, ought to absorb the losses. No money will pass hands, making TPA look like the mighty Archangel we barely knew and appreciated despite the enormous challenges it endured that excludes not political interference.

This is where the habitual lies of turning our ports into money minting machines will come into a cropper, and no amount of lies will cool the anger of the populace. Like all alien investments in this country that have floundered, DP WORLD will be no exception, and our politicians will have no place to hide just like a golden fish.

This will be a bitter medicine to swallow because the IGAs protect the investor under any circumstances, including fleecing the host nation on the very broad daylight. The clock is now quietly ticking....

Then, someone in the government will be compelled to be a fall guy, as the expected revenues fall short of ballooned figures. In fact, we anticipate the first three years DP WORLD cash to the Treasury will be less than what TPA sends!

Next year, they will claim they are still resolving teething issues following the handover, but the second year excuses will be difficult to justify when not a penny is paid to the Treasury. DP WORLD will later ask for government subsidy and bank guarantee for new loans to bankrolling other petty projects elsewhere


Who will be our FALL GUY?

We project the DP WORLD saga gonna be the biggest DECEPTION since we gained independence.

We are selling our gems to a company running colossal losses, hugely indebted, and the debts will mount to over $50 bill within the next five years to accommodate the largest port expansion operations in global history.


Just remember, DP WORLD is broke and borrows money from the western banks to make ends meet. The question for how long before this house of cards comes down tumbling? We suspect it may take two to three years from now before our dumb politicians learn how to spell "OUCH" the hard way.


WHAT IS THE REAL PROBLEM OF DP WORLD?


The massive debt, which can not be repaid and has been restructured a couple of times, is now slapped with hiked interest rates. The failure of meeting financial obligations makes DP WORLD a very unreliable as the mega infrastructure international investor of the magnitude envisioned globally.


We are now in a position to make our own considered projection.


DP WORLD is going to turn out as the biggest ponzi scheme since Bernie Madoff: the monster of Wall Street. It is a house of cards that will fall with a domino impact, leaving sub-saharan countries sinking deeper into external debt that may lead at disposing our natural resources to plug the gaping holes into our national budgets



What our scatterbrained politicians do not know the shares they were bribed with are duds, and they will never be able to cash in on them because western banks must collect their interest payments before anybody else thereafter there will be nothing for them to pick up.

In fact, the duds they cling to dearly are worthless than toilet paper, which at least you know you can wipe your ass with.

This is God's will that His enemies amass wealth to hand over to the guiltless. It is God's doing, and it is wonderful in our eyes, says the Lord God of Jacob.

IMG-20230702-WA0014.jpg
 
Back
Top Bottom