NENO: Nakulaga, nakimbiaga, nachekaga, nipo bajajini Ni sahihi?

Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,058
1,099
Habari zenu walimu wangu wa jukwaa hili..
kuhusiana na maneno hapo juu, je ni sahihi kuyatumia? maana ni mazoea ya watu wengi sasa nikiwemo mimi huwaga napendaga kuyatumiaga
 
Kiswahili sahihi ni "huwa ninakula" n.k. Lakini naona hicho Kiswahili cha ninakulaga karibu kitahalalishwa.
 
Watu tunaongea kilugha tukidhani ni kuswahili fasaha, hakuna kiswahili cha ga mwishoni.

Hivi fugo kwa kiswahili ni nini? Nimekuja mjini na gari la kabeji lakini bado sijajua neno hili.
 
umeona eeh kumbe hata wewe katika sentensi zako huwaga unatumia ga
 
Alafu siku hizi ndio imekuwa utaratibu na kinachosikitisha mpaka radio zetu watangazaji wanayatumia sana haya maneno (ukichanganya siku hizi hawatangazi bali vipindi vingi ni wanaongea, kunakuwa hakuna script wala mwongozo wowote mtu anatamka na mwisho wa siku nchi nzima inaingia kwenye huu uongeaji)

Huongeaji wa namna hii tulikuwa nao watu tuliotoka huku Imalamakoye, Ihayabuyaba na kule Sikonge, na ilikuwa ukizungumza unachekwa kweli unaonekana wa wapi sasa siku hizi kila mtu.
 
Last edited by a moderator:
Watu tunaongea kilugha tukidhani ni kuswahili fasaha, hakuna kiswahili cha ga mwishoni.

Hivi fugo kwa kiswahili ni nini? Nimekuja mjini na gari la kabeji lakini bado sijajua neno hili.
Kweli kilugha hiki, Hapa wametuenzi aisee maana ndio zetu hizi wenyeji wa kuanzia Tabora, Shy, MZA, Geita na ilikuwa ukiongea hivyo lazima kuna mtu atakurekebisha au atajua umeshuka leo kutoka Nyang'homango, ajabu siku hizi imekuwa common mpaka inasikitisha tena wengine wanapenda kutumia neno "tangia" badala ya "tangu"
 
Nahisi hata walimu wa kiswahili wameisha, shuleni kulikuwa na mabango kabisa, 'ongea kiswahili'.

Kule Ihayabuyaga ilikuwa kawaida, lakini ukija mjini watu watakukosoa, walau na shuleni tulikuwa tunakosolewa hadi tunafahamu. Siku hizi kila kitu 'heregeni'

Kweli kilugha hiki, Hapa wametuenzi aisee maana ndio zetu hizi wenyeji wa kuanzia Tabora, Shy, MZA, Geita na ilikuwa ukiongea hivyo lazima kuna mtu atakurekebisha au atajua umeshuka leo kutoka Nyang'homango, ajabu siku hizi imekuwa common mpaka inasikitisha tena wengine wanapenda kutumia neno "tangia" badala ya "tangu"
 
Alafu siku hizi ndio imekuwa utaratibu na kinachosikitisha mpaka radio zetu watangazaji wanayatumia sana haya maneno (ukichanganya siku hizi hawatangazi bali vipindi vingi ni wanaongea, kunakuwa hakuna script wala mwongozo wowote mtu anatamka na mwisho wa siku nchi nzima inaingia kwenye huu uongeaji)

Huongeaji wa namna hii tulikuwa nao watu tuliotoka huku Imalamakoye, Ihayabuyaba na kule Sikonge, na ilikuwa ukizungumza unachekwa kweli unaonekana wa wapi sasa siku hizi kila mtu.

duh basi ni ugonjwa wa taifa
 
Last edited by a moderator:
Kweli kilugha hiki, Hapa wametuenzi aisee maana ndio zetu hizi wenyeji wa kuanzia Tabora, Shy, MZA, Geita na ilikuwa ukiongea hivyo lazima kuna mtu atakurekebisha au atajua umeshuka leo kutoka Nyang'homango, ajabu siku hizi imekuwa common mpaka inasikitisha tena wengine wanapenda kutumia neno "tangia" badala ya "tangu"

Hivi hili nalo tutalaumu utandawazi kweli? Kwa wakati mwengine naona matumizi ya misamiati hii ni kusudi za mtu binafsi.
Ila kwa mbaali unakuta kuna umahili, mazingira na kujikweza ndani yake mpaka mtu anazungumza hivi. Kwa mfano mtu anapotamka "tangia" badala ya "tangu" ni dhahiri kuna kujibwetesha katika matumiz ya lunga na kukiuka kaida zake.
 
afu hili neno "Tangia" instead of "tangu" linatumika sana had wakenya wametuiga dah!! tunaitangaza lugha vibaya, utashangaa hata wazungu wa hapa wataanza kuyatumia dah!!

Hivi hili nalo tutalaumu utandawazi kweli? Kwa wakati mwengine naona matumizi ya misamiati hii ni kusudi za mtu binafsi.
Ila kwa mbaali unakuta kuna umahili, mazingira na kujikweza ndani yake mpaka mtu anazungumza hivi. Kwa mfano mtu anapotamka "tangia" badala ya "tangu" ni dhahiri kuna kujibwetesha katika matumiz ya lunga na kukiuka kaida zake.
 
Sioni ubaya wowote kama matumizi ya neno "ga" yakirasimishwa kwenye lugha ya kiswahili. Kwa hatua tuliyofikia ni itakuwa ni vyepesi zaidi kulikubali kuliko kulizuia.
 
kinachotakiwa ni kuunda misamiati mipya kutokana na uhitaji wake na sio kuongeza viambishi katika misamiati iliyopo.

Kwa mfano "alienda" utakaposema "aliendaga" itakuwa na maana gani mpya ambayo tunaihitaji katika lugha yetu?
 
Wazungumzaji huwa na kawaida uvivu yaani hupenda matumizi ya maneno yaliyo marahisi mfano mtu badala ya kusema "huwa anakuja" atasema tu neno moja "anakujaga" pia kuhusu "bajajini" ni sahihi ila sijajua "bajaji" ni sahihi kwa ujumla "bajajini" kwa upande wangu ni sahihi kwa sababu ni neno linaloelezea ndani ya bajaji.Kwa hiyo,hayo matumizi ya "-ga" kwa sasa si sahihi ila inaweza kuja kutumika kadri muda unavyokwenda
 
Back
Top Bottom