Never outshine the master

Never outshine the master

Scott junior

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2022
Posts
2,600
Reaction score
3,640
Sheria ya 1 ya kutoka kwenye kitabu cha "48 Laws of Power" kilichoandikwa na Robert Greene inasema "Never Outshine the Master" yaani kamwe ( Usiwahi kumfunika bosi wako)

Kamwe usijaribu kuonekana una akili, uwezo, au mafanikio zaidi ya mtu aliye juu yako, iwe ni bosi wako kazini, kiongozi, au mtu yeyote mwenye mamlaka juu yako. Lengo ni kuhakikisha kuwa huleti hofu, wivu, au hisia ambazo zitaonekana ni tishio kwako.

Watu wengi walio kwenye madaraka mara nyingi huwa na hofu ya kupoteza nafasi yao. Ukijaribu kuonyesha kuwa wewe ni bora kupita wao, hata kwa nia nzuri unaweza kuwafanya wajihisi kuwa wewe ni tishio na hatimaye watafanya kila jambo kukuangusha chini.

Mfano: Kama mfanyakazi, ukimfanya bosi wako aonekane hana uwezo mbele ya watu wengine (kwa mfano kwa kujibu maswali vizuri zaidi kwenye mkutano au kuonyesha maarifa mengi zaidi), huenda ukadhani unajionyesha kuwa una uwezo. Lakini bosi wako anaweza kuona kama unajaribu kuchukua nafasi au kumuaibisha na hilo linaweza kukuharibia

Unachotakiwa kukifanya, Fanya bosi wako aonekane mzuri na mwenye mafanikio. Kama kuna mafanikio, fanya aonekane kuwa yeye ndiye chanzo, hata kama wewe ndiye ulifanya kazi kubwa.

Epuka sifa nyingi mbele za watu, Maana sifa huleta hila, Tumia akili zako vizuri lakini usizitumie kumfanya mwingine aonekane mdogo. Tumia busara na hekima ya kijanja.

Haitakiwi kueleweka kama unapaswa kuwa mdogo au mjinga, bali kuwa mwerevu na mjanja, kuelewa nafasi yako, kujua ni lini uonyeshe uwezo na lini ukubali kutoa heshima hata kama unajua unaweza zaidi.
 
Tatizo ni watu ni wavivu sana wakufikiri, mwisho wa siku wamechukua hichi kitabu cha Robert Green 48 Laws kama msahafu vile.

Wewe fanya unachotakiwa kufanya kulingana na mazingira yako, hiyo kanuni ni juhudi za kuendelea kujaza wanafiki na watu waoga duniani ndio maana kuna kitu kinaitwa mapinduzi
 
My take you can win your master by considering the 3rd law "CONCEAL YOUR INTENTION”

NB;I mean to win and not to outshine since in order to outshine a master he must be your master by the time you exceed the dice,Remember that time h’s still a coach
 
Back
Top Bottom