Neno 'limited' lina maana gani kibiashara?

Pangah2011

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
260
208
Hivi neno limited lina maana gani kibiashara au pale mtu anapolitumia kwenye kampuni yake? Je, ili kuweka Ltd kitu gani kinahitajika?

Naombeni jibu kwa wenye uelewa wa hilo jambo.
 
Kampuni zenye majina hayo. kwanza zinamilikiwa kwa share (pertnership)sina uhakika na 'spelling' ya watu zaidi ya wawili, nazani kuanzia saba, pia huaminiwa ktk mikopo, kampuni hubeba zamana ya mikopo yake na sio wamiliki kama ilivyo ktk sole proprietership
 
Hivi neno limited lina maana gani kibiashara au pale mtu anapolitumia kwenye kampuni yake? Je, ili kuweka Ltd kitu gani kinahitajika?

Naombeni jibu kwa wenye uelewa wa hilo jambo.

Neno limited(ukomo) linatumika mwishoni mwa jina la kampuni kuonyesha kwamba madeni ya wanahisa hayatazidi thamani ya hisa za wanahisa( the liability of members of the company are limited to a state amount) .Hasa kampuni inapofilisika kama itashindwa kulipa madeni ya creditors ninyi wanahisa(shareholders) hamtalazimika kutumia Mali zenu binafsi kuwalipa wanaoidai kampuni. Tofauti na partnership(ubia) na sole proprietorship(biashara ya MTU mmoja) ni kwamba kampuni inafahamika kama MTU(a company is a corporate body, I.e it is created under law and has an entity of its own, quite separate from the members that comprise it. This is a very important difference and is in fact the main reason for the popularity of this form of ownership). Kwa kuongezea in kwamba mahakama inaitambua kampuni kama MTU kisheria ambaye anaweza kuingia mikataba, akashitaki na akashitakiwa, akakopa, akamiliki Mali na kufanya chochote ambacho ndicho kilichokusudiwa wakati Wa kuanzisha kampuni. Partnership and sole traders hawatumii ltd kwa sababu huwezi kumtenganisha mmliki na biashara take na kwa hiyo biashara ikifilisika atalazikia kutumia Mali zake binafsi ili awalipe wanaoidai biashara yake. Samahani kwa mahali popote ambacho sijaeleweka au sijaweka maelezo vizuri mkuu ila bila shaka utapata mwanga kidogo.
 
Ili uweze kutumia neno ltd kwenye jina la biashara yako ni lazima ubadili biashara yako iwe kampuni. Kila unapoona sehemu jina biashara na mwishoni mwa jina kuna ltd ujue hiyo ni kampuni.
 
Maana yake ni Limited liabilities, yaani madeni ya kampuni ni ya kampuni na sio ya wamiliki so kampuni ikichukua mkopo kwa mfano ikashindwa kulipa hawawezi kuja kupiga mnada nyumba za wenye kampuni. Of coz hapa ni kama haukuweka vitu vyako binafsi kama collateral wakati unaomba huo mkopo.

Kuna wakati mahakama inaweza kuamua kuondoa ulinzi huu wa limited ikiona ulitumika vibaya.
 
Ili uweze kutumia neno ltd kwenye jina la biashara yako ni lazima ubadili biashara yako iwe kampuni. Kila unapoona sehemu jina biashara na mwishoni mwa jina kuna ltd ujue hiyo ni kampuni.

Je kwenye saccos naweza kuitumia neno limited?
 
Ili uweze kutumia neno ltd kwenye jina la biashara yako ni lazima ubadili biashara yako iwe kampuni. Kila unapoona sehemu jina biashara na mwishoni mwa jina kuna ltd ujue hiyo ni kampuni.

Mwanga umenijia ila haujani kaa kikao kikamilifu, sina budi kuku Shakuru. Asante
 
Nmejifunza kitu ila naomba pia kuongezwa kitu, ni vigezo gan vinahusika ili biashara ipewe hadhi ya kua kampuni(ltd) ukiachilia mbali idadi ya wamiliki?
 
file:///C:/Users/Kijito/Desktop/BRELA-Company%20Registration.html. na ili upate nondo zaidi,jukwaa la ujasiriamali pale bila shaka pana vitu vizuri,pana elimu tosha kabisa
https://www.jamiiforums.com/ujasiri...i-katika-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania.html. bila shaka ukisoma hapo huwezi kutoka kama ulivyoanza kusoma mkuu. http://www.brela-tz.org/services.php
 
A word limited is a legal shield to protect the fortune of one bussiness to be affected by the miss fortune of another business in case of liability or forced liquidation of a firm.
 
Nmejifunza kitu ila naomba pia kuongezwa kitu, ni vigezo gan vinahusika ili biashara ipewe hadhi ya kua kampuni(ltd) ukiachilia mbali idadi ya wamiliki?

Unatakiwa kufanya search name,jina likipita Brela unaandaa Mermat(Katiba),then utafute wakili kwa ajili ya mhuri,kampuni lazima ianze na wana share wawili
 
Neno limited(ukomo) linatumika mwishoni mwa jina la kampuni kuonyesha kwamba madeni ya wanahisa hayatazidi thamani ya hisa za wanahisa( the liability of members of the company are limited to a state amount) .Hasa kampuni inapofilisika kama itashindwa kulipa madeni ya creditors ninyi wanahisa(shareholders) hamtalazimika kutumia Mali zenu binafsi kuwalipa wanaoidai kampuni. Tofauti na partnership(ubia) na sole proprietorship(biashara ya MTU mmoja) ni kwamba kampuni inafahamika kama MTU(a company is a corporate body, I.e it is created under law and has an entity of its own, quite separate from the members that comprise it. This is a very important difference and is in fact the main reason for the popularity of this form of ownership). Kwa kuongezea in kwamba mahakama inaitambua kampuni kama MTU kisheria ambaye anaweza kuingia mikataba, akashitaki na akashitakiwa, akakopa, akamiliki Mali na kufanya chochote ambacho ndicho kilichokusudiwa wakati Wa kuanzisha kampuni. Partnership and sole traders hawatumii ltd kwa sababu huwezi kumtenganisha mmliki na biashara take na kwa hiyo biashara ikifilisika atalazikia kutumia Mali zake binafsi ili awalipe wanaoidai biashara yake. Samahani kwa mahali popote ambacho sijaeleweka au sijaweka maelezo vizuri mkuu ila bila shaka utapata mwanga kidogo.

Naweza fungua saccos ikaishia na neno ltd?
 
Yes unaweza! Provided saccos husika inafunguliwa kwa misingi ya kampuni (chini ya sheria ya makampuni Sura no. 212 kama ilivyorejewa 2002!

Kumbuka, huwezi kufungua saccos peke yako yaani mtu mmoja!
 
Kuanzisha saccos hadi inakamilika usajili inaweza ika gharimu sh ngapi? Kikundi kina takiwa kisiwe na chini ya shilingi ngapi ili kiweze kianze.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom