Neno La Leo: Nchi Ya Wanaopigana Vinyundo Na Kurushiana Vijembe!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

SIKU hizi imekuwa ni ‘ burudani’ kusoma magazeti, kusikiliza redio na hata kutazama televisheni. Maana kuna habari ambazo ni ‘ vituko’ vya uchaguzi haswa. Ni vioja. Na kila kukicha Afrika, kunazuka kioja kipya, ilipatwa kusemwa.
Jana nimesoma mgombea ubunge anatamka hadharani; ‘ Niko fiti, anayebisha aende akamwulize mke wangu!’
Katika hilo hata hoja za msingi zinazopaswa kuzungumzwa katika wakati kama huu wa kampeni zinawekwa kando. Ni ‘ vijembe’ kwa kwenda mbele. Mathalan, kwenye gazeti la Uhuru ( pichani), Jumamosi Septemba 4 kuna kibonzo kilichoniburudisha. Jamaa amekwenda Kituo cha Polisi na kuripoti; anasema, “ Amenitupia vijembe vikali sana wakati akifanya kampeni!”. Polisi naye akamjibu kwa kumwuliza; “ Mipini ya hivyo vijembe umekuja nayo nayo ili viwe ushahidi?”
Ni katika nchi hii utasikia mtu analalamika ‘ anapigwa vinyundo’ na wenzake. Na kuna hata gazeti limesajiliwa kwa jina la ‘ Nyundo’.
Na kwanini tushangae, kwenye nchi ya Wakulima na Wafanyakazi wenye kutumia zana zile zile za enzi na enzi; vinyundo, vijembe , vinyengo na vinginevyo. Ukiwaona wanagombana wanarushiana hivyo hivyo, maana ni vyepesi. Nawe usikae ukapoteza muda kushabikia ugomvi wao. Ni ndugu hao, chukua lako jembe ukalime. Wakipatana, chukua lako kapu ukavune. Na hilo ni Neno La Leo.


mjengwa
0788 111 765
 
Back
Top Bottom