Peter umeongea vizuri lakini kuna mambo madogo tu unatakiwa ujue,kwamba tunaposema hauhitaji mtaji maanake ni kwamba ukiangalia unachotakiwa kutumia na kuuza ili kufikisha point za mwezi ni kidogo sana,unahitaji kama wateja watano kwa mwezi upate minimum points.Hao wateja ni ndugu zako,marafiki,jamaa,wafanyakazi wenzio ama kwa lugha rahisi ni watu unaokutana nao katika mizunguko yako ya shughuli za kawaida,na unachofanya unamweleza mtu bidhaa uliyo nayo akikupa order unaenda kumchukulia,je unafikiri mtaji wa kununua product 2/3 ni shs ngapi? ni sawa na tukisema haihitaji mtaji.
Pia kabla hujajiunga na hizi kampuni lazima uangalie mambo muhimu, hii ni biashara ambayo inawaconnect wateja manake kwa kuingia wewe unakuwa mteja hivyo basi lazima bidhaa ziwe consumables ambazo utakuwa ukizihitaji mara kwa mara,pia angalia kiingilio kiwe cha chini,kama wanatoa product package hizo bidhaa wanakuchagulia au wewe unachagua mwenyewe.Ukiangalia mfumo jinsi ulivyo unasema kwamba wakati mwingine kuuza si lazima kwa sababu kama umeingia kwenye kampuni ambayo ina bidhaa nyingi ambazo unazitumia katika maisha yako ya kila siku hizo minimum points utazipata kutokana na matumizi yako tu hivyo kuuza inakuwa option... mfano kampuni ninayofanya mimi kupata minimum points unaweza nunua vitu vya kama shs 100,000,kama malipo yangu kutoka kwenye hii biashara yanazidi hiyo kuna ubaya gani kununua bidhaa za thamani hiyo?ukumbuke hii na part time halafu inakuwa kadiri ninavyowasaidia wengine kukua.Na kama hayafikii hapo unatafuta wateja ambao watanunua products ufikie malengo huko baadae malipo yatakua.
Sasa kuna kuna makampuni mengine viingilio viko zaidi ya usd 400 hadi 1000 sasa kwa hapa tutasema ni mtaji manake si watanzani wengi wenye vipato vya kufika huko.
Mimi huwa napenda kumuuliza mtu hivi, kama unatumia sabuni,mafuta ya kijipaka na kadhalika,na wakati mwingine ungehitaji food suppliment na hivi vitu unanunua labda dukani kwa mangi au supermarket.....je?itakuwaje haya manunuzi ukayafanya kupitia biashara ya mtandao ambapo mwisho wa mwezi utalipwa? kwani matumizi yako yanahesabiwa kama mauzo uliyoyafanya kwa mwezi huo.Pia mjue unaweza kukua ukawa unalipwa fedha nyingi sana lakini si kwa kuingiza watu wengi sana bali kwa kuingiza watu na kuwafundiha namna ya wao kuingiza watu,imagine kama kila anayeingia atafundishwa jinsi ya kuingiza watu na akafanya hivyo ujue baada ya muda fulani idadi itaenda kwenye maelfu na malaki